Thursday, February 17, 2011

WATU 20 WAPOTEZA MAISHA NA 184 MAJERUHI KUFUATIA MLIPUKO WA MABOM GONGO LA MBOTO DAR ES SALAAM

 Kufuatia mlipuko ya mabomu leo  usiku Gongo la Mboto Dar es salaam watu 20 wamepoteza maisha na 184 majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali za Amana. Temeke,kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi ASP Advera Sensor alisema hali ni shuali wananchi watulie hali haiwezi kurudia tena ,alisema wasisikie uvumi wa watu ambao hauna ukweli.Ametahadharisha iwapo mtu ataona kitu ambacho si cha waida watoe taarifa polisi.

Alitaja Mawasiliano ni Namba za simu za,0783-260334 au 0774- 039020 au 0755 -756410.maana kuna uwezekano wa baadhi ya mabaki ya mabomu hayo hivyo wawe waangalifu.
 Mmoja wa wafanya kazi wa Red Cross akimpeleka majeruhi kupata huduma ya kwanza katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam ambako wamewahifadhi wahanga hao.
 Huyu ni mfadhili mmoja kutoka kiwanda kimoja wapo cha magodoro amefika kiwanjanai hapo kutoa msaada wa magoro 300 yanye thamani ya shilingi 10,000,000/=.
 Huyo ni Mtoa huduma wa RedCross toka jana usiku yuko kiwanjani hapo akitoa msaada wa chakula na matibabu kwa wahanga,alisema watoto 179 wamepotelewa na wazazi wao.
 Wahanga wa mlipuko wa mabomu Gongo la Mboto wapo Uwanja wa Uhuru hawajui nini cha kufanya kufuatia hali ilivyo wakuta usiku huo wa balaa.
 Hawa ni baadhi ya waumini wa dini za kihindu wametumwa na mkubwa wao  huko India kuja kutoa huduma za kibinadamu kwa wahanga hao.
Hawa ni wahanga wako kwenye viti vya uwanja huo sio wanatazama mpira  bali ni machungu tu yamewakuta kufikishwa hapo walipo.Jumuiya ya TUJIFUNZE KUSINI inato pole kwa wote waliopoteza ndugu zao,waliopata majeruhi kadhaa Mungu awape unafuu mapema warejee kujenga taifa letu.

No comments:

Post a Comment