Friday, May 13, 2011

90 wapewa vyeti na RPC Michael Kamuhanda baadaya kupata mafunzo ya kuendesha pikipiki Mbinga

Ili kupunguza ajali zitokanazo na waendesha pikipiki wasiopata mafunzo,ni muhimu elimu itolewe kwa waendesha pikipki na abiria Kamanda wa Polisi mkoa wa ( RPC ) Michael Kamuhanda aliwaambia wajumbe wa kikao cha ushauri cha mkoa RCC,kuwa waendesha pikipiki wa Wilaya ya Mbinga wapatao 90 wamepata mafunzo na kuwagawia vyeti vya kuhitimu.Amesema wilaya nyingine zifanye kama wenzao.

Naye kaimu  Katibu Tawala mama Nguluse aliongezea kuwa elimu kwa waendesha pikipiki ni muhimu na abiria hasa akina mama wakae mkao wa kiume katika pikipiki ili ajali ikitokea asianguke kiurahisi kama ilivyo wanavyo kaa upande kwenye pikipiki.

Aidha alisema ni muhimu dereva na abiria wake wawe wamevaa Crash Helmet ili kuepusha ajali itokanayo na kuendesha pikipikibila kinga kichwani


No comments:

Post a Comment