Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake leo.
Mkuu wa Wilaya Songea Bw.Joseph Joseph Mkirikiti
Afisa Elimu Mkoa ( REO ) Ruvuma.
Baadhi ya waandishi wa habari.wakimsikiliza mkuu wa mkoa.
MKUU
wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu ametoa siku kumi na nne kwa wazazi
na walezi ambo hawaja wapeleka shule za sekondari watoto wao ambao
wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka huu.
Mkuu
huyo wa mkoa amesema hayo katika ofisi yake leo alipokuwa akiongea na waandishi
wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu tatizo hilo la watoto wengi ambao wamechaguliwa
kuingia kidato cha kwanza mkoani humo lakini hadi tarehe 14/2/2013 hawaja
pelekwa shule.
Ameagiza
wakuu wa wilaya,wakurugenzi,mkatibu tarafa ,na watendaji wa vijiji na mitaa ambao wanaishi wa wazazi
na walezi wa watoto hao kuwahimiza kuwapeleke shule kabla ya tarehe 01/03/2013
kwa hiyari yao, na kwamba baada ya tarehe hiyo kupita wazazi na walezi
watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha
Bw.Mwambungu amesema tatizo hapa sio ada bali ni miundombinu ya wazazi na
walezi wa watoto hao kuwa mibaya.Kwa kuwa ada ya shule ni shilingi 20,000 kwa mwaka,muhula wa
kwanza shilingi 10,000 na muhula wa pili shilingi elfu kumi.
Aidha
alisema kuwa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mkoani
humo mwaka huu ni 16,578 lakini walioripoti ni 9,388 tu, na wanafunzi 7,190
hawajaripoti katika shule za sekondari walizopangiwa.
No comments:
Post a Comment