Tuesday, February 1, 2011

SLAA ATANGAZA MAANDAMANO YA AMANI KWA NCHI NZIMA

Katibu mkuu wa CHADEMA Dkt Slaa ametangaza maandamano ya amani kwa nchi zima kwa wabunge wa chama chake,wanachama wa chama hicho kupinga serikali kuiilipa Dowans.Mambo hayo,hizo ndizo changamoto za kisiasa.

1 comment:

  1. Mimi niko huku ughaibuni, lakini nami napinga kuilipa Dowans. Sababu yangu ya msingi ni kuwa sijapata uthibitisho kama Dowans ni kampuni halali. Ninasikia kuwa ni kampuni hewa, hata huku inakosemekana imesajiliwa, yaani Costa Rica. Na serikali ingepaswa kunithibitishia kuwa hii kampuni imesajiliwa kihalali. Vinginevyo, napinga kulipwa Dowans.

    Suala la pili ni kuwa nataka waliosababisha matatizo yote hayo, tangu mwanzo wawajibishwe. Kama ilikuwa ni ufisadi au ujinga wa kutoweza kusoma mikataba na kuielewa, ufisadi au ujinga wa kusaini mikataba iliyokuja kutuletea matatizo baadaye, hao wawajibishwe.

    Hili suala la mikataba lina vipengele vingine. Kwa mfano, kuhusu mikataba ya madini, serikali imekuwa ikituambia kuwa mikataba mibovu ya madini imerekebishwa au inarekebishwa, ili Taifa lifaidike na madini yetu.

    Serikali hii inatutaka turidhike na maelezo hayo. Mimi siridhiki hata kidogo, kwa sababu nataka nijue ni kwa nini mikataba mibovu ilisainiwa, hadi tuwe tunaongelea kuirekebisha. Wale waliosaini walikuwa na akili timamu au walikuwa wamelewa gongo, au walikuwa ni mafisadi? Serikali isikwepe suala hili.

    ReplyDelete