Hayati Padre Evaristus Mushi,jana kafikia mikononi mwa Ibilisi wakati akienda kusoma misa ya Ibada takatifu huko Unguja,Tukioa la kwanza ni kuchoma makanisa hakuna aliyeshtuka,lakini hatukusikia misikiti imechomwa moto,la pili Padre kavamiwa na kujeruhiwa hili nalo halikuchukuliwa mkazo,utadhani ni paka alikoswakoswa kuuawa,sasa funga kazi ni lajana la kumpiga risasi na kumuua padre wa watu.
Wakati Kamanda PC Mussa Ali Mussa wa Zanzibar anadai watu kadhaa wamekamatwa kwa mauaji hayo,ila hajui ni akina nani wanahusika na wimbi la mauaji na vurugu katika Kisiwa hicho,wala wa kuwatuhumu hawa jui na wala hawezi kusema ni sababu ya kisiasa au kudini, Hapo suala la kisiasa halipo kwa asilimia kubwa taka usitake,lakini yote kwa Mungu.
Ja Serikali ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar imetamka nini kuhusu hilo? , unadhani ni jambo la kawaida hilo ? ,je Kuna siri gani imejificha katika Fasihi hii ?. Kumbe tukiona mbwa amekenua meno tusidhani kuwa amefurahi, anaweza akatung'ata ?.kumbe ni kweli wakati wa biashara ya watumwa uhai wa mtu ulikuwa mikononi mwa mtu mwingine mwenye uwezo na siyo Mungu aliyetuumba?.E Mungu uwasamehe watu hao hawajui walilolitenda kwa Marehemu Mushi,na ilaze roho yake mahali pema peponi Amina.
SUALA
la mauaji wa viongozi wa Dini ya madhehebu ya Kikristo yanaendelea, na
hakuna hata siku imetokea wauaji wamekamatwa, ila Serikali inasisitiza tu kuwa walaifu wasakwe na wakamatwe mara moja basi
muda utapita hakuna kinacho endelea.
Swali linakuja,hivyo tangu mauaji hayo
yametokea ni lini umesikia kiongozi wa Madhehebu ya Kiislamu kauawa au
amepigwa? Au ni lini umesikia misikiti imechomwa moto zaidi ya Makanisa ? Kama
msomaji, hujapata kusikia vipi hili limetokea na linazidi kutokea serikali halilioni
hilo, utadhani wanaofanyiwa hivyo ni wanyama wasiyo na thamani ya kuishi katika
nchi hii ambayo inaitwa kisiwa cha
Amani,amani imetoweka,ni kazi kweli kuirudisha kwa mtindo huu unaoendelea
Hivyo Tanzania wanaotakiwa kuishi kwa
amani ni waislamu peke yao ? .Ingawa wauaji hao
sina uhakika kuwa ni wa kutoka dhehebu gani ,lakini yamkini ni kutoka katika Dhehebu
hilo.
Tunaianzisha Tanzania ya matabaka ya
udini ambayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyapiga vita vikali.Tunahangaika
na kitu gani,kila mtu anaimani yake ambayo anafikiri akiifuata hiyo itampeleka
peponi,isitoshe wote tuna mwabudu Mungu mmoja ingawa kila taifa lina jina lake wanalomwita
Mungu wao.
Mitume wote waliyo tumwa na Mungu kuja kuwakomboa wanadamu
kutoka dhambini binadamu wa karne hii tunawaumini tu, wala hatuwahi kuonana nao
wala siyo kutoka katika makabila yetu bali ni imani tu ya kuwaamini,lakini sisi
kwa sisi ambao wote hawaja kutana nao uso kwa uso tunauana, niushabiki usiyo na
maana wala busara,kwani hakuna mwenye haki ya kucheza na uhai wa mwenzake, kazi
hiyo tumwachie Mungu.
Hivyo basi serikali yetu sikivu iliangalie kwa macho ya
karibu matukio hayo, watu wa madhehebu ya kikristo wanaishi kwa mashaka, kwani
nchi hii inatawaliwa na serikali ya kidini?,kama serikali inaweza kutenga
maeneo ya wakulima na wafugani ,kwanini sasa wasitenge maeneo ya madhehebu Fulani
peke yao ili wasichanganyike nao kuwe na
amani katika kuabudu kwao.Haipendezi inasikitisha sana tunachoka kusikia historia
hiyo hiyo kila wakati. ( Padre Evaistitus
Mushi ) maskini alikuwa akienda kuendesha ibada, matokeo yake kafikia
mikononi kwa Ibilisi. Poleni Familia ya Padre Mushi.
No comments:
Post a Comment