Mvua zilipo chelewa wazee wa kingoni walikwenda kuomba mahoka kwenye makaburi ya machifu wa kingoni kwa jina maarufu Nkosi,Nduna kwenye Makumbusho ya Taifa ya Majimaji,na matokeo yake mvua zilinyesha,lakini ziliambatana na upepo mkali,nyumba zilibomoka,uribifu mkubwa pia ulifanyika.
Moja ya jengo la shule ya sekondari Muslimu hapa Songea,nusura liangukiwe na na mti huo kama unavyo uone.
Hayo mambo ya kuomba mvua yana maajabu. Nilisomea Seminari ya Hanga, 1963-66. Kuna wakati kulikuwa na ukame. Hapakuwa na dalili ya mvua wala mawingu ya mvua.
ReplyDeleteKatika mazingira haya, watawa wa Monasteri ya Hanga waliandaa maandamano ya kuomba mvua. Nasi waseminari tulishiriki. Amini usiamini, jioni hiyo hiyo mawingu ya mvua yalitanda na mvua ikanyesha. Sitasahau tukio hilo.
Profesa hayo ndiyo yalitutokea hapa kwetu,Lakini yameandikwa kili aombaye kwa jina langu atapata.Wale wazee walichinja kondoo nyama wakawapa wafungwa,na maombi yaliendelea.Lakini hakuna zuri likakosa ubaya.
ReplyDeleteNashukuru sana kwa maoni yako.