Sunday, February 20, 2011

HABARI NJEMA JUMAPILI YA LEO KWA WANADAMU,TUSIWE WATU WA KULIPA VISASI KWA WENZETU

 Katika kuazimisha misa katika kigango cha Matarawe Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma Padre Nicodemus Mbano,alisema katika mahubiri yake kuwa binadamu tusiwe watu wa kulipiziana visasi,kwa Mungu anafanyiwa makosa mengi na wanadamu lakini halipizi visasi ila anawapenda na kuwaongezea zaidi wakiomba.

Amesema visasi vikishamiri ndoa zinakuwa mashakani,isitoshe sikuhizi wanandoa kuachana imekuwa fashion,Aidha amewasifu waumini wa kigango cha Matarawe kwa jitihada zao.kikiwemo na kitabu cha kuendeshea ibada za misa ambacho amekishika.

 Padre Nicodemus Mbano  akimkabidhi mwenye mweka hazina wa kigango card ya kushiriki Jubilei ya miaka 25 ya Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea tarehe 9/6/2011.
Padre Mbano pia ni Padre wa miito mitakatifu jimboni.Bwana ni mwenye huruma,hivyo nasi tuwe na huruma kwa wenzetu..

No comments:

Post a Comment