Monday, May 23, 2011

LUGHA YA KISWAHILI ITUMIKE KUONYESHA UZALENDO - DKT. NCHIMBI

 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt  Emanuel Nchimbi amesema lugha ya kiwsahili itumike kuonyesha uzalendo wa Mtanzania.Lugha ambayo itamsaidia mtanzania kuwasiliana na mwenzake kiurahisi,watu watumie kiswahili kwenye ngoma,maigizo,michezo,mashairi,ngonjera,nyimbo.Dkt Nchimbi alitoa mifano kuwa kama kuna timu yetu inacheza na timu ya nje watu wanaishangilia timu hiyo,alisema huo ni ukosefu wa kinga ya uzalendo.
Dkt Nchimbi alisema hayo wakati wa kufungua kongamano la kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo.Alisema Lugha ya kiswahili ndiyo inayomwonyesha mtanzania na utamaduni wake.

Wanafunzi wajenge tabia ya kujifunza lugha ya kiswahili kwa kusoma vitabu mbalimbali,ili kukuza misamiati ya kiswahili,miundo,mbinu na tamathali za semi.

No comments:

Post a Comment