Thursday, June 30, 2011

MBUNGE AIOMBA SERIKALI KUPELEKA CHAKULA JIMBONI KWAKE

Mhe.Hussein Nassor Amar  Mbunge wa Matemwe  CCM aiomba serikali kupeleka chakula katika jimbo lake kwa sasa debe la mahindi ni shilingi 13,000/=,Amesa iwapo serikali haitapeleka chakula na kupunguza baei watu wa jimbo lake watakufa njaa.Maana jimbo hilo limekumbwa na njaa.
Aidha alisema walimu katika jimbo lake wanamatatizo makubwa ,yakiwemo ya Bima ya afya,walimu hao wamemtuma kuwa Bima ya Afya iwe hiyari kwani haiwasaidii na hawaitaki.pia alisema tatizo lingine ni upungufu wa madawati,nyumba za walimu na masilahi ya walimu hayatolewi kwa wakati.

Kilimo kwanza ndicho kitakacho mtoa mwananchi kwenye umasikini

 Mhe.Lucy Thomas Mayenga Mbunge Viti Maalum CCM amesema leo Bungeni wakati akichangia Hotuba ya Mhe.Waziri Mkuu kuwa Kilimo kwanza kama kikitekelezwa vizuri ndicho kitakacho mkomboa mkulima amabo ndiyo kundi kubwa.
Aidha Mhe. Mayenga amwemwagia sifa Rais Jakya Kikwete kuwa ni Mtu mwenye moyo mzuri,anacheka na kila mtu,hana kinyongo na mtu ni mtu mkarimu ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wame sisitiza sana kuhusu kilimo kwanza ,tatizo ni kwa watendaji wa kilimo kwanza waliyo kabidhiwa dhamana hiyo.

BUNGENI LEO MHE.RITTA KABATI AZITAKA HALMASHAURI ZITENGE MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA VIJANA

Mheshimiwa Ritta Enespher Kabati Mbunge Viti Maalum CCM Iringa,ameziomba Halmashauri kutenga maeneo ya kufanyia biashara vijana,na maeneo ya kuegesha Taxi zao.
Aidha ameiomba serikali kuangalia nyumba wanazoishi askari katika Mkoa wa Iringa haziridhishi kwani nyumba moja wanaisha familia zaidi ya mbili..
Mhe.Kabati amekerwa na maswali anayo ulizwa Waziri Mkuu amesema maswali mengine ni ya kumdhalilisha,ameomba kama maswali hayo yakiwa  ni ya kisera zaidi yapelekwe kwa Mawaziri wenye dhamana na hayo.

Wednesday, June 29, 2011

Malengo ya Mhe.Lucy Owenya la pigwa mkwala leo Bungeni.

Malengo ya Mhe.Lucy Phllemon Owenye hayakufanikiwa pale alipopigwa mkwala,kuwa masuala ya maadnamano ya CHADEMA yapo Mahakamani hivyo si vyema kuyazungumzia Bungeni.
Mhe.Owenya alikuwa akitaka kuelezea kuhusu maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo 
( CHADEMA ) Arusha yaliingiliwa na Polisi,kabala Mhe. Owenya ajaelezea mambo yalikuweje siku hiyo maana nayeye alikuwepo katika maandamano hayo ,aliambiwa aache kuelezea Bunge ingawa yeye ni hodari wa kujieleza,au atafute mbinu nyingine ya kujieleza.Je kuna haki kweli ya kujieleza Bungeni wakati wa kuchangia hoja? ikiwa nikikao cha bajeti,

MITI NI MUHIMU KUIPANDA KATIKA MAJENGO YETU KUZUIA UPEPO MKALI

Kupanda miti katika makazi ni jambo la busara sana kwani kuna faida nyingi zikiwepo za:-
  • kuzuia upepo mkali kuezua nyumba.
  • kuhifadhi unyevu katika maeneo yanayo izunguuka nyumba.
  • kuhifadhi unyevu kwenye maeneo yaliyopandwa mibuni,migomba na miwa kama inavyo onekana.
  • Lakini pia kupata mbao ,kuni,mkaa na boriti za kupaulia vibanda,kuni za kuchomia matofali na kupikia.

Tuesday, June 28, 2011

BREAKING NEWS ! Mikataba ya madini iangaliwe upya ili mwananchi anufaike na rasilimali yake



Viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini wameitaka serikali kuangalia upya mikataba ya madini iliyo wekwa awali ambayo haimsaidii mwananchi kutokana na mapato yatokanayo na madini hayo,badala yake huambulia kuona mashimo tu maeneo yanapochimbwa madini hayo.

Tamko la pamoja la viongozi hao wa madhehebu ya dini nchini lilitolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT ) ,Baraza la Maaskofu katoliki  Tanzania ( TEC ) na Baraza kuu la Waislamu Tanzania ( BAKWATA ),wote kwa pamoja waliitaka serikali kutazama upya mikataba ya madini kwa wawekezaji wa nje.

Aidha Viongozi hao walitamka hayo hivi karibuni kuwa haki ya kikatiba haikuzingatiwa kwenye mikataba hiyo ya madini, hivyo katiba haina budi kuandikwa upya ili maslahi ya pande zote yazingatiwe.

Walisema haki za binadamu katika maeneo  ya migodi haipo,haki za binadamu si suala la kisiasa,kama kuna raia amefanya makosa hatua stahiki za kisheria zichukuliwe,sio vyombo vya sheria  vinaibuka na kuanza kuhatarisha amani kwa raia wake.

Walisema athari zilizopo katika sekta ya madini zisipotatuliwa mapema ni hatari kwa umoja wa Taifa ( Source Mwananchi Juni 25 mwaka huu )

Monday, June 27, 2011

BREAKING NEWS CHILUBA ALIYEKUWA RAIS WA ZAMBIA AZIKWA LEO

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Zambia Frederick Chiluba amezikwa leo,Lusaka Zambia baada ya kupoteza maisha yake kufuatia kwa matatizo ya moyo.Rais Chiluba alianza safari yake ya kuiongoza Zambia kuanzia mwezi Novemba mwaka 1991 hadi Januari 2002. ( Source Lewes Mwanangombe )

BREAKING NEWS ABIRIA ZAIDI YA 600 WALIOKWAMA KWA SIKU TATU MKOANI TABORA KUANZA SAFARI LEO KUELEKEA KIGOMA KWA GARI MOSHI

Abiria waliokuwa wakisafiri kwa gari lamoshi  (Train ) Reli ya kati katiya Usinge na Nguruka kufuatia ajali ya gari la mizigo lililo anguka na kuziba njia, na kufanya gari la moshi kutoka Dar es salaam kwenda Kigoma na kutoka Kigoma kwenda Dar es salaam kukwama kwa siku tatu.
Wasafiri hao wanasema kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa kuwa abiria walikabiliwa na matatizo ya :-
  • Huduma ya choo hakuna
  • kushindwa kuoga
  • Hakuna chakula
  • Hakuna maji ya kunywa
  • vitu vimepanda bei vikiwemo chakula na maji ya kunywa.
Abiria wanaokwenda Kigoma wameondoka leo saa 1.30a wale wanaoelekea Dar es salaam watasafiri siku ya Juma tano saa 2.30 asubuhi.( Source TBC ) Nico Mwaibale.

TAMISEMI NI CHOMBO KIKUBWA SANA NA CHA MUHIMU KATIKA MAENDELEO YA WANANCHI

 Mheshimiwa George Simba chawene Mbunge  ( CCM ) akielezea umuhimu wa TAMISEMI katika kipindi cha Jambo Mjini Dodoma leo Kupitia TBC ,kuwa chombo hicho ni cha muhimu sana katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali nchini.

 Mheshimiwa Chawene alisema kuwa Ili chombo hicho kiweze kuwa na mafanikio katika kutekeleza miradi yake ni vyema Waheshimiwa madiwani wangepewa meno katika kufuatilia fedha zinazopelekwa kwenye Halmashauri zetu
 Mheshimiwa Regia Mtema mbunge Viti Maalumu CHADEMA,asema kuwa TAMISEMI ina watendaji wengi mmno  kama ilivyo maafisa tarafa watendaji wa vijiji kama VEO na WEO na Madiwani,ni bora wote hao waondolewe na majukumu yote waachiwe waheshimiwa madiwani.
Aidha Mhe. Mtema anasema kuwa visingizio vya kuwa Waheshimiwa madiwani wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu hawaja pelekwa semina ya kueleweshwa majukumu yao hiyo si kweli.
Alisema mara mtu anapokwenda kuomba achaguliwe kuwa Diwani ama Mbunge anatambua wajibu wakekatika kuomba nafasi hizo isiwe kizingizio cha kushindwa kutekeleza kwa sababu hawakupelekwa semina elekezi,yote hayo ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.(Source TBC kipindi cha Jambo).

KOMBE LA KAGAME SARE YA TAMBA KATI YA YANGA NA AL MEREIKH JANA

 Kikosi cha Yanga ya Dar es salaam kilicho pambana na Al Mereikh  ya Sudan  kutoka sare ya mbili kwa mbili ( 2 - 2 ) katika michezo ya kagame hapo jana.
 Kikosi cha Timu ya Al mereikh kilicho toana jasho na timu ya Yanga katika michezo ya Kagame hapo jana na kutoka sare ya mbili kwa mbili ( 2- 2 ) hadi kipenga cha mwisho alicho puliza refa aliyechezesha mchezo huo.
Mchezaji wa Al mereikh aliyekuwa akishangilia mara baada ya kufunga goli la kwanza la kuifunga timu ya Yanga hapo jana.

Sunday, June 26, 2011

JINSI MAHINDI YANAVYO NUNULIWA NA WALANGUZI VJIJINI NA KUPELEKWA NJE YA MKOA WA RUVUMA

 
 
Hivyo ndivyo wakulima wetu wanavyo languliwa mazao yao yangali yakiwa shambani ,kwa na walanguzi hao,kisha huyakusanya kwa bei ya chini,na wao huyasafirisha nje ya mkoa wa Ruvuma.
 Hayo ni mahindi yaliyofuatwa na wafanya biashara wa mazao ya chakula katika vijiji vya Madaba Mkoani Ruvuma wanayarundika hapo baada ya kuyakausha kwa jua.

JUMAPILI YA LEO ILIKUWA NI YA UTALII WA NDANI SAFARINI,MASHAMBA YA CHAI LUPEMBE NJOMBE

 Mashamba ya chai Lupembe Njombe ni ya wawekezaji wa Kiitalia ambao kutokana na mashamba hayo wananchi wa Mkoa wa Njoruma wanapata ajira ya kuchuma chai,kusafisha mashamba,Lakini kutokana na ukuaji wa teknolojia wawekezaji hao wanarahisha kazi ya uchumaji wa chai kwa kutumia mashine za kuchuma chai

Hivyo kitendo hicho cha kutumia mashine za kuchuma chai kunapunguza idadi ya wafanya kazi katika mashamba hayo ambapo hapo awali wananchi wengi waliajiriwa kama vibarua katika kazi ya uchumaji chai.

MASHAMBA YA NGANO YALIYOKO KILIMO UYOLE JIJINI MBEYA

 Hilo ni shamba la ngano ambayo imekauka na iko tayari kuvunwa kwenye shamba la kilimo Uyole Mbeya,ngano inastawi vizuri katika Mkoa huo.
Hilo shamba la ngano la kilimo Uyole mbeya ngano yake bado haija kauka,kwa hiyo kutokana na kilimo chao wamelima kwa awamu awamu ili zipishane katika kukomaa na kukauka na kuivuna ngano yao.

JUMAPILI YA LEO JIJI LA MBEYA LILIVYO

 Jiji la Mbeya kama linavyo onekana kutokana na camera yetu ilivyo chukua maeneo ya Soweto
 Majengo ya biashara maeneo ya Mwanjelwa Jijini Mbeya

Njia panda ya kwenda  Tukuyu, Uyole Jijini Mbeya camera yetu ilivyo pata picha hii wakati Blogger wetu akiwa safarini toka Mbeya kwenda Songea.

Saturday, June 25, 2011

UKISHANGAA YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI

Ni kitu cha kawaida katikamaisha ya kilasiku kwa binadamu,Watu wanasema mkimbie binadamu kuliko simba anaweza akakusamehe.
Bali binadamu akikukamia jambo kuwa lisifanikiwe,atajitahidi hadi usifanikiwe,iwe kwa nguvu zake,fedha,Supernaturals power basi  ili  ikikosa kufanikiwa yeye anafurahi kuwa amamkomoa.Lakini ukifuatilia watu kama hao hawana ujira wowote katika kujituka kwao katika kuharibu.
Sasa  watu kama hao katika Jamii wanakuwa na nafasi gani?,je wanakuwa na usalama gani katika maisha yao ?,Watu wametofautiana katika busara,je wakiwafanyia mambo kama hayo kwa watu wenye busara hafifu watakuwa katika hali gani?Na wanapo waharibia wenzao  wao wananufaika na kitu gani?

Hayo ni matukio yanayowatokea watu wengi wanao paga mipangilio yao kisha ikaharibiwa na watu kama hao dakika za mwisho na watu wakabaikia midomo wazi.Je huo ni ungwana?

MAMBO MOTOMOTO JIJI LA MBEYA JUMAMOSI YA LEO

Wasomaji wa blog hii nawatakia Jumamosi njema,na kupata habari motomoto kutoka jiji la mbeya,ukweli Mji ukisha kuwa Jiji mambo mengi yatajitokeza.
Jiji hili sasa lina show room za magari kwa wale wenye kutaka kununu magari Soweto na nyingine Ilomba (CCM ) ,huvyo wenye nia na haja ya kupata magari basi watafika Jijini Mbeya katika Show room za Soweto na Ilomba.
Una juwa wengi wao walikuwa wakienda D'salaam kufuata magari ya kununua kwa matumizi yao ama ya ofisi,hivyo ili kupunguza gharama Jiji la Mbeya sasa magari yapo.

Sunday, June 19, 2011

JUMAPILI YANLEO NI PEKEE KATIKA KANISA KUU LA JIMBO KUU LA SONGE,KWA KUMSHUKURU BWANA HAMISSI SADI AU KANGA ULAYA KWA MSAADA WAKE

Familia ya Bwana na Bibi Hammis Sadi ( Joice Lugongo) Bila kujali madhehebu ya dini wao walitoa basi lao,bila malipo yoyote  ili kuwasafirisha mahujaji wa Kitume wa Fatima kwenda Mbeya kwenye kanisa la hija,

Mwenyekiti wa chama cha kitume cha Fatima aliwashukuru zana kwa moyo waliyoutoa wa kutoa basi lao ambalo lilikuwa Mbeya na lilifanya shughuli za kitume kwa muda wote wa siki 5,Mungu awazidishie baraka alisema mwenye kiti huyo.
  Bibi Joice Lugongo alimwakilisha Mmewe kupokea shukrani hizo pia kuwasalimu waumini walisali ibada ya ya pili katika kanisa hilo leo.


leo ni siku ya Mtoto wa Afrika je ,watoto wanapewa haki zao za msingi?

Leo ni siku ya Mtoto wa Afrika lakini kuna baadhi ya watoto,wako kwenye mazingira magumu,hatarishi,wanatumikishwa kazi kwenye migodi,kwenye uvuvi,kwenye ajira mbaya ya kuudhalilisha utu wao,wengine wamejiingiza kwanye madawa ya kulevya.

Lakini jamii inasema nini kuhusu watoto hawa,Pole kwa wale amboa wamepoteza wazazi wao wote,je jamii inawachukuliaje hawa?,lakini pia kuna baadhi ya watoto hawa wazazi wapo,wana nguvu,kutunza hawataki,waliwazaa wanini?
Watoto wanahitaji huruma yako na yangu,mtoto wa mwenzako ni wako,ingawa siku hizi usemi huo hauingii masikioni mwa watu,ukitamani kumweonya mtoto wa mtu anapokosea,utakijua kilicho mfanya mbwa abweke.Maana atakujia mama yake,shangazi shoga watakuanadama hata ukose amani.Lakini tusikate tamaa.

Wednesday, June 15, 2011

MASHINDANO YA MICHEZO YA SHULE ZA MSINGI MKOANI RUVUMA IMEFUNGWA LEO KATIKA CHUO CHA UALIMU MATOGORO SONGEA

Mashindano ya michezo ya shule za msingi Mkoani Ruvuma imefungwa leo katika Chuo cha Ualimu Songea Matogoro ambapo wanafunzi kutoka wilaya zote katika mkoa huo walijumuika katika kuandaa michezo hiyo,tayari kwa kwenda kushindana katika ngazi ya  Taifa.

BREAKING NEWS ! ! ! KUPATWA KWA MWEZI HAKUNA MADHARA KWA WATAKAO UTAZAMA LEO

Mtaalamu wa Sayansi kutoka Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania ( Open University of Tanzania ) Dkt Norarild Haji alisema hayo alipo hojiwa na TBC leo.

Alisema Mwezi kupatwa kwa mwezi ni kitendo cha mwezi kupita katikati ya Kivuli,ambapo mwezi umepatwa kuanzai saa 3.23 itachukua muda wa saa moja hadi saa 4.20.kupatwa kuhu kwa mwezi ni kukubwa ambapo haijawahi kutokea kwa miaka 10.

Hivyo wote wenye kutaka kuangaliwa jinsi mwezi unavyo patwa washuhudie wenyewe,wala wasiwe na wasiwasi kwani hakuna madhara yoyote.( source Dr.Norarild Open)

Tuesday, June 14, 2011

BREAKING NEWS WANAFUNZI 1,200 UDOM KULIPWA MADAI YAO

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prf.Philipo Mulugo alisema hayo jana wakati wa maswali na majibu Bungeni,ambapo wakati kipindi hicho cha maswali na majibu kinaendelea,wanafunzi wa UDOM tayari walikuwa nje ya ukumbi huo kwa maandamano yaliyo ya  sambaratishwa na Polisi.
Aidha Prf.Mulugo alisema  walioko kwenye Progam 13  watapata fedha zao,alisema serikali itawalipa wanafunzi wote waelimu ja juu wanao omba fedha   kwa ajili ya masomo.
Pia alisema kuwa kiasi cha fedha wanazopata wanafunzi wa elimu ya juu hakitoshelezi hivyo kitaongezwa bila ya kutaja kiasi kitakacho ongezeka.

Sunday, June 12, 2011

BREAKING NEWS !111JUKWAA LA WATOTO -KAMA HAKUNA MAKTABA WATU WATASOMA NINI ?

Jukwaa la Watoto leo wameuliza mambo kadhaa na kutafuta ufumbuzi wake kama ifuatavyo:-
  • Kama shule haina maktaba  wanafunzi watasoma nini?
  • Mwanafunzi kama hapati chakula shuleni je Atamwelewa mwalimu darasanai?
  • Iwapo vifaa vya kujifunzia na kufundishia havipo shuleni,taaluma itaacha kushuka ?
  • Walimu kama hawana nyumba za kuishi ,je wataweza kufundisha vipindi vyote ?
  • Mwanafunzi akikaa chini darasani ,je ataweza kumsikiliza mwalimu sawasawa na yule aliye keti kwenye dawati?

Furahia kwaya za dini Mbinga na songea katika ibada Jumapili ya leo

 Jumapili ya leo kwaya hii mchanganyiko katika Jimbo kuu la songea imeimba katika ibada ya kwanza na ya pili kwenye kanisa la Mathias Mulumba Kalemba.

Hiyo ni kwaya ya Porokia ya Mji mwema katika Manispaa ya Songea ambayo nayo imeimba katika Parokia hiyo  katika Ibada ya Juma pili ya leo.


Ibada iliyofanyika katika kanisa la  Jimbo la Mbinga kwaya iliyokoleza ibada,katika kuinjilisha kwa nyimbo na sala.

Saturday, June 11, 2011

MATUKIO YA WIKI HII SONGEA KWENYE JUBILEI YA NORBERT MTEGA

 Askofu Mtega akikata keki

 Kwaya iliyotumbuiza wakati wa Ibada ya Jubilei ya Askofu Norbert Mtega
 Baadhi ya Maaskofu
 Rais Mstaafu Willium Mkapa  katika picha ya pamoja
 Muadhama Polikapi Pengo
 Askofu Mtega akizawadiwaakizawadiwa vitu mbalimbali
 Mkapa akihutubia maaskofu ,mapadre,watawa na waumini kanisani Songea siku ya Jubilei ya Mtega
Rais Mstaafu Mkapa akibusu pete kisha akaaga kwenye hafla ya kumpongeza Mtega Bombambili Songea

JUMAMOSI NJEMA NA SUMMARY YA MATUKIO SONGEA MBINGA WIKI HII

 Songea Rais mstaafu alitangulia kutua Air port Songea
 Baadaye alitua Rais Jakaya Kikwete wote walielekea Mbinga
Madiwani wa manispaa ya Songea walifika kwenye mapokezi
 Rais Kikwete mara baada ya kushuka kwenye ndege na hajavishwa skafu
 Kanisa la Jimbo la mbinga aliposimikwa uaskofu Askofu John Ndimbo mgeni rasmi alikuwa Jakaya Kikwete
 Kanisani Rais Mstaafu ,Mkewe na Rais Kikwete na viongozi wengine wa serikali kanisana Mbinga
 Baadhi ya Maaskofu
 Askofu ndimbo akitoa baraka mara baada ya kuwekwa wakfu
 PICHA YA PAMOJA