Tuesday, December 31, 2013

HANDING OVER THE CERTIFICATE OF HAND OVER TO JUMA T, NYUMAYO





Handing over the certificate of hand over to Mr Juma T. Nyumayo as a new Editor of Southern Zone.Ruvuma,Lindi and Mtwara.

Friday, December 27, 2013

KILA CHENYE MWANZO HAKIKOSI KUWA NA MWISHO.HII NI SIKU AMBAYO ILIKUWA YA MWISHO WA UTUMISHI WANGU WA UMMA KANDA YA KUSINI







WATOTO WA SHULE YA AWALI CHARITY UWANJA WA SABASABA SONGEA WAMALIZA ELIMU YA AWALI

Mgeni Rasmi Bwana Bakule bakule maarufu kwa kuwa na timu yake ya miguu Matarawe Songea aliahidi kutoa mchango wake wa shilingi laki mbili.
Aidha alisema kuwa elimu ya Awali ni muhimu sana kwa kuinua taaluma hasa shule za English Medium,na kwamba alisema wakaze uzi wa kuendeleza watoto hao hadi darasa la saba
 Baadhi ya mwanafunzi wa Awali akimkabidhi shairi Mgeni Rasmi siku hiyo ya Awali
 Wanafunzi hao wakisoma shairi bila kubabaika utadhani darasa la saba kumbe ni watoto wa Awali

Baadhi ya wazazi wa watoto waliyo maliza elimu ya Awali siku hiyo

Thursday, December 26, 2013

Kifo cha mtoto Jems Steven wa mwaka mmoja na miezi miwili cha kinyama chashitua wakazi wa mtaa wa nanenane katika Manispaa ya Morogoro leo

Mtoto Jems Steven wa Mtaa wa Nanenane katika Manispaa ya Morogoro akutwa amekufa wakati mwili wake umefunikwa na takataka za mto Morogoro akiwa amekatwa sehemu zake za siri ,kidole na kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika paji la uso.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Bw. Isack Ilomo ,anaema mtoto huyo alipotea jana jioni wakati mama yake mzazi alipo mwacha akinywa uji wakati yeye alienda kuchota maji nje ya nyumba yao ya kupanga,
Alisema mama huyo baada ya kuona mwanae hayupo aliwauliza wapanagaji wenzake kama wamemwona mtoto wake ,nao walikataa kuwa hawaja mwona wala kumwona mtu aliyeingia chumbani mwake kwani ni muda mfupi tu alipo mwacha mtoto huyo.
Alipeleka taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya mtaa,Uongozi ulikwenda kwenye kituo kidogo cha polisi kuomba kibali cha hufanya upekuzi ili kubaini kama kuna mtu alimficha kwa malengo yaliyojitokeza. Polisi walikataa kutoa kibali wakidai mpaka baada ya masaa 24 ndipo kibali kitolewe.
Baada ya masaa hayo wananchi wameukuta mwili wa mtoto huyo pembeni ya kijito cha Morogoro akiwa amekufa.Kutokana na kifo hicho cha kusikitisha kimefanya wananchi wa mtaa huo kukilaumu kituo cha polisi kwa kukataa kutoa kibali kama wananchi wa mtaa huo walivyo omba,kwani walivyokuta  maiti hiyo ilikuwa bado ina joto,ni dalili kuwa kitendo hicho kilifanywa baada ya masaa hayo 24.Ambapo ni leo.
Ifike mahali sheria nyingne za Jeshi la Polisi zilegezwe ,maana raia hawezi kufanya upekuzi wa nyumba hadi nyumba bila ya search warrant.kama wangeruhusu wangeokoa maisha ya mtoto huyo.kwa vyovyote vitendo vilifanywa na majirani palepale hasa wapangaji wenzake.
Mwili wa Mtoto huyo umesafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwa wazazi wake mbele ya Biahawana Mkoani Dodoma Jioni hii leo kwa mazishi.Mungu ailaze roho ya Marehemu Jems Steven mahali peme peponi Amein.