Sunday, February 17, 2013

WALIOKOSA KUPAKWA MAJIVU JUMATANO YA MAJIVU KUPAKWA LEO

Padre Mtalemwa pia Lecturer of History akipaka majivu waumini ambao siku ya Jumatano ya majivu hawakuwahi kupakwa.Padre anasema 'Tubuni na Kuiamini Injili" Ina maana kuwa binadamu ni mavumbi,na mavumbini atarudi
Kwaresma ni kipindi cha mfungo na majuto ya kumrudia Mungu kuomba toba kwa yale matendo ambayo hayampendezi Mungu.Kutokana na udanganyifu wa shetani,kwa kuwa katika siku 40 Bwana wetu Yesu Kristo alijalibiwa na ibilisi mara tatu na kumshinda.na hata haivyo aliondoka na kumwacha kwa muda.
Ibilisi hachoki katika majaribu yake ili ahakikishe anakuingiza kwenye dhambi,ndipo anapo furahi,kwa hiyo binadamu anajaribiwa na ibilisi kila siku hadi anapoingia kaburini.

No comments:

Post a Comment