Friday, February 1, 2013

TUJIFUNZE KUSINI KWA MARA NYINGINE KUPATA UGENI KUTOKA MISA TANZANIA

 Bwana Andrew Marawiti kushoto akipata maelezo kutoka kwa Bw.Juma Nyumayo Mhariri msaidizi wa Mradi wa Magazeti Vijijini ( Rural Press Project Songea } hatua za awali ya maandalizi ya gazeti la kanda TUJIFUNZE .kuziandika habari ,kuzifanyia Editing ,Lay outing, Scaling,Picture cropping and designing to film kwa Computer.
 Mhariri mkuu wa gazeti hilo Bwana Christian Sikapundwa mwenye tai nyekundu akimwonyesha Bw. Marawiti Gazeti lililo andaliwa Page 1 na 12 ambalo linatoliwa film na kupelekwa kwenye hatua ya Plate ili hatua ya uchapaji ianze.
Hatua ya uchapaji Bw.Marawiti  mwenye kitabu anapata maelezo ya uchapaji wa rangi ( Headline}kutoka kwa fundi mchapaji Bw.Winifredy Kaimbe aliyeshika plate.
Bw. kaimbe aliyeshika plate akimwonyesha plate ya ukurasa wa 12 Master head ya rangi.


ANDREW Marawiti Kutoka  Media Institute of Southern Africa ( MISA ) akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma kutembelea vyombo vya habari vilivyoko Songea Mjini na Peramiho ,ametembelea Kituo cha Magazeti Vijijini TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Songea, Kuona jinsi wanavyo andaa gazeti lao,kuanzia hatua ya awalihadi kumalizia..
Bwana Marawiti ametembezwa sehemu zote muhimu katika kituo hicho na kupata maelezo na historia fupi ya Magazeti hayo ya kisomo ambayo Serikali iliyaanzisha kwa lengo la kusambaza vijijini kwa wanakisomo hasa watu wasiyo jua  kusoma,kuandika na kuhesabu kkk.
Kwa sasa Magazeti vijijini yanasomwa na wote kwa kuwa yana toa habari zenye viwango kama habari zinazoandikwa kwenye magazeti mengine yanayo tolewa kila siku kwa watu wa mjini peke yao.na vijijini hayawafikii walengwa wetu.
Gazeti hili linasambazwa Kanda ya Kusini katika mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi katika wilaya 19,kutokana ufinyu wa bajeti yetu tunachapisha nakala chache chache tunazo zisambaza kwa walengwa wote.Aidha kituo hakina waandishi wa habari wa kutosha na ufinyu wa bajeti inabidi kuwatumia waandishi wa habari wengine kukusanya habari.
Bw.Marawiti ametembelea Rural Press Project Songea TUJIFUNZE, Radio Jogo FM, Radio Maria na Peramoho Publishing House kunachapwa Gazeti la Mwenge na kuongea na baadhi ya waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment