Saturday, February 12, 2011

JUMAMOSI YA LEO TWENDE PAMOJA HADI KILWA KISIWANI MKOA WA LINDI TUKAONE MAGOFU YA MAJENG

 Ngome iliyojengwa na Wareno karne ya 16 kwa ajili ya kujilinda na maadui sehemu ya juu unayo iona Kilwa Kisiwani Wilaya ya Kilwa Masoko mkoani Lindi.Wareno walivyo kimbia utawala wa Kisultani,Masultani wa kiarabu waliendeleza. huku ni kwa nyuma ya ngome.Sehemu hii ni ya kitalii,katika ukanda wa pwaani ya Bahari ya Hindi.


 Hiyo ni ngazi ya kupandia kwenda chumba cha juu cha ngome hiyo wareno ndipo wakikaa wakiangalia maadui wanatokea upande gani wakiwa na maboti yenye Tanga.
 Huu ni msikiti  mkubwa ambao warabu walikuwa wakiswalia,ingawa msikiti huo ulijengwa karne ya 16 lakini hadi leo inaonekana kama ni magpfu ya mfupi,Nimeona leo nikuchukue wewe msomaji wa blog  tuwe watalii katika magofu ya waarabu kilwa kisiwani.kisiwa hiki ni chimbuko la Histori ya Afrika masharili,biashara zilianzia katika kisiwa hicho,utumwa,dhahabu,pembe za ndovu ambapo bidhaa zikiwemo watumwa ndipo walipo kuwa wakisafirishwa kwenda mashariki ya mbali Oman na kwingineko.
Hapo ni eneo walipo zikwa masultani wa kilwa,na kuna eneo jingine ambapo halijaoneshwa hapa ni mabinti wa masultani ndipo walizikwa hapo.

No comments:

Post a Comment