Kero ya wafugaji kulisha mashamba ya wakulima hazijaanza leo au jana,bali ni kero ya muda mrefu imekuwa kilio cha samaki mchozi kwenda na maji, Serikali imeshindwa kuwadhibiti wafugaji hao kwa nguvu ya fedha huwenda.
Mkulima Mmoja Bw.Amadi Njole anasema wafugaji hao hulisha kwenye mashamba ya watu,huchoma nyumba za wakulima,huchukua mbegu za wakulima hao,na wakiuliza basi wanashambuliwa kwa fimbo,mishale na sime zao.
Je hali hiyo itaendelea mpaka lini,je serikali imeshindwa kutenga maeneo ya wakulima peke yao na wafugaji peke yao ? Kila miaka ni kero wa wafugaji na wakulima katika wilaya ya kilosa,mali na uhai wa watu unapotea.
Wote wana umuhimu katika Taifa hili sasa kwanini hali inazidi kuwa mbaya kila mwaka na uongozi wa mkoa ,wilaya na vitongoji upo kwa nini unafumbia macho kero hizo ?
No comments:
Post a Comment