Sehemu ya jengo ambalo lilikuwa na ukumbi mkubwa wa kunadi bidhaa zikiwemo watumwa,pembe za ndovu,simbi,mbao na vyombo vya kufinyangwa kutoka bara la Arabu na Ghuba ya uajemi,kisha kuingiza kwenye ngarawa tayari kwa kusafirisha.
Hicho ni kiberenge kilitumiwa na mmoja wa mwanaakolojia ambaye akikuwa akichimba ili aone masalia ya vyombo vilivyo kuwa zikitumika wakati huo na washirazi kisiwani hao wakati huo.aliyeshika kiberenge ni Bw.samweli mtembeza wattalii.
Hapo si kiwanja ila ni ukumbi amabo mnada ulikuwa ukifanyika,au sherehe zao watawala hao wa kiarabu walikuwa wakifanyia humo,kwa mbele kuna maji ni bahari ambapo kuna ngazi za kuteremshia bidhaa kuingiza kwenye ngarawa zao.fika ukajionee ni utalii nafuu zana wa kuona kisiwa cha kihistoria Tanzania.
Pwani ya kusini mwa Tanzania Mafia na kilwa ilikuwa ni miji
ya biashara katika karne ya kumi na moja,pia biashara ilishamiri Mogadisho
nchini Somalia.Ngarawa zilipeleka pembe za ndovu,dhahabu kutoka
Msumbiji,watumwa na bidhaa kadhaa kutoka pande nyingine za pwani kwa ajili ya
kuwauzia warabu wakati wa msimu wa biashara.
Aidha Kilwa kutokana na wanaisimu wanasema historia ya Kiswahili
imeanzia miji ya pwani ya Afrika Mashariki,na Kilwa ni mmoja wapo.warabu
waliingia kiujanja ujanja kufundisha dini ya kiislamu ambapo shehe wa kwanza alikuwa
mshirazi Muhammad mtoto wa Ali bin Hasan.
Alikuwa mwanzilishi wa utawala wa Kilwa na kukutwa na
Wareno,na ndiye aliyekuwa wa kwanza katika mlolongo wa Waarabu kutoka Bara la
Arabu na Ghuba ya Uajemi.Ili kujua tamaduni na asili ya waswahili katika pwani
hizo wanaakolojia wanachambua kwa makini ambapo wanaantropojia nao walifanya
tafiti zao za kuchunguza mabaki katika miji na vijiji katika Pwani hiyo.
Mapema katika milenia ya kwanza kabla ya Kristo ngarawa
zilikuwa zikisafiri kutoka Bara la Arabu na Ghuba ya Uajemi zikipeperushwa na
pepo za kaskazi,kuleta vyombo vilivyofinyangwa,nguo na vyombo vya chuma vilivyo
badilishwa na pembe za ndovu,watumwa,mbao,simbi na rangi na kurudi kwao na pepo
za kusi.
Kwa wale wanaochukua shahada ya kwanza ya Kiswahili ningewashauri
wafanye ziara kwenda maeneo yenye chimbuko la historia ya Kiswahili waone eneo
warabu walopokuwa wakipakizia bidhaa zao kwenye majahazi wakiwemo binadamu
maarufu watumwa kupelekwa bara Arabu na Ghuba ya Uajemi.
Ukifika utapata kuelewa mamwinyi na umarufu wao,kuliko
kusoma tu kwenye vitabu,ustarabu na utamaduni wa kiafrka wa pwani hiyo na
washirzi noa kuwepo kwa lugha ya Kiswahili,pia kuondoa dhana potofu ya kuwa
asili ya Kiswahili ni kiarabu au kibantu kwa kuangalia lahaja zilizokuwa
zikitumika pwani na wenzao wa bara.
Na kuyaona magofu yaliyojengwa kwa mawe matumbawe,yanye
asili ya majengo ya kishirazi.yalikuwa majengo imara hadi leo ushahidi
unaonekana,lakini kustawi kwa Kilwa Kisiwani kutakuwepo iwapo atapatikana
mwekezaji wa kujenga hotel ya kitalii kwenye kisiwa hicho cha
kihistoria,kilicho nunuliwa kwa kipande cha nguo kukizunguuka.
No comments:
Post a Comment