Wednesday, May 4, 2011

HONGERA CATHERINE MWIKWA SEND - OFF YAKO ILIFANA SANA

 HAPO NI JINSI GANI WATAALAMU WA KUPAMBA JUKWAA LA MAHARUSI AMA SEND - OFF.Hilo ni Jukwaa Bwana alilopambiwa Bibi Catherine Mwikwa siku ya Send  Off yake Songea Club Ruvuma
 Aliyetulia ni Bibi Catherine Mwikwa ,amepozi mwenyewe hapo.
 Hapa ni mume wake Bibi Catherine Mwikwa anashuhudia jinsi wapambe wanavyo mwaga mazawadi  ng'ombe,mashamba,makabati,vyombo basi mradi sofa kwenda mbele wacha kuna watu wanafupa mchezo hakuna bwana hapa Songea.
 Hao ni mabesti wao mume na mke wamepozi wakishuhidia watu walivyo furika ukumbini ( Mradi sherehe kulwa)
 kwenye mambo kama haya utaona mambo mengi Huyo sio anatakakuruka hapana ila yeye ni Baba mkwe wa Catherine pia ni Mchungaji hapo alikuwa anamwaga maombi kabla watu hawaja karibia meza ya vyakula.
 Hapo hapakuwa Demonstration ya vinywaji bali ni vinywaji vilivyo wekwa high table ila waliowekewa si wakata maji ingekuwa ni wale wakata maji basi siku hiyo ingekuwa viroja.
 Bibi Catherine akiwa na shangazi yake kutoka kwao Morogoro kwa Marehemu  Baba yake Dr.Mwikwa
Send off hiyo ilikwa na watu mashughuli katika mji wa Songea wakwanza kulia mwenye miwani ni Dr.Manyai wa Hospitali ya Peramiho na pili ni Mkurugenzi wa Chembele Applied Zone walitoka kumpa mkono wa heri na baraka Bibi Catherine.

No comments:

Post a Comment