Thursday, February 14, 2013

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AKERWA NA WATU WAZIMA WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu.akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake leo.


Afisa Eilimu Mkoa wa Ruvuma


MKUU wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu ametoa siku kumi na nne kwa wazazi na walezi ambo hawaja wapeleka shule za sekondari watoto wao ambao wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka huu.
Pia kuwatahadharisha watu wanaofanya mapenzi na wanafunzi ambao ni watoto wadogo,amesema watu wazima kufanya mapenzi na watoto ni dhambi pia ni kosa la jinai,matokeo yake wanawapa  mimba na kuwakana kwamba hawahusiki.  Atakaebainika atachukuliwa hatua.
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo katika ofisi yake leo alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu tatizo hilo la watoto wengi ambao wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mkoani humo lakini hadi tarehe 14/2/2013 hawaja pelekwa shule.
Ameagiza wakuu wa wilaya,wakurugenzi,mkatibu tarafa ,na watendaji  wa vijiji na mitaa ambao wanaishi wa wazazi na walezi wa watoto hao kuwahimiza kuwapeleke shule kabla ya tarehe 01/03/2013 kwa hiyari yao, na kwamba baada ya tarehe hiyo kupita wazazi na walezi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha Bw.Mwambungu amesema tatizo hapa sio ada bali ni miundombinu ya wazazi na walezi wa watoto hao kuwa mibaya.Kwa kuwa ada ya  shule ni shilingi 20,000 kwa mwaka,muhula wa kwanza shilingi 10,000 na muhula wa pili shilingi elfu kumi.
Aidha alisema kuwa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mkoani humo mwaka huu ni 16,578 lakini walioripoti ni 9,388 tu, na wanafunzi 7,190 hawajaripoti katika shule za sekondari walizopangiwa.
Pia amesema kuwa waandishi wa habari wananchi na viongozi wa ngazi zote mkoani watoe taarifa za haraka kwa uongozi wa wilaya na mkoa kwa watu wazima wanaojihusisha kufanya mapenzi na wanafunzi ambao ni watoto wadogo,na kuwasababishia mimba.
Amesema tatizo la mimba kwa wanafunzi ni kubwa mmno kwa sababu ya kulindana na wale wanaowapa mimba wanafunzi.

No comments:

Post a Comment