Saturday, May 7, 2011

ISHENGOMA AOMBA MGAO MKUBWA WA WALIMU KUTOKA MATOGORO

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma
 

'KAMA kunauwezekano walimu wanaomaliza mafunzo ya ualimu chuo cha ualimu Matogoro wapangwe mkoa wa Ruvuma kwa kuwa hapa ni kwao istoshe wanayafahamu mazingira ya mkoa huu,ukilinganisha na wale wakutoka mikoa mingine' alisema Dkt Ishengoma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma alisema hayo kwa Naibu waziri wa elimu wakati akimshukuru kwa ujio wake mkoani humo.Alisema kama kuna uwezekano wa kupata mgao mkubwa wa walimu kutoka chuo cha Matogoro Songea ilii ni  kupunguza idadi ya walimu wanaoacha baada ya kuona mazingira magumu ya kazi.

Aidha alisema wanachuo wa chuo hicho karibu wengi ni wenyeji wa mkoa huu hivyo wakaipangwa mkoa huu hawatakuwa na mashaka ya kufanya kazi katika mazingira ambayo wanayafahamu kwakuwa ni kwao.

No comments:

Post a Comment