Saturday, February 12, 2011

KILWA KISIWANI FIKA UTEMBELEE UONE CHIMBUKO LA HISTORIA YA NCHI YETU

 Jinsi ya kuvuka kwenda kilwa kisiwani hapa ndiyo  Gati  ndipo utapata usafiri wa boti ya injini au ya Tanga kwa watalii wote hupelekwa ng'ambo na maboti hayo na wanaowatembeza watalii wapo kilwa masoko.
 hii ni sehemu ya ndani ya msikiti mkubwa ,uone jinsi warabu hao walivyo kuwa mahili katika ujenzi,lakini ikumbukwe walio jenga ni mababu zetu wakiwa kama watumwa.malighafi ni mawe meupe kama ya chokaa ndiyo yaliyotumika na matumbawe.
 Huo pia ni msikiti mdogo ambao masultani na familia zao walikuwa wakiswalia,na wafanya biashara wenzao.
 Ile sahemu  ambayo mtembeza wageni katika magofu hayo Bwana Samweli Gafao anayeonyesha,anaonyesha Kibla ya msikiti huo ambapo Imamu huwa anaazini wakati wa kuazini.
Usichoke kuona majengo ya misikiti,ni kutaka tu kutaka uone ufundi na umahili waliokuwa nao mababu zetu walivyo jenga majengo hayo karne ya 16 na kuendelea.Tuwe na tabia ya kuwa watalii wa ndani,kuona maeneo ya kihistoria,mbuga za wanyama,jiwe la kimodo na makaa ya mawe na samaki wa mapambo wa ziwa nyasa,wilaya mpya ya ziwa nyasa mkoa wa Ruvuma Tanzania.wageni karibuni sana.

No comments:

Post a Comment