Tuesday, May 29, 2012

MADWA YA KULEVYWA NAYO NI HATARIII,BW,JUMA NYUMAYO ANAWAHOJI VIJANA WANAOTUMIA MADAWA HAYO KILWA KIVINJE

Hao vijana walioketi wanatumia madawa ya kulevywa wa Kilwa Kivinje lugha wanayozungumza ni ya ina yake .Mhariri  Msaidizi wa magazeti ya Kisomo vjijini Kanda ya Kusini Bw. Juma Nyumayo  mwenye suluali nyeusi anawahoji vijana hao,kwa nini wanatumia madawa hayo.wanadai kuwa hawana kazi ya kufanya,hivyo wakiyatumia madawa hayo wanakuwa bomba.
   Hivyo kwa hali hiyo tutawafikisha wapi vijana wetu ? ukweli ukiwaona vijana hao utawahurumia,wamekuwa kama mazezeta,tahira hivi.maana wanamawazo ya mbali sana,kwamba meli wana uwezo nazo katika kuzamia.

KILWA KISIWANI NA SONGOMNARA IMEWEKWA KWENYE URITHI WA DUNIA,BW.JUMA NYUMAYO MWANDISHI WA HABARI NA MHARIRI WA MAGAZETI YA KANDA TUJIFUNZE KUSINI ANASOMA KIVUKONI KWENDA KISIWANI

Bw.Juma Nyumayo aliyeshika kibao kilicho andikwa UNESCO- HIFADHI YA URITHI WA DUNIA,Kilwa Kisiwani na Songo Mnara,kibao kilichowekwa kabla ya kupanda maboti kwenda Kilwa Kisiwani ambako kuna majengo ya kihistoria na ustaarabu wa Kiarabu na Masultani na Ngome ya Wareno.
 Huyo ni mfanya kazi katika kivuko hicho ambaye kazi yake ni kutambulisha wageni/watalii wanaokwenda Kisiwani huko kuona mabaki ya majengo misikiti iliyojengwa enzi za biashara za waarabu zikiwemo za watumwa,pembe za ndovu.
UNESCO ndiyo wanaosaidia kufanya majengo yaliyoachwa yawe katika hali ya kuvutia na kupendeza .Tuna vivutio vingi pwani ya kusini mwa Tanzania.

Monday, May 28, 2012

Haya bado hayaja malizika kusombwa kwenye ghala la chakula la Taifa Ruhuwiko Songea ,na mengine yanavunwa sasa.kazi kwa walaji.

Shehena ya magunia ya mahindi ya zamani ambayo bado yanasombwa ,lakini pia wakulima wameanza kuvuna mahindi mapya katika Mkoa huo wa Ruvuma.Ni kazi kweli kwa walaji.

Hivi ndivyo ilivyo kuwa, Askofu wa Anglican Songea alivyo wahusia wakuu wapya wa wilaya baada ya kuapishwa

Bishop/Askofu wa Anglican aliwaambia ukweli wakuu hao wa Wilaya kuwa Mungu amewateua kwenda kuhudumia jamii,kwenda kutangaza amani na utulivu katika jamii wanayoikuta,kwenda kuongeza chachu ya maendeleo ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Ruvuma na mabungwa wa kuzalisha chakula kwa kilimo.
  Wananchi na Taifa linawategemea wao katika kuhamasisha wananchi kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.Hivi sasa wakuu hao wameunganika na wakuu wa mikoa,makatibu tawala wa mikoa kupata semina elekezi Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete

MWENGE WA UHURU MKOANI RUVUMA UTAFANYA KAZI YA KUKAGUA MIRADI 51 YENYE GHARAMA YA TSHS,1,930,357,902.



Gharama hiyo yenye mchanganuo wa uchangiaji wa gharama za miradi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka  2012 ni kama ifuatavyo:-
  • Nguvu za wananchi Tshs.296,022,645/=
  • Halmashauri za wilaya na Manispaa Tshs.204,486,125/=
  • Serikali Kuu Tshs.773,599,581
  • Wadau wa Maendeleo Tshs.458,809,551/=
  • Watu Binafsi Tshs.287,440,000/=
Mwenge uko Mkoani Ruvuma Umepokelewa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma kutoka Mkoa wa Njombe katika Wilaya ya Nyasa na  kuanza kukimbizwa katika wilaya zote tano zenye Halmashauri sita ambazo ni Wilaya ya Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru.
    Ukiwa Mkoani Ruvuma Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kufungua miradi 13 yenye thamani ya Tshs.390,684,832 kuweka mawe ya msingi miradi 22 yenye thamani ya Tshs.1,303,187,695, kuzindua miradi 12 yenye thamani ya Tshs.141,045,375 na miradi 04 yenye thamani ya Tshs.34,840,000 itakaguliwa na kufanya jumla ya miradi yote kuwa 51 yenye thamani ya Tshs.1,930,357,902.
Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema “Sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau”.
Mwenge umekuwa ni kichocheo kikubwa cha shughuli za maendeleo, umoja, mshikamano na amani kwa Taifa letu.Lakini usemi wa Baba wa Taifa unaanza kuingia dosari Amani hiyo inaanza kutoweka,unasikia wenzetu Zanzibar Makanisa yanachomwa,tatizo hawataki Muungano sasa kukataa Mungano kuna uhusiano gani na Kuchoma makanisa ? Tunaelekea wapi sasa.



Sunday, May 27, 2012

Maisha in kuhangaika kila kukicha watu wnahangaika kutafuta ridhiki

 Kama hivyo foleni ya Malori yakisubiri kupakia mahindi ankuyapeleka Uganda,madereva wanakaa muda mrefu  hawaonani na familia zao yote hayo nikuhangaika kutafuata ridhiki.
Yote tisa huyo kijana anapgonga mawe katika Jiji la Mwanza ambako wameanzisha ujenzi wa barabara za mawe kutokana na uwingi wa mawe uliyopo katika Jiji hilo 'Rock City' anagonga mawe hayo kulingana na kipimo anachopewa anapata fedha za kwenda kumsaidia katika maisha yake.Maisha ni safari ndefu kila mmoja Mungu amempangia maisha yake,

RAIS KIWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAZAMANI 63 NA WAPYA 70 AMBAPO WAKONGWE MAJINA YAO HAYAPO



Tuna watakia uwajibikaji mwena wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu wakishirikiana na wadau wa sekta mbalimbali watakao wakuta katika wilaya walizopangiwa ,ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi.Mkoani Ruvuma Songea Joseph Joseph Mkirikiti,Tunduru Chande BaruUcho,Namtumbo Abdulah S.Lutavi,Mbinga Senvi S.Ngaga na Nyasa ( Mpya ) Ernest N Kahindi.Karibuni sana Ruvuma.

Majina na wilaya wanayokwenda wakuu wa wilaya za zamani 63 hayo:-

WAKUU WA WILAYA WA ZAMANI NA WILAYA WANAZOKWENDA  NI HAO

NA.    JINA           WILAYA ANAYO KWENDA
1.         James K. O. Millya             Longido
2.         Mathew S. Sedoyeka          Sumbawanga
3.         Fatuma L. Kimario             Igunga
4.         Capt. (Mst.) James C. Yamungu Serengeti
5.         Lt. (Mst.) Abdallah A. Kihato       Maswa
6.         Sarah Dumba          Njombe
7.         Jowika W. Kasunga            Monduli
8.         Elizabeth C. Mkwasa         Bahi
9.         Col. Issa E. Njiku    Misenyi
10.       John B. Henjewele Tarime
11.       Elias W. Lali            Ngorongoro
12.       Raymond H. Mushi            Ilala
13.       Francis Miti             Ulanga
14.       Evarista N. Kalalu             Mufindi
15.       Mariam S. Lugaila             Misungwi
16.       Anna J. Magowa     Urambo
17.       Anatory K. Choya   Mbulu
18.       Fatma Salum Ally Chamwino
19.       Deodatus L. Kinawiro        Chunya
20.       Ibrahim W. Marwa             Nyang’hwale (mpya)
21.       Dkt. Norman A. Sigalla     Mbeya
22.       Moshi M. Chang’a   Mkalama (mpya)
23.       Jordan M. Rugimbana       Kinondoni
24.       Georgina E. Bundala         Itilima (mpya)
25.       Halima M. Kihemba           Kibaha
26.       Manzie O. Mangochie        Geita
27.       Abdula S. Lutavi     Namtumbo
28.       Zipporah L. Pangani          Bukoba
29.       Dkt. Ibrahim H. Msengi    Moshi
30.       Col. Cosmas Kayombo       Kakonko (mpya)
31.       Lembris M. Kipuyo             Muleba
32.       Elinasi A. Pallangyo          Rombo
33.       Queen M. Mlozi       Singida
34.       Juma S. Madaha     Ludewa
35.       Angelina Mabula    Butiama (mpya)
36.       Hadija H. Nyembo Uvinza (mpya)
37.       Ernest N. Kahindi Nyasa (mpya)
38.       Peter T. Kiroya        Simanjiro
39.       John V. K. Mongella           Arusha
40.       Baraka M. Konisaga          Nyamagana
41.       Husna Mwilima       Mbogwe (mpya)
42.       Sophia E. Mjema     Temeke
43.       Francis Isaac           Chemba (mpya)
44.       Abihudi M. Saideya            Momba (mpya)
45.       Khalid J. Mandia    Babati
46.       Anna Rose Nyamubi          Shinyanga
47.       Dani B. Makanga    Kasulu
48.       Amina J. Masenza Ilemela
49.       Mercy E. Silla          Mkuranga
50.       Christopher R. Kangoye    Mpwapwa
51.       Lt. Edward O. Lenga          Kalambo (mpya)
52.       Halima O. Dendego            Tanga
53.       Lephy B. Gembe      Dodoma
54.       Saidi A. Amanzi      Morogoro
55.       Jackson W. Msome             Musoma
56.       Elias C. B. Goroi      Rorya
57.       Lt. Col. Benedict Kitenga Kyerwa (mpya)
58.       Erasto Sima             Bariadi
59.       Nurdin H. Babu      Mafia
60.       Khanifa M. Karamagi        Gairo (mpya)
61.       Gishuli M. Charles             Buhigwe (mpya)
62.       Saveli M. Maketta Kaliua (mpya)
63.       Darry Rwegasira     Karagwe

MAJINA 70 NA WILAYA WANAZOKWENDA WAKUU WA WILAYA HAO WAPYA NI HAO:-

1.         Novatus Makunga Hai
2.         Mboni M. Mgaza     Mkinga
3.         Hanifa M. Selungu             Sikonge
4.         Christine S. Mndeme         Hanang
5.         Shaibu I. Ndemanga          Mwanga
6.         Chrispin T. Meela   Rungwe
7.         Dr. Nasoro Ali Hamidi       Lindi
8.         Farida S. Mgomi     Masasi
9.         Jeremba D. Munasa           Arumeru
10.       Majid Hemed Mwanga      Lushoto
11        Mrisho Gambo         Korogwe
12.       Elias C. J. Tarimo   Kilosa
13.       Alfred E. Msovella Kiteto
14.       Dkt. Leticia M. Warioba    Iringa
15.       Dkt. Michael Yunia Kadeghe       Mbozi
16.       Mrs. Karen Yunus Sengerema
17.       Hassan E. Masala   Kilombero
18.       Bituni A. Msangi    Nzega
19.       Ephraem Mfingi Mmbaga            Liwale
20.       Antony J. Mtaka     Mvomero
21.       Herman Clement Kapufi   Same
22.       Magareth Esther Malenga           Kyela
23.       Chande Bakari Nalicho     Tunduru
24.       Fatuma H. Toufiq   Manyoni
25.       Seleman Liwowa     Kilindi
26.       Josephine R. Matiro           Makete
27.       Gerald J. Guninita Kilolo
28.       Senyi S. Ngaga        Mbinga
29.       Mary Tesha Ukerewe
30.       Rodrick Mpogolo     Chato
31.       Christopher Magala           Newala
32.       Paza T. Mwamlima            Mpanda
33.       Richard Mbeho        Biharamulo
34.       Jacqueline Liana    Magu
35.       Joshua Mirumbe     Bunda
36.       Constantine J. Kanyasu    Ngara
37.       Yahya E. Nawanda            Iramba
38.       Ulega H. Abadallah            Kilwa
39.       Paul Mzindakaya   Busega (mpya)
40.       Festo Kiswaga         Nanyumbu
41.       Wilman Kapenjama Ndile            Mtwara
42.       Joseph Joseph Mkirikiti    Songea
43.       Ponsiano Nyami      Tandahimba
44.       Elibariki Immanuel Kingu           Kisarawe
45.       Suleiman O. Kumchaya    Tabora
46.       Dkt. Charles O. F. Mlingwa          Siha
47.       Manju Msambya     Ikungi (mpya)
48.       Omar S. Kwaangw’             Kondoa
49.       Venance M. Mwamoto       Kibondo
50.       Benson Mpesya       Kahama
51.       Daudi Felix Ntibenda        Karatu
52.       Ramadhani A. Maneno     Kigoma
53.       Sauda S. Mtondoo   Rufiji
54.       Gulamhusein Kifu Mbarali
55.       Esterina Kilasi        Wanging’ombe (mpya)
56.       Subira Mgalu           Muheza
57.       Martha Umbula      Kongwa
58.       Rosemary Kirigini Meatu
59.       Agness Hokororo     Ruangwa
60.       Regina Chonjo         Nachingwea
61.       Ahmed R. Kipozi     Bagamoyo
62.       Wilson Elisha Nkhambaku          Kishapu
63.       Amani K. Mwenegoha       Bukombe
64.       Hafsa M. Mtasiwa   Pangani
65.       Rosemary Staki Senyamule         Ileje
66.       Selemani Mzee Selemani Kwimba
67.       Lt. Col. Ngemela E. Lubinga       Mlele (mpya)
68.       Iddi Kimanta           Nkasi
69.       Muhingo Rweyemamu      Handeni
70.       Lucy Mayenga         Uyui