Monday, December 19, 2011

NAWATAKIA CHRISTMAS NJEMA NA HERI YA MWAKA MPYA WA 2012

Nawatakia kristmas njema na heri ya mwaka mpya wa 2012 waomaji wa Blogg hi na Blogg nyingine ,kwa kumshukuru Mungu kutuweka hai mwaka 2011 uliyopita na muda kidogo,tutasherekea sikuu ya Kristmas na mwaka mpya wa 2012.hatuna budi kumshukuru,maana kwake chochote kinaweza kumtokea mtu katika maisha yake.

BREAKING NEWS Z Z Z ! ! ! MGOMO WA WAFANYAKAZI WA POSTA NCHINI KENYA UMEINGIA SIKU YA TATU LEO

Mgomo huo unafuatia madai ya  nyongea ya asilimia 30 ya mishahara yao kutoka asilimia 5 walizoongezwa.Wafanya kazi hao wanadai hawawezi kufanya kazi hadi madai yao yatekelezwe,ambapo Serikali imetishia kuwasimamisha kazi viongozi wao iwapo hawatabadilisha msimamo wao.

Sunday, December 18, 2011

TUKIWA KATIKA MITAA YA HALMASHAURI YA MJI WA LINDI JIONI BAADA YA KUTOKA UFUKWENI BARABARA ZAKE ZILIVYO KATIKA MIAKA 50 YA UHURU

 Barabara itokayo Bandarini katika mji wa Lindi
 nikiwa katika barabara ya miji wa Lindi ingawa muda huo magari hayakuwa mengi kama tulivyo weza kuyaona magari mida ya jioni kwenye fukwe kupunga upepo
Huyo Mhariri msaidizi wa Tujifunze Bwana Juma Nyumayo akielekea Bandarini katika mji wa Lindi mida ya jioni ,ila mji una barabara nzuri magari si mengi sana mida ya jioni kwenye Bandari yao iliyokufa.

MKUU WA MKOA WA LINDI MHESHIMIWA LUDOVICKI MWANANZILA AYASHUTIA MALORI YANAYOSOMBA JASI ( MAWE YA CHOKAA ) WILAYANI KIWLA BILA KULIPIA MAPATO HALM,ASHAURI

 Lori lililokutwa na mpigapicha wa blog hii wilayani kilwa kijiji cha Manadawa taika mkoa wa Lindi likiwa na shehene ya mawe ya chokaa yakipeleka katika kiwanda cha saruji,Wazo Hill kama malighafi katika kiwanda hicho.
 Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila, katika siku tofauti katika ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Kilwa, aliwaambia wananchi na uongozi wa wilaya hiyo kuwa macho na maliasili walizo nazo,na kwamba kama mali hizo zinachukuliwa basi zichukuliwe kihalali,Ha;mashauri ipate mapato yake kutokana na mali iliyopo katika halmashauri.
Alisema malori kwa malori yanachukua mawe ya chokaa bila  ya kulipia mapato katika halmashuri alisema tani moja ya mawe hayo ni Tshs.80,000/= na kwa siku ni tani ngapi zinachukuliwa,ni kiasi gani cha pesa halmashauri kinapoteza,aliwahimiza kuwa halmashauri iwatoze ushuru wa kuchukua malighafi hizo.

Thursday, December 15, 2011

MFUMO WA MAJITAKA KATIKA SOKO NA MITAA YA MANISPAA YA SONGEA BADO KITENDAWILI BWANA HUYO ANAJITAHIDI KURUKA VINYESI

Hayo ni maji machafu kutoka vyooni yalitanda katika mtaa wa Verlis katikati ya mji wa Songea,harufu kali ilwafanya wafanya biashara ya maduka kuondoka kwa muda hadi fudi mzibua vyoo alipo fika katika moja ya mfuniko uliyokuwa ukitiririsha maji hayo.

Picha ya juu kamera yetu ilipata huyo bwana akijitahidi kuruka maji hayo machafu au kinyesi kilicho pita katika ya maduka na wauza nguo nje,mafundi vyerehani,siku ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru Kiblang'oma wao wakipata manukato ya maji machafu hayo kutoka kwenye vyoo vya watu.

RUVUMA IMETANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2011 NA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA KWA AWAMU YA KWANZA WANAFUNZI 16,818 NA WANAFUNZI 163 WAMEFUTIWA MATOKEO KWA UDANGANYIFU

 Kaimu RAS Dokta Enselm Tarimo akielezea hatuazitakazochukuliwa ili kupandisha kiwango cha ufaulu.
Baadhi ya waandishi wa habari ofisini kwa RAS mjini Songea jana wakimsikiliza anavyo pambanua mikakati hiyo ya kuinua ufaulu mwaka ujao.
Waandishi wa habari wa TBC na Blogger wakimrekodi Afisaelimu mkoa Bibi Paulina Mkonongo jana baada ya kutangaza matokeo ya darasa la saba kuingia kidato cha kwanza mwakani

Kaimu Ras Dkt Tarimo aelezea mikakati
Kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Dokta Anselm Tarimo jana alitangaza matoke ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingingi na uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2012 mkoani Ruvuma.na kwamba wanafunzi 163 wamefutiwa matokeo yao kwa ajili ya udanganyifu.
Dkt Tarimo alisema walimu wakuu wa shule za msingi 7 ambazo zimebainika wanafunzi wao wamefanya udanganyifu watapata adhabu ya kuvuliwa madaraka iwapo itathibitishwa.
Alisema nawasimamizi wa mitihani nao wakikutwa na hatia wataondolewa dhamana ya kuwasimamia mitihani tena kwakuwa wamekiuka viapo vyao walivyoapa vya utunzaji wa siri.
Dkt Tarimo alisema kutokana na matokeo mabaya mwaka huu,amegiza halmashauri za wilaya kufanya tathimini ya matokeo hayo kabla ya Desemba mwaka huu, na Juma la kwanza la mwezi januari mwaka 2012 kila halmashauri iwakilishe kwenye kikao cha mkoa cha kutathimini maendeleo ya elimu.
Aidha alisema kuwa mikakati ya itakayochukuliwa na uongozi wa mkoa mwaka ujao ni pamoja na kutoa chakula kwenye shule za msingi na sekondari,kwa kuwa hakuna sababu ya kuacha kuwapa wanafunzi chakula shuleni wakati mkoa huu unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.
Kuhusu kuinua kiuwango cha ufaulu Dkt tarimo amewaagiza maafisa elimu wilaya wote kuandaa mpango wao wa kazi,ambao watabandika kwenye ofisi zao,kwa Mkurugenzi wake na kwa mkuu wa wilya hiyo,na nakala ipwelekwe Mkoani.
Naye Afisaelimu wa Mkoa huo Bibi baulina Mkonongo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kila halmashuri itaweka utaratibu wa ufuatiliaji wa ufundishaji,ukaguzi wa ndani,kwa maelekezo ya wakaguzi wa shule.
Alisema walimu wakuu wa shule watafuatili kwa karibu mahudhurio ya wanafunzi,walimu ili kuthibiti utoro kwa wanafunzi  na walimu.
Wanafunzi 123 wakiwemo wavulana 67 na wasichana 56 wanasubiri shule mbili za sekondari ambazo bado kusajiriwa.

Wednesday, December 14, 2011

MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2011 NA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA MKOANI RUVUMA YATANGAZWA

 Kaimu RAS wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Anselim Tarimo waktangaza matokeo ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwaka 2012.
 Afisaelimu Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo anaelezea hatua zitakazochukuliwa za kuinua kiwango cha ufaulu ,kama ilivyo fanya vizuri Manispaa ya Songea.
a
 Baadhi ya waandishi wa habari Mkoani Ruvuma wakifuatilia matangazo hayo ofisini kwa kaimu Ras huyo  Hapa songea Jioni hii leo.
Mmoja wa waandishi wa habari wakitafakari jinsi mkoa ulivyo fanya vibaya katika mtihani huo,wakati mkoa una chakula cha kutosha,nini tatizo.


Kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Dokta Anselim Tarimo leo ametangaza matoke ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingingi na uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2012 mkoani Ruvuma.

Dkt Tarimo ametangaza matokeo hayo kwa kusema kuwa si mazuri sana na yanasikitisha,alisema wanafunzi waliyo faulu mtihani ni 16,941 mkiwemo wavulana 8,335 na wavulana 8,606 sawa na asilimia 46.1 ya watahiniwa 36,718 waliyofanya mtihani mkoani na GPA ya 3.49,ambapo wasichana wamafanya vizuri zaidi ya wavulana.

Matokeo hayo ya kimkoa ni wastani wa matokeo ya kiwilaya,ambayo yanaonyesha Halmashauri za Mbinga,Namtumbo na Tunduru zimeshuka kiufaulu ikilinganishwa na  mwaka 2010.

Alitaja ufaulu huo kuwa Mbinga ni asilimia 40.2 ( GPA 3.32 )  ni chini kwa asilimia 0.82,Namtumbo asilimia 50 ( GPA 3.44 ) na Tunduru asilimia 41.2 ( GPA 3.56 ).

Songea Manispaa ufaulu ni asilimia 67.2 ( GPA 3.21 ) ni ongezeko la asilimia 2.46 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2010 kwa asilimia 64.54.

Wanafunzi wote 16,941 waliofaulu  wakiwemo wavulana 8,335 na wasichana 8,606 wamepata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza  mwaka 2012. kwa asilimia 99.2

Wanafunzi 34 wamepangiwa shule za wanafunzi waliyofaulu vizuri zaidi wavulana 18 na wasichana 16,wanafunzi 38 wamepangwa shule za ufundi wavulana 35 na wasichana watatu ( 3 ) na wanafunzi 56 wavulana 30 na wasichana 26 wamapangwa shule za bweni za kawaida,ambapo wanafunzi 16,813 wamepangiwa shule za kutwa katika halmashauri zao.

Aidha wanafunzi 24 wavulana 15 na wasichana 9 wenye ulemavu wamepangwa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kati yao 2 waioona wavulana na bubu viziwi 22 wavulana 13 na wasichana 9.

Sunday, December 11, 2011

MIAKA 50 YA UHURU WANANCHI WA MIKOA YA KUSINI WANAISHUKURU SANA SERIKALI ZA AWAMU ZOTE KWA MABADILIKO MAKUBWA YA MIUNDOMBINU

Miaka 50 ya Uhuru kusini barabara kwa kiwango cha lami,hii nia barabara kutoka Nanyumbu Mtwara kwenda Masasi Mtwara.
 Hiki ni kipande cha barabara ya lami katika wilaya ya Namtumbo kuelekea Tunduru Mkoani Ruvuma.

 Barabara kutoka Lindi kuelekea Dar es salaam,kabla ya kufika Nangulukuku wilayani Kilwa
Mnazi mmoja pacha   ya Mtwara na Lindi ,hapo ni kuelekea Lindi,Dar es salaam,zamani baada ya uhuru barabara kama hizo ilikuwa ndoto,watu walisafiri kwa meli au ndege kwa wenye pesa,miaka 50 ya uhuru,saa 12 Tunduru na saa 9 jioni upo Dar es salaam.,
lazima tukiri kwa mambo mazuri,yaliyotendeka ndani ya miaka hii,kwa vyovyote mabaya yapo,tuyarekebishe sote kwa pamoja,"kuna mambo mazuri,myachukue,na yale mabaya myaache' alisema Mwalimu Nyerere.

TUTOKAKO, TULIKO NA TWENDAKO MIAKA 50 YA UHURU MKOANI RUVUMA SHEREHE ZILIFANYIKA KIBLANG'OMA LIZABONI SONGEA LAKINI ZILIFUATIA KWA MAANDAMANO

 Maandamano ya watumishi wa sekta mbalimbali katika Manispaa ya Songea ,kupinga ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia.
 Maandamano ya watumishi na wanafunzi wa shule za sekondari zilizoko katika Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma kupinga ukatili.
Tunapo sherehekea miaka 50 wa Uhuru wa Tanzania Bara, nchi yetu bado unyanyasaji wa kijinsia bado upo na unazidi kuwepo,kwa hiyo maandamano hayo yalikuwa ni kupinga ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia,yaliyofanyika katika Manispaa ya Songea.

Wednesday, December 7, 2011

NAMSHUKURU MUNGU,MAJIRANI NA ZIMAMOTO DODOMA KWA KUOKOA MAISHA YA MKE WANGU NA WATOTO WANGU,KUTOKANA NA AJALI YA MOTO ULIYOTOKEA KATIKA NYUMBA HIYO WIKI LIYOPITA

 kama Mungu hajampangia mtu kifo,hata vitendo vya kishetani vya mauaji vikifanywa na watu au mtu haviwezi kufanikiwa.Ndivyo Mungu alivyoonyesha miujiza yake usiku wa saa 2.baada ya mama huyo,Mrs Sikapundwa alivyo taka kupata kifo kibaya cha kuungulia ndani ya nyumba,namshukuru sana Mungu,majirani kikosi cha Zimamoto cha Manispaa ya Dodoma kwa jitihada zao za kuvunja dirisha na kumwokoa mama huyo.
 Isitoshe Mke wa mwanagu mkubwa Bibi Coleta Epimak Sikapundwa naye alitaka kuwa katika kifo hicho cha kinyama,lakini Mungu alikataa,kilikuwa kilio kikubwa cha kutisha.E Mungu uabudiwe sana.
Watatu ni mtotoBinti wa darasa la saba Sarah Sikapundwa,kulia akiwa na Bibi yake Mrs Sikapundwa mwenye kitambaa cheupe kichwani.Leo nisngekuwa nao hao duniani,kwa ajili ya watu wenye uwezo wa kuwa na mamlaka ya maisha ya watu wengine zaidi ya Mungu ,lakini kaonyesha kuwa yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa mamlaka na uhaia wa mtu.