Friday, September 30, 2011

RAIS KIKWETE AWATAKA WANANCHI WA IGUNGA WAACHANE NA VIONGOZI WENYE UROHO WA MADARAKA UBINAFSI WAKATI AKIZUNGIMZA NA TAIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JANA

 Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kama kawaida yake aliyojiwekea ya kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kila mwisho wa mwezi jana,alisema mwezi uliyopita uliuwa na matukio mengi ya  kusikitisha,kama ajali ya meli Zanzibar na  matukio mengine ya ajali za barabarani.
 Aidha ame mshukuru Rais wa Baraza la Mapinduzi Dkt Shein na Makamu wake wote wawili katika kushughulikia maafa hayo maiti 203 zilipatikana na kuzikwa ambapo maiti 197  walizikwa eneo la tukio,5 Kenye na Mmoja Tanga nao walizikwa walikopatikana,Rais kaendelea kutoa pole na rambirambi kwa ndugu na jamaa walifikwa na msiba huo na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengini Rais aliwasihi watumiji wa vyombo vya moto kuwa makini katika kuvitumia,pia kawataa wananchi wa Wilaya ya Igunga kujitoeza kwa wingi atika kumchagua kiongozi wanao mtaka,wasirubuniwe na viongozi wapenda madaraka na wabinafsi.

MVUA ZA VULI ZA RASHARASHA ZIMEANZA MJINI MOROGORO

 Mkoa wa Morogoro katika miaka ya 70 ulikuwa na mvua nyingi na ulikuwa ni miongoni mwa mikoa inayozalisha chakula wa wingi.lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu wa mazingira,hasa kukata mitikatika vyanzo ya maji,kuchoma mkaa,kuchoma moto misitu,kumesababisha mkoa huo upoteze ratiba zake za mvua kunyesha,hivyo hata namna ya uandaaji wa mashamba unawachanganya waulima wa mkoa huo.

Vyanzo vikuu ni milima ya Uruguru ( Uruguru Mountain ),na milima mingine ya mwambao ya mto Ruwaha,milima hiyo miaka ya nyuma ilikuwa ikibubujisha maji kipindi chote cha mwaka,Ila kwa sasa hali hiyo haipo  kutokana uharibifu wa mazingira atika uchezea uoto wa asili,na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mvua hizi zilianzia Kijiji cha Doma ,Melela ,Morogoro mjini,hadi Mikese.

Tuesday, September 27, 2011

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE LEO

 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu leo afanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa ofisi yake,Halmashauri na kuhitimisha na waandishi wa Habari wa Mkoa huo.
 Waandishi wa vyombo mbalimbali vinavyowakilishwa katika moa huo.
 Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club  mwenye shati leupe na Kaimu RAS Dkt Anselim Tarimo mwenye suti ya bluu aunda.
 Mwandishi wa habari Dada Cresencia Kapinga akitoa hoja.
 Waandishi akiwemo mwenye baraghashia ni wa TBC Songea Msigwa
Bwana Mwambungu akiwasikiliza waandishi,lengo lake ni kutaka kufahamina ili kuweza kubadilishana mawazo ya ujenzi wa maendeleo ya Mkoa huo.

Monday, September 26, 2011

Chuo Kikuu Songea cha anza,mkuu wachua atambulishwa

 Profesa Donatus Komba akisalimia waumini baada ya kutangazwa kuwa mkuu wa chuo kikuu cha Songea  na Asofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbert Mtega katika Kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulemba Kalemba Jumapili iliyopita kwenye ibada ya misia ya kwanza.
 Dokta Kiremire Araka akisalimia waumini baada ya kutangazwa kuwa ndiyo atashirikiana na Priofesa Kapinga katika kupoea wanachuo 250 watakao anza mwezi ujao tarehe 25 katika chuo hicho kipya Kusini mwa - Tanzania
 Askofu Mkuu Norbert Mtega akiwatangaza rasmi Mkuu wa chuo cha Songea cha Sayansi ya Jamii Profesa Donatus Komba na mwenzake Dkt.Kiremie Araka baada ya Ibada ya Misaa takatifu Jumapili iliyo pita.
 Kabla ya kuwatangaza Asofu aliwashika waumini mono wa heri na baraka katika kuchangia mfuo wa jimbo.
 Hapo amekaa wenye kiti chake akisubiri waumini kwende imshika mkono
i
 Profesa Komba wa kushoto mwenye kaunda suti miono mifupi na Dokta Araka  kulia wakitokea eneo walilotambulishwa.
 Hayo ni baadhi ya majengo ya chuo kikuu hicho cha Songea Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Kanda ya kusini.
Baadhi ya waumini waliyo shiriki Ibada hiyo iliyoandamana na michango mbalimbali kutoka katika Parokia za jimbo hilo ambapo parokia ya Bomba mbili na Parokia ya mjini zimetoa Tshs.1,500,000 kila parokia,kisha kuwatangaza Profesa Kapinga na Dokta Araka.


CHUO kikuu cha Songea Kitivo cha Elimu ( Sayansi ya Jamii ) kinatachukua wanachuo 250 kuanzia trehe 25 October mwaka huu kilicho anzishwa na Baraza la Maasofu Tanzania,na mkuu wa chuo hicho katangazwa rasmi na Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbert Mtega baada ya ibada yamisa jumapili iliyopita.

Mhashamu Mtega alimtangaza mkuu wa chuo hicho kuwa ni Profesa Donatus  Komba na Dokta Kiremire Araka ambao wataanza kuwapokea wanachuo hao mwezi ujao.

Aidha Asofu Mtega alisema Mkuu huyo wa chuo hicho na mwenzake wakishirikiana na uongozi wa kanisa wataanzisha ( Marafiki wa Chuo kikuu cha Songea ) ‘Songea University Friends’ chenye lengo la kukisaidia chuo hicho.

Kikundi hicho kimeanzishwa tokea Jumapili iliyo pita,alisema wale ambao walikuwa tayari waliambiwa waende wamwone Profesa Kapinga ili waweze ujiandikisha.’ Mwenye simenti,maplastic, fedha wanaombwa kujitolea  au kutoa msaada ili chuo hicho kitimize  malengo yake kusini mwa Tanzania katika Jubilei ya miaka 50 ya Uhuru.

Askofu Mkuu Norbert Mtega pia amewatangazia wananchi wa Manispaa ya Songea ambao wana nyuma kuzipangisha nyumba hizo kwa walimu na watumishi wa chuo hicho na wanafunzi watakao jiunga chuoni hapo kwa kuwa chuo hakina mabweni ya kutosha.

Saturday, September 24, 2011

WAJUE VIONGOZI WA MANDAO WA MAZINGIRA MKOA WA RUVUMA ( R NEA ) MWANGAZA FOUNDAION ( MF )

 Bwana Method John Ngerangera akiorodhesha mradi inayo endeshwa na Mtandao wa Mazingira Mkoa wa Ruvuma.Alisema kuwa jina la mradi ni Hifadhi na Ulinzi Shirikishi Jamii wa misitu na vyanzo vya Maji.Alisema Mtandao wake unatarajia kutoa mafunzo katika Tarafa ya Madaba katika Kata za Wino,Mahanje na Matumbi.
 Hiyo ni Nembo ya Mtandao wa Mazingira Mkoa wa Ruvuma
t
 Wajue viongozi wa Mtandao huo,wa kwanza juu  ni mwenye kiti Bwana Methodi Jo hn Ngerangera,wapili ni Bwana Wilbery Xavery Mahundi Katibu na watatu ni Bibi Magreth Gregory Ponera Mweka hazina
Bwana Ngerengera anaelezea jinsi Mtandao wao unavyo fanya kazi,alisema wanafanya kazi kihalali na wamepata Namba ya Usajili OONGO/0000/3881 Maeneo ya kufanya kazi ni Tanzania Bara wapo tayari kufanya kazi mkoa wowote iwapo watapata mialiko.Ametaja namba zake za simu kuwa ni pamoja na:-
  • Ofisi + 255 - 252602505
  • Res. + 255 - 25260241
  • Mob +255 - 713066677
  •         + 255- 784609639
  •        + 255 - 755 377784
Kwa mawsiliano nao,mwendelezo wa Mwangaza Foundation ( FM ) Utakuwa unaletwa kwenu kupitia Blog hii kwa maelezo zaidi Kutana na Mkurugenzi Bwana Method John Ngerengera.

Friday, September 23, 2011

UMEYA MANISPAA YA SONGEA NI VITIMBWI TUPU, MAKAMU MEYA ATIMKA NA KURA MADIWANI WA CHADEMA WAMKIMBIZA AIBU TUPU ,MEYA AVUA JOHO

Leo ndiyo leo hao waheshimiwa madiwani ni wa chama TAWALA na wa CHADEMA lakini Madiwani wa CCM ni wengi kuliko wa CHADEMA,cha ajabu madiwani hao katika kupiga kura za kuchagua Mstahiki Meya Mheshimiwa Charles Mhagama,ni kwamba  waliyo sema ndiyo ni 12 na waliyo sema hapana ni 14 hiyo ina maana hata baadhi ya Madiwani wa CCM walikuwa hawana imani na Mheshimiwa Mhagama kuwa Meya wa Manispaa ya Songea.

Kutokana na matukio yaliyotokea leo ya kumtangaza Meya mpya Mhe.Charles Mhagama katika manispaa hiyo kutangazwa na Makamu Meya badala ya Mkurugenzi wa Manispaa,ndipo madiwani wa CHADEMA na CCM kutoridhishwa na matokeo hayo.kesho nitakuletea na baadhi ya picha za vurumai hizo za kuwania Umeya.Hiyo ni dalili mbaya kiuongozi,maana Meya huyo atakuwa katika wakat mgumu kuongoza Manispaa hiyo kwa kutokuwa na imani  naye.


Thursday, September 22, 2011

SITTA ATAJA VIKWAZO ZINAVYO RUDISHA NYUMA MAENDELEO YA MKOA WA TABORA

 Mheshimiwa Samweli Sitta Waziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki ametaja vitu ambavyo vimesababisha mkoa wa Tabora kuchelewa kupata maendeleo kuwa ni pamoja na Umeme,maji miundo mbinu ya barabara na reli.amesema kuwa serikali sasa imeelekeza Tabora kuboresha miundombinu ya usafirishaji,basi baada ya miaka mitano kuanzia sasa.mkoa huo utapiga hatua kubwa katika maendeleo.
Naye aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Abed Mnyemusa anasema Tabora itakuwa moja ya mikoa ambayo itakuwa katika mandeleo baada ya miundo mbinu ya usafiri kukamilika.Alisema shirika la reli limechangia kwa kiasi kikubwa katika kurudisha nyuma maendeleo katika mkoa huo.kwa sababu ya shindwa kufanya kazi kama zamani.

VIONGOZI WA WANANCHI WA MANISPAA YA SONGEA LEO WAMEMPOKEA MKUU MPYA WA MKOA WA RUVUMA BWANA SAID MWAMBUNGU

 Mkuu wa mkoa mpya wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu alipokuwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Morogoro,baada Rais Kikwete kumteua kuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,kutoka kwenye wadhifa wa ukuu wa wilaya ya Morogoro.Leo ameripoti katika mkoa wa Ruvuma kwa wadhifa wa ukuu wa Mkoa ( Source MICHUZI )
a
 Waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya Songea ni miongoni mwa viongozi waliyempokea mkuu huyo wa mkoa kwa shangwe na furaha,kama ilivyo desturi ya wananchi wa mkoa huo wanavyo jua kupokea watu.
Mhe. Mwambungu anakaribishwa mkoani Ruvuma badala ya Mhe.Dkt Christine Ishengoma aliyehamishiwa mkoa wa Iringa.Mwambungu atapokea changamoto kadhaa katika mkoa huo zikiwemo za umeme,miundo mbinu ya barabara hasa katika manispaa ya Songea,Soko kuu,halina sakafu ,stendi ya mabasi siyo ya kuridhisha.kazi ni kwake .karibu sana Ruvuma ushirikiano na watu aliyowakuta ndiyo kutaleta maendeleo ya mkoa huo.

Wednesday, September 21, 2011

WABUNGE WA VITI MAALUMU RUDINI KWA WALIYO WACHAGUA,MSIKILIZE SHIDA ZAO

Blog hii imekutana na akina mama kadhaa wakiwalalamikia wabunge wa viti maalumu nchini kwa vitendo vyao vya kusahau kwenda kutoa shukurani kwa akina mama ambao wana matatizo kibao yanayo hitaji wawakilishi wao kuwa saidia,

Waheshimiwa wabunge wa viti maalumu tangu wachuguliwe na akinamama wa chama Tawala na wengine wamebahatika kupata vyeo vya juu kama uwaziri,ukuu wa mikoa.hawaja rudi kuwashukuru akina mama wenzao,akina mama hao waliwaamini kuwa watakuwa tayari kuwa wawakilishi na msaada mkubwa katika masuala ya maendeleo.
Wanasema wakitaka uongozi wanakaa  na akimama wenzao lakini wakishachaguliwa tu wanaondoka na kukaa Dar es salaam mpaka uchaguzi ujao,je huo ndiyo uwakilishi wa kweli,je watajuaje matatizo ya akinamama wenzao au watapataje mikopo kwa ajili ya biashara ndogo ndogo ? ni maswali mengi Blog hii imekutana nayo kutoka mitaani. katika Manispaa ya Songea.

MWIZI HAPENDI KUIBIWA HEBU ONA MCHEO HUO INGWA NI MCHEZO LAKINI KUNA UKWELI NDANI YAKE

Madereva wa pikipiki au boda boda kupandisha abiria wawili au mishkaki ni jambo la kawaida,ingawa askari wa usalama barabarani wanajaribu kuzuia.Lakini kwa tukioa la wanasanaa hao,linawakilisha mwizi kuogopa kuibiwa.Huyo bwana naliyekaa akiangalia alikotoka aliogopa kukaa kumwangalia dereva,na mwenzake akae nyuma yake,huenda aliyekaa nyuma yake angemwibia pesa yake aliyeweka mifuko ya nyuma.

Waziri Mkuu awashtukia polisi katika usindikizaji wa magari ya mizigo yanayokwenda nje ya nchi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amewashtukia askari polisi wanao sindikiza magari ya mizigo kutokuwa makini na kazi yao ,hasa katika kupitisha sukari kwenda nje ya nchi,Ametoa angalizo kuwa iwapo askari polisi hawatakuwa makini ,askari jeshi watafanya kazi hiyo badala yao.

BREAKING NEWS ! ! ! SERIKALI IMERUHUSU WATU BINAFSI KUWEKEZA KWENYE UMEME

Waziri wa Nishati na Madini Mhe.William Ngereja amesema kuwa serikali imeruhusu watu binafsi kuwekeza kwenye umeme,wakiwekeza kwenye umeme wataweza kuiuzia TENESCO umeme wao,ili kupunguza tatizo la umeme lililoikumba taifa.

Saturday, September 17, 2011

MFANYAKAZI WA KITUO CHA MAGAZETI URU YETU MBEYA MAREHEMU JOSEPH MHAGAMA AMEZIKWA LEO SONGEA

 Joseph Mhagama amezikwa kwenye makaburi ya Lizaboni  katika manispaa ya Songea jana ambapo alifariki duia katika hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya.
 Marehemu Joseph Mhagama alizaliwa tarehe 19/01.1957 na akafariki tarehe 14/9/2011 na kuzikwa tarehe 17/9/2011,marehemu ameacha mjane na watoto watano ( 5 )
 Baada ya kuwekwa mataji kwenye kaburi lake watoto wa marehemu waliwasha mishumaa
 Mama wa marehemu Joseph aliyeinama kidogo na mke wake aliyejikumbatia wakilia kwa uchungu wakumpoteza mtu aliyekuwa tegemeo lao katika maisha.
Baada ya historia ya marehemu salamu za mwakilishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zilitolewa na Mkuu wa kituo cha Nuru Yetu Mbeya Bibi Tupeligwe mwenye miwani,aliye sema badala ya mwakilishi kutoka wizarani Bwana Fridolini Banzi kuchelewa kutokana na gari lake kuharibika njiani,lakini alifika baada ya mazishi.Mungu ailaze Roho ya Marehemu huyo mahali pema peponi Amina.

Friday, September 16, 2011

MKURUGENZI WA ELIMU YA WATU WAZIMA ANAUNGANA NA FAMILIA YA MAREHEMU JOSEPH MHAGAMA ALIYE FARIKI GHAFLA JIJINI MBEYA MWILI WAKE UMELETWA SONGEA KWA MAZISHI

Marehemu Joseph Mhagama aliajiriwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima kwenye vituo vya Kanda.Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Jijini Mbeya.Marehemu amefariki ghafla,na mwili wake umeletwa Songea kwa mazishi ambako ndiyo kwake.Wafanya kazi wa TUJIFUNZE KUSINI kinatoa pole nyingi kwa familia ya Mhagama kwa kufiwa na mfanya kazi mwenzao hasa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.Mungu ailaze roho ya marehemu Joseph Mhagama mahali pema peponi Amina.

KUMBE UZURI WA GARI NI INJINI!

Kuchimba dawa,lugha isiyo na makali kwa waungwana.basi hilo lilikuwa likielekea Mbeya,la Kampuni ya Super Feo,linaloondoka saa 5,abiria walivyo fika stendi ya Songe hawa kuamini macho yao kuona basi hilo likifika pale na wasafiri waingie.Tiketi zao zinaonyesha basi jipya lakini lililoletwa lazamani na limechoka ile mbaya.

Wasafiri waliingia kwa shingo upande nikiwemo mimi pia,kuwa safari haitafikika,kumbe basi lile ni imara injini yake bado inadai,tulifika mbeya mapema na kurudi nalo hadi Songea.Ama kweli uzuri wa gari ni Ijini na siyo rangi au bodi.

SEMINA YA SIKU MBILI YA WAANDISHI WA HABARI INAENDELE JIJINI MBEYA

Semina hiyo inahusu maadili ya waandishi wa habari inayoendeshwa kwa vyama vya waandishi wa habari katika mikoa nchini.( Press clubs}.tunawatakia mafunzo mema ,pia wayashike mafundisho wanayo elekezwa na walimu wao.kila kazi ina maadili,miiko yake ili ifanyike katika utaratibu uliyowekwa.

Hivyo waandishi ndiyo kisemeo katika jamii,waandishi ndiyo wanaowasemea wasio na sauti katika jamii,kwa maantiki hiyo hawatakiwi kuipotosha jamii kwa kutumia kalamu zao,au kuichonganisha jamii kwa uwezo waliyokuwa nao.Pia wanahaki ya kupata habari na kuiandika.
Pamoja na hayo na wadau wa habari nao wana nafasi yao ya kutoa habari hata kama inaumiza kwake lakini itanufaisha taifa.Hivyo mtoa na mpokea habari wote wana nafasi kubwa kwa jamii.

SOKO LA SIDO MWANJLWA MKOANI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO MALI NYINGI ZA WATU ZIMEANGAMIA

 Moto mwingine wa teketeza sokola SIDO lililoko Mwanjelwa Jijini Mbeya uliyo anza takribani saa 3.00 asubuhi ,pamoja na jitihada ya magari ya zimamoto Jijini humi lakini haikuzaa matunda.moto uliwaka utadhani wamemwagia petrol.
 Kama unavyoona hali ilivyo kuwa ,ilikuwa siku ya maswali mengi kwa wana mbeya kwanini masoko ya Jijini humo yanateketea kwa moto? lilianza la Mwanjelwa,likaja la Mbeya mjini,kisha la Tunduma na sasa la SIDO ambalo lilikuwa uti wa mgongo wa mapato ya Jiji hili vitega uchumi vya watu.
a
 Lakini watu nao hasa vibaka walipata vya kupata badala ya kuokoa kwa ajili ya wenye mali bali ni kwa manufaa yao wamepata mitaji bila jasho.
 Ndipo FFU walipo tumia mabomu ya machozi kutawanya wimbi la vibaka hao,hali ilikuwa tete sana hasa kwa wenye maduka ambayo yaliteketea hakuna kilicho okolewa.ikumbukwe wawekezaji hao walikopa kwa lengo la kulipa baada ya kuuza bidhaa hizo lakini bidhaa hizo zote zimekuwa majivu je watalipa lipa vipi?
 Blog hii imekuletea uone tu hali ilivyo kuwa moto ulivyo kasirika katika kuangamiza mali za watu wasio na hatia jijini humo,hata kama haukuwa karibu kushuhudia nini kilicho tokea kwa akina mwanafyale hao umejionea hali ya kutisha ilivyo kuwa,moto ni mzuri kwa kupikia na ukitumiwa vizuri lakini ukitumika bila utaratibu ,moto ni adui mkubwa wa maisha ya watu.
Poleni sana wana - Mbeya Pole Pia Mheshimiwa Kandoro mkuu wa Mkoa anaye kwenda mkoani humo anakaribishwa kwa matukio ya moto,lakini usijali cha msingi utafiti kwa nini masoko jijini humo yanaungua kila mwaka?.

Tuesday, September 13, 2011

WANA - BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI IPO KATIKA KUUNGANA NA NDUGU,JAMAA WALIYO POTEZA NDUGU NA JAMAA ZAO KATIKA AJALI YA MELI HUKO PEMBA

Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ina toa pole kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kwa kupoteza nguvu kazi yake kutokana na ajali ya meli ambayo imewapa watanzania wakati mgumu wa majonzi. Kama waswahili wasemavyo ) kuwa mtu akiumwa na nyoka ,akiona kamaba anashtuka.Ajali hiyo imewakumbusha Wa - Tanzania ajali ya MV Bukoba ambayo haitasahaulika na watanzania walio wengi.Pole kwa familia zilizokumbwa na matatizo hayo

Lakini kama ni kosa kama lile la MV Bukoba,Serikali ifuatilie maana uzembe wa wachache unasababisha maangamizi ya maisha ya watu,kama meli ina uwezo wa kuchukua abiria 600 sasa iweje ichukue abiria 800 na mizigo,kwa vyovyote ilizidiwa na mzigo na ule mzigo meli haijachue yenyewe ikasema basi bali ni watu wenye akili ya kujua sasa meli imejaa iondoke ,lakini walivaa nafsi zisizojali uhai wa wengine.

AMA KWELI KILA KITU NA WAKATI WAKE, ZAO LA MKONGE LILIKUWA NI ZAO LA BIASHARA NA MASHAMBA MENGI YALIKUWA YAKISHIKILIWA MAGRIKI YALIVYO CHUKULIWA NA SERIKALI ZAO HILI LILIPUNGUA THAMANI NA MASHAMBA YALIKUFA.

 Mkonge ni zao linalotoa nyunzi ambazo zinatengenezea mazulia,kamba mbalimbali,magunia,na vitu vingi.kwa matumizi ya nyumbani.Aidha zao hili lililimwa  katika mikoa ya Morogoro,Tanga,Kilimanjaro na kusini kidogo mkoa wa Lindi.Lakini baada ya serikali kuyachukua mashamba hayo kutoka kwa ( Wazungu } Magriki mashamba mengi yalikufa.
Mashamba ambayo wawekezaji wanaendeleza zao hilo kwa kiasi kidogo ni kama hayo ya Morogoro - Kigruila,Kimamba Kilosa,Korogwe,na mengine.Serikali kama haijapata wawekezaji wa kuendeleza zao hilo basi wananchi wanao yazunguka mashamba hayo wapewe walime mazao ya mahindi,kunde,maharage na mazoa mengine mchanganyikoa kuliko kuyaacha na kuwa msitu na mapori ya kuhifadhi wanyama waharibifu wa mazao ya wakulima.

Friday, September 9, 2011

NIKIWA SAFARINI NIKITOKEA BONGO NILIJIFUNZA MENGI KUHUSU MADERVA NA UENDESHAJI WA MAGARI YAO

 Morogoro kwenye mzunguko kwnea Stendi ya mabasi makubwa
 ukisha ingia uwanjani hapo utawakuta watu wamekaa katika kibanda ndani ya uwanja huo katika stendi ya Morogoro.

Hiyo ndiyo stendi ya Morogoro kwa ndani inavyo onekana,picha hizi nilizipata nikiwa ndani ya basi la Sumry,lakini ni kazi kidogo,kuna watu wengine wana mawazo hasi,wakikuona una kamera wanakuwa wakali wakidai kuwa wakipigwa picha hizo wanakwenda kuuzwa ulaya,Basi mkasa huo ulinipata kwa kijana mmoja aliyekuwa akiuza mikate.