Tuesday, May 3, 2011

MIMBA 1,027 MKOANI RUVUMA ZIMEKATISHA MASOMO WANAFUNZI WA KIKE MWAKA JANA

AFISAELIMU wa mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo mwenye suti ya mistari anamkabidhi taarifa ya elimu ya mkoa huo Naibu Waziri wa nchi Elimu TAMISEMI Mhe.Kasimu Majaliwa kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma baada ya kuisoma.

Bibi Mkonongo katika taarifa yake alisema kikwazo kikubwa cha kushusha kiwango cha taaluma mkoani Ruvuma ni pamoja na utoro sambamba na watoto wa kike kupewa mimba,alizitaja mimba hizo kuwa ni pamoja na mimba 1,027 kati ya hizo mimba 912 ni kwa wanafunzi wa shule za msingi na mimba 115 ni kwa shule za sekondari.

Alisema hakuna ushirikiano wa kutosha baina ya wazazi na walimu katika kuwachukulia hatua za kinidhamu wanaowapa mimba wanafuzni,kwa kuwa wazazi wanawaficha wanaotia mimba hizo,Iwapo ushirikiano ungekuwepo wa kutosha wa serikali za mitaa , vijiji na polisi vitendo vya watu kuwapa mimba wanafunzi ungekoma.

No comments:

Post a Comment