Saturday, May 21, 2011

MWANAFUNZI KUMPANGIA NYUMBA MITAANI ATASOMA KWA MAKINI ?

 Inasikitisha sana kwa vitendo ambavyo wanafunzi waliopangiwa mitaani ili wawe karibu na shule,baadhi ya wapangishaji wa nyumba hizo kuwaona wanafunzi hao kama watu wazima hasa kwa wasichana kwa kuwataka kimapenzi ndani yao hata walimu wakawamo.Je huo ni ungwana ? kumfanyia hivyo mtoto wa menzako,ua ule usemi wa mtoto wa mwenzako ni wako ulipitwa na wakati?
Huyu mwanafunzi aliwaambia wenzake kuwa yeye ada ya shilingi  20,000 anajitafutia mwenye baada ya kutoka shuleni,huchukua madumu ya maji na kuyauza kwa kutumia baiskeli,basi huwa anachoka sana hata akifika shuleni hata mwalimu hawezi kusikiliza vyema.

1 comment:

  1. Huu ni ufisadi wa kutisha. Hao wanaoitwa waalimu wanafedhehesha hadhi ya ualimu, ambayo ina maadili ya pekee. Niliposomea ualimu, Chuo Kikuu Dar es Salaam, 1973-76, nilifundishwa kuwa mwalimu anashika nafasi ya mzazi. Inaudhi kwamba mafisadi hao waliojificha mashuleni wanaitwa waalimu.

    ReplyDelete