Wednesday, February 23, 2011

NI MAMBO YA WATOTO HAYO,KUANGUKA KWA MTI NI FURAHA YAO

Camera yetu iliwakuta wanafunzi  hawa wa shule ya msingi Matarawe Manisoaa ya Songea Mkoani Ruvuma hivi karibuni , wakipanda juu ya matawi ya mti mkubwa uliyokuwepo shuleni kwao,ambao uliangushwa na upepo usiku wa siku hiyo.Hivyo kipindi cha mapumziko cha wanafunzi hao walipata nafasi ya mchizo wa kupanda kwenye matawi hayo na kutambiana ninani anaweza akawa bingwa wa kupanda kwenye miti?.Hayo ndiyo mambo ya  uanafunzi na Utoto wa utafiti wa kutaka kujua mambo hata ya hatari kwao.

No comments:

Post a Comment