Wednesday, February 27, 2013

MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI UKOMBOZI KATIKA MANISPAA YA SONGEA ATEMBELEA KITUO CHA TUJIFUNZE KUONA JINSI KINAVYO FANYA KAZI

 Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ukombozi katika Manispaa ya Songea Bibi Emeld Mbawala akipata maelezo ya mashine ya uchapishaji wa magazeti kanda ya kusini Songea kutoka kwa mhariri msaidizi Bw, Juma Nyumayo alipotembelea kituoni hapo jana.
 Bibi Mbawala akizungumza ofisini kwa Mhariri Kanda ya Kusini Songea kabala hajaende kutembezwa kiwandani hapo jana.
Bibi Mbawala akiuliza jambo kwa fundi mchapaji hayupo katika picha jinsi mashine inavyo chukua karatasi na kupelekwa kuchapwa.

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MASHUJAA RSONGEA RUVUMA LEO

 








 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Joel Bendera akisalimiana na mwandishi wa habari na mhariri msaidizi wa magazeti vijiji Kanda ya Kusini  ,na pia Ripota wa Radio UHURU FM Bw.Juma Nyumayo katika viwanja vya makumbusho ya majimaji Manispaa ya Songea leo.
Mhe. Balozi Khamis Kagasheki  Waziri wa Maliasili na Utalii mwenye mgolole mweupe akiteta jambo na wakuu wa mikoa ya Ruvuma na Morogoro leo Katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji katika Manispaa ya Songea leo.

MHE. BALOZI KHAMIS KAGASHEKI ATAKA MAKUMBSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI SONGEA YATUNZWE ILI KUVUTIA WATALII


 Picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Hkamis Kagasheki  wa kwanza kulia mwenye kitambaa cheupe,wakatikati ni mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu na tatu kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera kwenye makumbusho ya Taifa ya Majimaji Manispaa ya Songea leo.

 Picha ya pamoja na wazee wa mila wa makumbusho ya majimaji

 Picha ya pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Ruvuma waliyo simama nyuma.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Kagasheki ametaka Makumbusho ya Taifa ya Majimaji katika Manispaa ya Songea yatunzwe yawe katika hali ya usafi ili yawe kivutio kwa watalii ambao watatembelea makumbusho hayo kusini mwa Tanzania.

Amesema kuwa Maazimisho ya siku ya Mashujaa katika Makumbusho ya Taifa Mahenge ni muhimu sana kwa ajili ya kuwakumbuka  mashujaa wa Kingoni waliponyongwa kwa kamba hadi kufa na Wajurumani baada ya Watemi hao kukataa kufanyishwa kazi na Walowezi hao, ambapo sasa eneo hilo pamejengwa mnara. Wa kuwakumbuka.
Pamoja na mambo mengine maadhimisho hayo yalianza mwa maandamano kuanzia kwenye mnara waliponyogewa wazee wa kingoni,ambapo paliwekwa silaha walizotumia wazee hao zikiwemo,Nago.kishoka ( Kinjenje ),na Mkuki
Baada ya hapo kuelekea kwenye makumbusho ya Taifa ya Majimaji ambako kuna kaburi moja walilizikwa wazee hao wa kingoni wapatao 66,viongozi wa dini walitoa dua zao kuwakumbuka wazee hao.

Tuesday, February 26, 2013

KISIWA CHA AMANI TANZANIA SASA KINATAKA KUWA KISIWA CHA BALAA SOMA UJUMBE HUO UNAOSAMBAZWA KWENYE SIMU ZA WATU JE KAMA NI KWELI WAKRISTO WAIHAME NCHI YAO ?, NA SERIKALI INAPATA UJUMBE MBALIMBALI UNAOTISHIA UHAI WA WATANZANIA?

NANUKUU Ujumbe huo,'Tahadhali kundi la waislamu toka Dar, Tayali limeshawasili mikoani  kwa ajili ya kuja kubomoa na kuchoma makanisa, tunatakiwa makini tuwapo makanisani hata katika kazi zetu, usipuuzie ni taarifa kutoka Jimbo kuu la Dar es Salaam. Wajulishe Mapadri,Watawa na makatekista, Wachungaji, Wainjilisti, Mapastor na wakristo wote, ni vema na haki kusambaza ujumbe huu kwa kasi zaidi na kuwajulisha wakristo wote, upatapo ujumbe huu tuma kwa waombaji 12.
   Na si ujumbe huu tu bali kuna mahubiri katika baadhi ya Miskiti ambayo yanatishia amani kwa wakristo na CD zipo zinaonyesha kwa kiasi gani Madhebu ya Kikristo yanavyo pigwa vita na kutishia amani katika uhai wao, Je Serikali inalifahamu hilo,kama lina fahamu ni hatua zipi zinachukuliwa ili kunusuru uhai wa wakristo nchini?.
  Mbona matokeo mabaya ya kidato cha nne tunasikia Tume imeundwa kutoka Zanzibar kuna wajumbe watatu ( 3 ) ?, nini zaidi kutishiwa kwa uhai wa watu au Kufeli kwa wanafunzi?, Inasikitisha  sana huwa tunasikia tu Mashariki ya Kati sasa tunaona Live Emungu tutaukumbuka maneno ya Baba wa Taifa kama  kuna ukweli wowote kwa watu wanaosambaza ujumbe huo.
 Na kama hakuna ukweli kwanini waendelee kusambaza na serikali inawafumbia macho wasambazaji?

Sunday, February 24, 2013

Majimaji 3 polisi Iringa 2 katika uwanja wa majimaji

 Hicho ndicho kikosi cha timu ya Wana- Lizombe Majimaji ya mkoani Ruvuma iliyoilaza Polisi ya Iringa 3-2 katika uwanja wao wa nyumbani wa majimaji.
 Mgeni rasmi katika mechi hiyo Injinia Steven Shauri akisalimiana na wachezaji wa timu ya majimaji wakati wa kukagua timu.
 Hicho ndicho kikosi cha wanausalama Polisi Kutoka Iringa ambao kabla ya mchezo wa leo walikuwa wa pili kutoka City Mbeya ambayo ilikuwa ikishikilia nafasi ya kwanza katika michozo ya Ligi daraja la pili.Ambapo majimaji walikuwa watatu katika msimamo wa ligi,Lakini baada ya kushinda leo Majimaji ipo katika nafasi nzuri.
Injinia Steven Shauri akisalimiana na wachezaji wa timu ya Polisi Iringa katika uwanja wa majimaji leo ambapo wameshindwa kutamba mbele ya wana lizombe hao wa Majimaji. walipochabangwa bao 3 kwa 2.



TIMU ya soka  ya Majimaji imefunga timu ya Polisi Iringa magoli 3 kwa  2 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa majimaji mjini Songea leo katika ligi ya daraja la pili.

Mchezo ulikuwa wa vuta ni kuvute katika dakika ya 14 Polisi Iringa ilianza kuliona lango la Majimaji kupitia mchezaji wake Demoso Mbalika jezi namba 11 mgongoni,Lakini katika dakika ya 19 majimaji ilisahwadhisha goli hilo kupitia mchezaji wake Sixmundi Mwasikaga namba 15.

Mambo yalikuwa hivyo ambapo katika dakika ya Tito Sanga  namba  2  aliipatia timu ya Polisi Iringa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 22 , katika patashika hiyo naye mchezaji wa majimaji Edward Philipo Songo  jezi namba 10 alilisawadhisha bao hilo katika dakika ya 24. Hadi kipenga kupigwa katika kipindi cha kwanza ilikuwa Majimaji 2 na Polisi Iringa 2.

Katika kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanjani kwa nia ya kupata ushindi ukizingatia Polisi Iringa Ilikuwa ya pili katika msimamo wa Ligi ya daraja la kwanza nyuma ya Mbeya City inayo ongoza Ligi hiyo ambapo majimaji walishika nafasi yatatu, kabla ya kushinda mechi ya leo.

Katika dakika ya 59 kipindi cha pili majimaji ilipata bao la tatu kupitia  mchezaji wake Edward Songo,goli ambalo lililoipaia majimaji ushindi wa magoli 3 – 2 hadi kipenga cha mwisho. Wakati Pilisi Iringa ilipata kadi 1 na Majimaji kadi 3.

Kutokana na matokeo hayo yamezidi kuiweka majimaji katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.Maji maji itakuwa na kibarua kingine na timu ya Mkamba kutoka Kilombero tahere 2/3/2013, tarehe 9/3/2013 na JKT Mlale na tarehe 13/3/2013 na Mbeya City.

Monday, February 18, 2013

ASKOFU DR.VALENTINO MOKIWA AITAKA SERIKALI KUJADILI MAUAJI

 Askofu Dkt Valentino Mokiwa katika mahojiano na vyombo vya habari kuhusu mauji yanayoendelea nchini ya baadhi ya viongozi wa madhehebu fulani ya dini,amesema Serikali ikae na viongozi wa dini zote kujadili suala hili la kikatili linaloendelea Tanzania Bara na Visiwani.
Naye Bwana Huyo alivyo hojiwa na ITV jana kuhusu mauaji yanayo endelea,alisema Serikali ifanye msako wa kuwasaka wauaji,kwa kuwa amani inazidi kutoweka miongoni mwa Wa- Tanzania, 'erikali bado haijachukua hatua za kuosha kukomesha mauaji'. Alisema Bw. huyo.

DKT SHUKURU KAWAMBWA ATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 789 WAFUTIWA MATOKEO YAO

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru Kawambwa leo ametangaza matokeo ya kidato cha nne,amesema matokeo ya ni mabaya sana ikilinganishwa na matokeo ya nyuma. Hasa kwa masomo ya sayansi sababu shule nyingi za vijijini hazina maabara wala walimu wa kufundisha masomo hayo.
Aidha Mhe.Kawambwa amesema wanafunzi 789 wamefutiwa matokeo yao kati ya hao 624 wa shule za serikali na wanafunzi 148 wa kujitegemea na 17 wa wanaojiandaa kwa mitihani.kwa sababu ya udanganyifu wengine wemeingia katika chmba cha mitihani na madaftari na waliyoshindwa kabisa kujibu maswali katika mitihani hiyo waliamua kujaza matusi.
Sasa ninani wa kulaumiwa?,wanafunzi,wazazi ,walimu,au viongozi wa Elimu? Tutafakari sana kuhusu hilo,sekondari ni nyingi na matokeo mabaya ni mengi vilevile,ni elimu au bora elimu? ni wakati wa kubangua bongo watanzania kila kona ni matatizo lukuki.

HIVYO WENYE HAKI YA KUISHI NI VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU PEKE YAO , TANZANIA ?, TANGU MAUAJI HAYO YAANZE NCHINI UMEWAHI KUSIKIA KIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU KAUAWA NA WAKRISTO ? TATIZO LIKO WAPI ?

Hayati Padre Evaristus Mushi,jana kafikia mikononi mwa Ibilisi wakati akienda kusoma misa ya Ibada takatifu huko Unguja,Tukioa la kwanza ni kuchoma makanisa hakuna aliyeshtuka,lakini hatukusikia misikiti imechomwa moto,la pili Padre kavamiwa na kujeruhiwa hili nalo halikuchukuliwa mkazo,utadhani ni paka alikoswakoswa kuuawa,sasa funga kazi ni lajana la kumpiga risasi na kumuua padre wa watu.

Wakati Kamanda PC Mussa Ali Mussa wa Zanzibar anadai watu kadhaa wamekamatwa kwa mauaji hayo,ila hajui ni akina nani wanahusika na wimbi la mauaji na vurugu katika Kisiwa hicho,wala wa kuwatuhumu hawa jui na wala hawezi kusema ni sababu ya kisiasa au kudini, Hapo suala la kisiasa halipo kwa asilimia kubwa taka usitake,lakini yote kwa Mungu.

Ja Serikali ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar imetamka nini kuhusu hilo? , unadhani ni jambo la kawaida hilo ? ,je Kuna siri gani imejificha katika Fasihi hii ?. Kumbe tukiona mbwa amekenua meno tusidhani kuwa amefurahi, anaweza akatung'ata ?.kumbe ni kweli wakati wa biashara ya watumwa uhai wa mtu ulikuwa mikononi mwa mtu mwingine mwenye uwezo na siyo Mungu aliyetuumba?.E Mungu uwasamehe watu hao hawajui walilolitenda kwa Marehemu Mushi,na ilaze roho yake mahali pema peponi Amina.


SUALA  la mauaji wa viongozi wa Dini ya madhehebu ya Kikristo yanaendelea, na hakuna hata siku imetokea wauaji wamekamatwa, ila Serikali inasisitiza tu kuwa  walaifu wasakwe na wakamatwe mara moja basi muda utapita hakuna kinacho endelea.

Swali linakuja,hivyo tangu mauaji hayo yametokea ni lini umesikia kiongozi wa Madhehebu ya Kiislamu kauawa au amepigwa? Au ni lini umesikia misikiti imechomwa moto zaidi ya Makanisa ? Kama msomaji, hujapata kusikia vipi hili limetokea na linazidi kutokea serikali halilioni hilo, utadhani wanaofanyiwa hivyo ni wanyama wasiyo na thamani ya kuishi katika nchi hii ambayo  inaitwa kisiwa cha Amani,amani imetoweka,ni kazi kweli kuirudisha kwa mtindo huu unaoendelea

Hivyo Tanzania wanaotakiwa kuishi kwa amani ni waislamu peke yao ? .Ingawa wauaji hao sina uhakika kuwa ni wa kutoka dhehebu gani ,lakini yamkini ni kutoka katika Dhehebu hilo.

Tunaianzisha Tanzania ya matabaka ya udini ambayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyapiga vita vikali.Tunahangaika na kitu gani,kila mtu anaimani yake ambayo anafikiri akiifuata hiyo itampeleka peponi,isitoshe wote tuna mwabudu Mungu mmoja ingawa kila taifa lina jina lake wanalomwita Mungu wao.

Mitume wote  waliyo tumwa na Mungu kuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini binadamu wa karne hii tunawaumini tu, wala hatuwahi kuonana nao wala siyo kutoka katika makabila yetu bali ni imani tu ya kuwaamini,lakini sisi kwa sisi ambao wote hawaja kutana nao uso kwa uso tunauana, niushabiki usiyo na maana wala busara,kwani hakuna mwenye haki ya kucheza na uhai wa mwenzake, kazi hiyo tumwachie Mungu.

Hivyo basi  serikali yetu sikivu iliangalie kwa macho ya karibu matukio hayo, watu wa madhehebu ya kikristo wanaishi kwa mashaka, kwani nchi hii inatawaliwa na serikali ya kidini?,kama serikali inaweza kutenga maeneo ya wakulima na wafugani ,kwanini sasa wasitenge maeneo ya madhehebu Fulani peke yao ili wasichanganyike nao kuwe  na amani katika kuabudu kwao.Haipendezi inasikitisha sana tunachoka kusikia historia hiyo hiyo kila wakati. ( Padre Evaistitus  Mushi ) maskini alikuwa akienda kuendesha ibada, matokeo yake kafikia mikononi kwa Ibilisi. Poleni Familia ya Padre Mushi.





Sunday, February 17, 2013

JENGO LA RADIO MARIA SONGEA NA MADHARI YA KANISA KUU LA SONGEA

 Jengo la kurushia matangazo la Radio Maria Songea
Madhari ya kanisa kuu la Songea

WALIOKOSA KUPAKWA MAJIVU JUMATANO YA MAJIVU KUPAKWA LEO

Padre Mtalemwa pia Lecturer of History akipaka majivu waumini ambao siku ya Jumatano ya majivu hawakuwahi kupakwa.Padre anasema 'Tubuni na Kuiamini Injili" Ina maana kuwa binadamu ni mavumbi,na mavumbini atarudi
Kwaresma ni kipindi cha mfungo na majuto ya kumrudia Mungu kuomba toba kwa yale matendo ambayo hayampendezi Mungu.Kutokana na udanganyifu wa shetani,kwa kuwa katika siku 40 Bwana wetu Yesu Kristo alijalibiwa na ibilisi mara tatu na kumshinda.na hata haivyo aliondoka na kumwacha kwa muda.
Ibilisi hachoki katika majaribu yake ili ahakikishe anakuingiza kwenye dhambi,ndipo anapo furahi,kwa hiyo binadamu anajaribiwa na ibilisi kila siku hadi anapoingia kaburini.

TUNAWATAKIA KWAREMA NJEMA WATAKAO JALIWA KUFUNGA KATIKA MFUNGO WA KWARESMA SIKU 40.LEO IKIWA JUMAPILI YA KWANZA YA KWARESMA

 Paroko msaidizi wa Parokia ya Jimbo kuu la songea Padre Otieno akipokea vipaji kutoka kwa Jumuiya ya Mtakatifu Joseph ya Mfaranyaki  katika ibada takatifu ya kwanza leo katika kanisa kuuu la Mt.Matias Mulumba Kalemba Songea.
 Vipaji
 Vipaji
Rv.Father  Otieno akitoa baraka baada ya kupokea vipaji hivyo

MKANDARASI MZURI WA KUTENGENEZA BARABARA KWA KIWANGOCHA LAMI NIPAMOJA NA VIFAA.LEO NIMEBAINI MALORI YA WATENGENEZA BARABARA YA SONGEA MBINGA KIWANGO CHA LAMI

 Blog hii leo imekutana na malori ya kampuni ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Songea hadi Mbinga,ni dalili kuwa kazi imekamilika,wakati waliopewa kipande cha Namtumbo hadi Tunduru ni kitandawili. tupu hakuna kinaccho endelea,
 Malori yakitoka Mbinga kuja Songea leo asubuhi hapa mjini
Si hayo matatu tu bali yalikuwa zaidi ya sita

Saturday, February 16, 2013

HISTORI YA MWAMBAO MWA PWANI YA MKOA WA LINDI NA USTAARABU WA KIARABU KATIKA MAJENGO YAO



JUMATANO YA MAJIVU NDIYO SIKU WAUMINI WANAO MWAMINI KRISTO WANAANZO SIKU 40 ZA TOBA ZA KUJUTA MAKOSA YAO,KESHO YAKE IKAWA SIKU YA WAPENDANAO KATIKA MJI WA SONGEA

 Hivyo ndivyo siku ya wapendanao ilivyo kuwa katika manispaa ya Songea ,ambapo jana yake ilikuwa siku ya majivu kwa wale wanaomwamini Yesu Kristo ambapo alifunga siku 40 jangwani.Basi ni wakati sasa wa kujirudi na kujuta makosa ambayo binadamu kamkosea Mungu.
 Blogger alipita mitaa ya Kanisa la Anglican katika Manispaa hiyo hakusita kuona jengo la kitega uchumi la Chama Cha Walimu Tanzania  ( CWT ) kuonyesha pamoja na siku ya majivu lakini bado tunamshukuru Mungu kwa Maendeleo yanayo fanya katika Manispaa hiyo.
Hatimaye Blogger alifutiwa na utitili wa mitandao ya simu kwenye miamvuli nje ya soko Kuu la Manispaa ya Songea.hiyo ni kuonyesha ni kwa kiasi gani mitandao inavyo shindana katika kuwavutia wateja wake.Ruvuma Inavuma na Mbinga ni Mbinguni kwa Kahawa,Makaa ya mawe na vivutio lukuki.

Breaking newsssssssssssss.Upepo mkali uliyoandamana na mvua ya mawe iliyonyesha leo katika Manispaa ya Morogoro yasababisha hasara

Upepo mkali uliyoambatana na mvua ya mawe iliyonyesha kwa masaa mawili katika Manispaa ya Morogoro leo imesababisha hasara kubwa kwa wakazi wa Manispaa hiyo.
Source wa chanzo hicho mwanachuo cha uandishi wa habari Morogoro ,anasema upepo huo umeezua nyumba nyingi za wakazi wa Manispaa ya Morogoro,karibu maeneo mengi ya Mji huo,Tunigi,Nanenane,Mjipya,Kihonda kwa chambo, na maeneo mengine ambapo upepo na mvua hizo zilinyesha.
Hadi tunazipata taarifa hizo kiasi cha hasara hakijatambulika mpaka pale uongozi wa mkoa huo utakapo fuatilia kuona jinsi wananchi walivyo athirika na mvua hiyo.

Thursday, February 14, 2013

NI SIKU YA WAPENDANAO INAKARIBIA KUMALIZIKA NAWAPA HONGERA WAPENDANAO WOTE WANAOTEMBELEA BLOG HII

 MRS Sikapundwa and her last born Emanuel Sikapundwa and two grand children
 Lovely flowers for Valentine day
 MRS Sikapundwa and her Sarah Sikapundwa at Dodoma -Tanzania
 Baby boy Cal max Joseph Sikapundwa grand son  Dodoma
 Blogger Mr Christian Sikapundwa ,Happy day finished.
Mr and Mrs Sikapundwa at Valentine day.I like it.

JAMII IMETAKIWA KUACHA KUWANYANYAPAA VIJANA WALIOACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA JIJINI DAR ES SALAAM

Baadhi ya vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya Jijini Dar es salaam ,Wakitoa kilio chao kwa serikali cha kuwapatia shughuli za kufanya ili wasirudie tena kwenye utumiaji wa madawa hayo.
Vijana hao ili jamii iwatambue na kuwakubali kuwa ni vijana wema wamefanya shughulu za usafi,katika kituo cha uhamasishaji wa kuacha madawa ya kulevya (SOABAR ) na sokoni
 ( Source ITV )

HUDUMA ZA UHAMIAJI MKOANI RUVUMA ZINATIA FORA KWA WATEJA WAKE

 Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Bw.Shaaban Omar mwenye miwani ankiwa na Mhariri  Msaidizi wa TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Bw.Juma Nyumayo wakiwa kwenye Mtandao wa Internet katika ofisi ya Uhamiaji Mkoa leo.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Bw.Shaaban Omar mwenye suti nyeusi akizungumza na Mhariri wa TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Bw.Christian Sikapundwa katika ofisi ya Uhamiaji leo Mjini Songea.



NAIBU Afisa uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Shaaban Omar amethibitisha hayo ofisini kwake leo alipotembelewa na Blog hii kutaka kuelewa shughuli zao katika kuhudumia wananchi na wageni kutoka nje ya nchi.

Bw. Omar amesema ofisi yao inajitahidi kuhudumia wateja wanao kwenda kuhitaji huduma zao.

Ametaja huduma ambazo wanazitoa ni pamoja na  kutoa hati za kusafiria ( Pass Port ).kutoa Visa kwa wageni,kutoa hati za muda mfupi kwa wageni ambao watahitaji kufanya shughuli zao zikiwemo za kufanya kazi za kijamii,kuanzisha mchakato wa utoaji wa Uraia, ambapo katika utoaji wa vitambulisho vya taifa wao ni wadau.katika masuala ya upatikanaji wa vitambulisho vya taifa vya Uraia.

BAADHI YA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WAMEKANUSHA KUWEPO KWA BURE. KITU AMBACHO SI CHA KWELI.

 Wakuu wa shule za sekondari za Mashujaa na Mazoezi Matogoro wakileza jinsi wanafunzi wa kidato cha kwanza wanavyo ripoti kwa kusua sua hadi sasa.Mwenye kaunda suti nyeusi kushoto ni Bw.Leonard Matao wa Shule ya sekondari Mashujaa na wa kulia mwenye shati nyekundu ni Mkuu wa shule Mazoezi Matogoro Bw. Marianusi A. Komba.
 Bw.Marianus A,Komba
Bw.Leonard Matao

 

BAADHI ya wakuu wa shule za sekondari katika Manispaa ya Songea wamekanusha  kuwepo kwa utitili wa michango katika shule zao za sekondari.wamesema kuwa michango ambayo inachangishwa ni michango ambayo inasaidia kuendesha shule.
Wamesema kuwa Serikali haipeleki fedha ambazo zingilipwa kwa kila mtoto kusaidia wazazi na walezi kama walivyopanga,hivyo kamati ya shule na wazazi na walezi wanakubaliana kuchangisha fedha ili kuziba mapengo ambayo serikali ilipaswa kuchangia kwa kila mtoto kama ilivyo ahidi.
Kuhusu watoto kutoripoti shule wale waliyochaguliwa kuingia kidato cha kwanza , Mkuu wa shule  ya sekondari Mazoezi Matogoro Bw.Marianus A. Komba na Mkuu wa shule Mashujaa Bw.Leonard Matao wanasema ni kweli kwamba bado kuripoti kwa wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza hakuridhishi.
Hivyo wakuu hao wanaungana na tamko la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwa wazazi na walezi kuwapeleke watoto wao shule kabla ya tarehe 01/03/2013 aliyo sema mkuu wa mkoa huyo,