WASWAHILI lazima watakuwa na Historia yao
ingawa si rahisi kuelezea bila kujua lugha yao ilianza lini na wapi karne gani.Wataalamu
wa lugha ya Kiswahili wamechambua kuwa kwenye karne ya 18 au kabla yake
maandishi ya Kiswahili ya aina Fulani yalianza kuonekana
Wachambuzi waliowengi wamadai Kiswahili
kina asili ya Kibantu ambao labda walitokea Afrika Magharibi na jinsi walivyo
zagaa Mashariki na Kusini mwa Afrika na namna walivyo jigawa katika makundi yao mbalimbali lakini cha
ajabu historia haichambui vikundi vilivyo unda jamii hiyo bali marejeo mengi
yanazungumzia jamii ya Wabantu kwa ujumla.
Marejeo yanazungumzia historia ya
lugha na jamii ya waswahili kupitia enzi za nyuma katika kitabu cha Derek Nurse na Thomas Spear.walau
kitabu hichi ndicho kinatoa mwanga kidogo kuhusu jamii ya Wabantu walioelekea
mashariki na mahusiano yao
na jamii zisizo za Kibantu.
Kila lugha ina historia yake na
chimbuko lake,Watu wengi wanadhani Kiswahili ni lugha nyepesi,lakini ni nyepesi
kwa kuongea bali si rahisi kwa wanafunzi,ugumu unaojitokeza ni upungufu wa
vitabu vya rejea na ziada,na tatizo hilo ni kwa wanafunzi wa ngazi zote.
Kwa hiyo ukitaka kujua historia
ya lugha na jamii ya waswahili ni lazima uwe na ushahidi wa kiakolojia na
kihistoria kuanzia karne za nyuma hadi miaka 800 na ya 1500 B.K.Aidha marejeo
yanabaini historia ya Kiswahili ilianza tangu karne ya 19 hadi 20.
Kiswahili hicho kikaanza kukuzwa
katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na kwa kiasi Fulani Afrika ya Kati.Kama mwanzo wa Blogu hii
nilileta Magofu ya miskiti na majengo ya Masultani ya Kilwa Kisiwani ambayo
yalijengwa na Masultani wa Kiarabu waliofika kwa shuhguli za biashara na
kueneza dini ya Kiislamu.
Tangu Milenia ya kwanza Pwani ya
bahari ya Hindi ilijikita katika mazingira mapana ya biashara ambapo ngarawa
zilisafiri kutoka Bara Arabu na Ghuba ya Uajemi zilizopeperushwa kila mwaka na
pepo za kaskazi na kuleta vyombo vilivyo finyangwa,nguo na vyombo vya chuma.
Warabu hao walibadilishana na
watumwa,pembe za ndovu,dhahabu,mbao,simbi,rangi na manukato,kisha walirejea
kwao na zikipeperushwa na pepo za kusi.Ingawa bidha hizo zilikwisha fikishwa na
Wareno na Wagiriki kabla ya karne ya tatu.
Ukisoma marejeo mengi,vitabu vya
rejea na ziada utapata uhakika wa chimbuko la lugha ya Kiswahili katika Upwa wa
Bahari ya Hindi Afrika Mashariki ambapo
wafanya biashara wa kiafrika na waarabu na wajemi walitokea kwenye bandari
katika Ghuba ya Uajemi.Baadaye biashara ilihamia kusini – magharibi mwa Uarabu
Yemen na Hadhramaut hatimaye Oman.
Baadaye tutaendelea na biashara……….
No comments:
Post a Comment