Sunday, February 24, 2013

Majimaji 3 polisi Iringa 2 katika uwanja wa majimaji

 Hicho ndicho kikosi cha timu ya Wana- Lizombe Majimaji ya mkoani Ruvuma iliyoilaza Polisi ya Iringa 3-2 katika uwanja wao wa nyumbani wa majimaji.
 Mgeni rasmi katika mechi hiyo Injinia Steven Shauri akisalimiana na wachezaji wa timu ya majimaji wakati wa kukagua timu.
 Hicho ndicho kikosi cha wanausalama Polisi Kutoka Iringa ambao kabla ya mchezo wa leo walikuwa wa pili kutoka City Mbeya ambayo ilikuwa ikishikilia nafasi ya kwanza katika michozo ya Ligi daraja la pili.Ambapo majimaji walikuwa watatu katika msimamo wa ligi,Lakini baada ya kushinda leo Majimaji ipo katika nafasi nzuri.
Injinia Steven Shauri akisalimiana na wachezaji wa timu ya Polisi Iringa katika uwanja wa majimaji leo ambapo wameshindwa kutamba mbele ya wana lizombe hao wa Majimaji. walipochabangwa bao 3 kwa 2.



TIMU ya soka  ya Majimaji imefunga timu ya Polisi Iringa magoli 3 kwa  2 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa majimaji mjini Songea leo katika ligi ya daraja la pili.

Mchezo ulikuwa wa vuta ni kuvute katika dakika ya 14 Polisi Iringa ilianza kuliona lango la Majimaji kupitia mchezaji wake Demoso Mbalika jezi namba 11 mgongoni,Lakini katika dakika ya 19 majimaji ilisahwadhisha goli hilo kupitia mchezaji wake Sixmundi Mwasikaga namba 15.

Mambo yalikuwa hivyo ambapo katika dakika ya Tito Sanga  namba  2  aliipatia timu ya Polisi Iringa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 22 , katika patashika hiyo naye mchezaji wa majimaji Edward Philipo Songo  jezi namba 10 alilisawadhisha bao hilo katika dakika ya 24. Hadi kipenga kupigwa katika kipindi cha kwanza ilikuwa Majimaji 2 na Polisi Iringa 2.

Katika kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanjani kwa nia ya kupata ushindi ukizingatia Polisi Iringa Ilikuwa ya pili katika msimamo wa Ligi ya daraja la kwanza nyuma ya Mbeya City inayo ongoza Ligi hiyo ambapo majimaji walishika nafasi yatatu, kabla ya kushinda mechi ya leo.

Katika dakika ya 59 kipindi cha pili majimaji ilipata bao la tatu kupitia  mchezaji wake Edward Songo,goli ambalo lililoipaia majimaji ushindi wa magoli 3 – 2 hadi kipenga cha mwisho. Wakati Pilisi Iringa ilipata kadi 1 na Majimaji kadi 3.

Kutokana na matokeo hayo yamezidi kuiweka majimaji katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.Maji maji itakuwa na kibarua kingine na timu ya Mkamba kutoka Kilombero tahere 2/3/2013, tarehe 9/3/2013 na JKT Mlale na tarehe 13/3/2013 na Mbeya City.

No comments:

Post a Comment