Thursday, October 28, 2010

IKIWA ZIMEBAKI SIKU MBILI WATAZANIA WAINGIE KWENYE UCHAGUZI MKUU KIKWETE AJA NA CCM NI CHAMA KUBWA KUBWA LA MBEGU NDICHO KIME ZAA CHADEMA,NCCR,CUF,TLP NA VYAMA VYOTE VYA UPINZANI NI NINI KAMA CCM

 Zikiwa zimebakia siku mbili kuelekea  kwenye uchaguzi mkuu tarehe 31 /10/2010,mgombea Urais kupitia CCM Dkt Jakaya kikwete aseama CCM ni Chama Kubwa tena dume la mbegu iliyozaa,akina CHADEMA,NCCR,TLP CUF navingine ambavyo havijulikani sawasawa.( Source Christian Sikapundwa)
 Dar es salaam awambia tatizo la maji litakuwa ndoto kwao wakazi wa jiji hilo,kama Ilani ya CCM inavyoeleza.
Mikoa ya Lindi waambiwa kuwa ruzuku ya dawa za korosho itaongezwa,na kuimarisha soko la uhakika lenye tija kwa mkulima wa zao hilo.

Saturday, October 23, 2010

THE MAJI MAJI NATURAL HISTORICAL OF NGONI MUSEUM AT SONGEA MUNICIPALITY

HISTORICALLY the Ngoni people were situated as the Bantu speakers had settled in Southern Africa in groups such as Sotho –Tswana the Ngoni Shone and the Tsonga  Ngoni who became dominant and also the Xhosa were the one of the branch of Ngoni.

Due to the historical  background shows that the Ngoni people were escaped the ruling power  of Shaka Zulu,when the Mzilikazi in 1823 decided to run away Northwards to the  Shonaland and modern Zimbabwe. Because Shaka was an autocrat person.

 Shaka became a supreme autocrat controlling everything in Zululand. he made himself as spiritual and judicial leader, had no children for fear they would turn against him when they grew up, therefore he was a killer he slaughtered thousand of people when his mother died.

Politically the Ngoni people were organized into numerous but small hereditary chiefdoms, in average Ngoni chiefdom consisted of four to five villages with the chief called the Nkosi. But among the ngoni were chosen from the royal clan, the heir to the throne son was in principle the eldest son of the senior wife of the chief.

The ngoni chiefdoms were temporal and spiritual leaders, they were responsible for administration of the chiefdoms and for the dispensation of justice, they presided over social and religious ceremonies.

In other hand the chief did not enjoy his power, because the chief’s power were checked by his own privy council, is also his power was also often challenged by his brothers or even his sons therefore the chief had to attract and retain supporters in order to maintain their power.

Economically the ngoni people were subsistence economies which encompassed the cultivation of crops, animal husbandry ,crafts, mining ,metallurgy and barter trade which the structure and composition of these economies varied from community to community and were conditioned by environmental factors. such as distribution of water and rainfall, soil fertility and natural resource  endowment.

Finally we welcomed you to the Majimaji  National  Historical museum of Songea the place  Chiefs were buried  among of them were Nkonsi Gama, Songea Mbano,Chandamali,and also the Memorial of majimaji war of July 1905 to August 1907 which started at Nandele village Kilwa District Lindi Region.



When you face majimaji National museum Songea  Municipality
This is the attractive place of  majimaji National  Museum  of  Songea  Municipality,where you can enjoy  your self  by  observing  traditional historical things of the Ngoni people and the place were chiefs buried,Welcome Songea,Welcome Majimaji Museum. ( Photo by Christian Sikapundwa ) 

Thursday, October 21, 2010

MBIO ZA ELIMU YA SEKONDARI KWA KIDATO CHA KWANZA ZINAISHIA KIDATO CHA NNE UKIKIMBIA VIZURI UTASHINDA NA VIBAYA UTASHINDWA BWANA EMANUEL C.SIKAPUNDWA NI MIONGONI MWA WALIOANZA MBIO HIZO.

 Emanuel C.Sikapundwa  mwenye miwani ni mwanafunzi wa Msamala  Muslim Seminari Songea amehitimu elimu ya sekondari kidato cha nne (IV ) mwaka huu,baada ya kutunukiwa cheti cha kumaliza elimu hiyo,Dada na ndugu zake walimkabidhi zawadi mbalimbali kama ishara ya upendo na hungera kwa huhimili mikikimikiki ndini ya maisha ya shule kwa miaka yote akiwa shuleni.
Lakini kabla ya sherehe hizo kuanza huko shuleni kwao,Nyumbani  kwa Emanuel Ndani ya uwanja wa Sabasaba Matarawe Manispaa ya Songea wameonekana akina mama wakiamwandalia chakula yeye na wapambe wake,ndugu na jirani,Sherehe ni kula (.Source Christian Sikapundwa )  
Akina mama hao walianadaa wali mweupe na mwingine Pilau,unajua wasahili husema mchele ni mmoja lakini mapishi mbalimbali.watu wa pwani wana ujua zaidi mchele na aina mbalimbali za mapishi yake,mimi si mwanataaluma wa mapishi hayo.Na kwenye miti hakuna wajenzi,inamaana kule wanako ulima mpunga inawezekana  hakuna  mbwembwe nyingi za kuupika mchele huo.Je wewe wasemaje ? fuatilia ...............

Wednesday, October 20, 2010

VIJANA BAADA YA KUGUNDUA KUWA AJIRA IMEKUWA NI MAZUNGUMZO MAJUKWAANI KARIBU NCHI NYINGI DUNIANI,KUNA BAADHI YA VIJANA WAGUNDUA AJIRA YA CHAPCHAP HUKO NCHINI KENYE AJIRA GANI HIYO ENDELEA NA ‘FILER’ HAPO CHINI

BAADHI ya vijana nchini Kenya wamebuni ajira ya harakaharaka baada ya kuona ajira imekuwa wimbo wa majukwaani hasa kipindi cha chaguzi mbalimbali za uongozi duniani.

Kwa taarifa ya Wanyama Kibusire wa Kenya zinasema amekutana na vijana hao wakiwa katika ajira hiyo ambayo wanasema inawapa Dollar 7 za Kimarekani baada ya kumaliza kazi ambayo wamepangiwa na mwajiri wao,Siku hiyo hiyo.

Alisema vijana hao na wananchi wa Kenya wamoena njia rahisi ya kuemboleza msiba ndugu yao akifariki na kuajiri vijana kufika kuwalilia kuanzia chumba cha maiti,hadi nyumbani kwa mfiwa,walilia vijana hao wa ufundi mkubwa wakati wengine wakiomboleza kwa nyimbo za sala kama watakuwapo.

Ingawa baadhi ya madhehebu ya dini yamekipinga sana kitendo hicho,lakini vijana hao walisema ajira hakuna,kama kuna watu ambao hawana uwezo wa kuomboleza kwa kulia kwanini wao wasifanye kazi hiyo ambayo inawapa ujira.

Lakini kama kuna ajira ya kutengeneza masanduku ya kuzikia watu ambapo watu wenyewe hawajulikani watakufa lini  na kifo kipi na wapi wameruhusiwa kufanya hivyo sasa kwanini vjiana mabingwa wa kulia kwenye msiba wasiajiriwe?.Kazi ni kazi tusije tukadharau kazi za watu tutakuwa hatuwatendei haki.

Tuesday, October 19, 2010

WAKAZI WA MJI WA SONGEA HAWAPO NYUMA KWA KUJICHANA KWA VINYWAJI BARIDI,KUNA USEMI USEMA UKITAKA KUJUA NGUVU ZA MLEVI UMWAGE POMBE YAKE,SASA UKITAKA KUZIJUA NGUVU ZA MNYWA SODA UFANYE NINI?

Jumanne ya leo nilipo shuhudia Lori lililojazwa makasha matupu ya vinywaji baridi aina ya Coca Cola ,liloshambuliwa na wauzaji wa vinywaji hivyo katika mji wa Songea,karibu na baa za vinywaji vikali maarufu kwa jina la bia maeneo ya Standi ya mabasi yaendayo nje ya mkoa wa Ruvuma ,vijana wakitupia na makasha hayo kama mpira wa kikapu bila kuangusha.

Ilikuwa inafurahisha lakini wao ni ajira wala siyo mchezo,mwingine kajaribu kama hukupata kesi na mwenye kampuni ya soda au utozwe faini.Kazi ni kazi bwana usidharau kazi za watu ndizo zinazo wapa umaarufu.Hata hao wanao dai kuwa wakichaguliwa watatoa ajira,hazitakuwa tofauti sana na hizo.kwa hiyo tuheshimu ajira za watu.

Lakini kando kulikuweko na wateja wengine wakijiburudisha kwa soda,kutokana na jua kali liwakalo katika mji wa Songea lakini hautoki jasho,matokeo yake unazidi kuwa mweusi,lakini Dar,joto na jasho mtindo mmoja, mambo haya jamani yanafurahisha kweli.

DKT.NCHIMBI AENDELEA KUNADI SERA ZA CCM MISUFINI LEO KATIKA MANISPAA YA SONGEA,,KUWA TAREHE 31 MWEZI HUU SIKU CHACHE KUANZIA SASA WANANCHI WACHAGUE MAENDELEO, WACHAGUE VIONGOZI WATAKAO WALETEA MAENDELEO, NA KATIKA KATA YA MISUFINI WAMCHAGUE ELIZA NGONGI KUWA DIWANI WAO NA SIO MFA MAJI MAANA MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA.

 Dkta Emanuel Nchimbi anayetetea kiti chake cha ubunge jimbo la Songea Mjini kwa Tiketi ya CCM amemnadi mgombea uduwani wa kata ya Misufini Songea mjini Bibi Eliza Ngongi ambaye alikuwa naibu Meya wa Halmashuri ya Manispaa ya Songea,Nanatetea nafasi yake ya udiwani ambapo anagombea nafasi hiyo na mgombea kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mfamaji.Bibi Ngongi ni  msomi wa Shahada ya biashara amea ahidi mambo kadhaa.
 Ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya barabara,Soko la manzese,maji safi na salama,bishara ndogondogo kwa akona mama.(Source Christian Sikapundwa)
 Dkt Nchimbi Mbunge na Eliza Ngongi waliye inamiana wakitetajambo kabla ya kwenda kusalimia wananchi waliye kwenda kwenye kampeni ya ubunge na Udiwani leo Katika manispaa ya Songea kata ya misufini.
Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea anaye wania Udiwani katika kata ya Misufini akimsikiliza kwa makini Mhe.Dkt Emanueli Nchimbi hayupo kwenye picha.Wakati akimsifia mgombea wa udiwani katika kata hiyo Bw.Mfamaji kuwa ni mtu mpole,mwenye unyenyekevu,msikivu na mwenye kuelewa watu wanahitajinini kutoka kwake.

Alisema Bw.Mfamaji yeye anajua hawezi kushinda udiwani katika kata hiyo,hivyo uchaguzi ujao atahamia kata nyingine,sifa hiyo kwake imemjenge sifa ya kuhama hama kata baada ya kushindwa katika chaguzi za udiwani.Lakini majina mengine yanaweza kuashiria jambo kuwa zuri kwake au baya kwake.Sasa mfa maji jamani haachi kutapatapa.ndiyo maana uhama kata hii kwenda kata nyingine baada ya kushindwa.( Source Christian Sikapundwa)

Monday, October 18, 2010

MKULIMA BADO HANUFAIKI NA KILIMO CHAKE ANAYE NUFAIKA NI MAFANYA BIASHARA ANAYEFUATA MAZAO VIJIJINI KWA WAKULIMA

 Hiyo ni shehena ya mahindi inayosafirishwa nje ya mkoa wa Ruvuma yaliyo nunuliwa na wafanya biashara kwa bei ya hasara,ukilinganisha na gharama walizotumia katika kilimo.Je mkulima huyu atakuja fanikiwa siku moja?.Anauza kwa bei ya hasara siyo kwa kupenda,kutokana na matatizo yakiwemo ya usafiri kufikisha mazo yake kwenye soko.Shehena ambayo ilitaka kukuta nyaya za umeme wakati likipita  lori hilo leo mjini Songea. ( picha na Christian Sikapundwa)

 Ruvuma inavuma kwa mazao mbalimbali,ya chakula na biashara yakiwemo kahawa,tumbaku,na korosho,kwenye chakula ni mahindi ,mpunga lakini kuna magarage ambayo unayaona yamerundikana chini yakingojea wa laji,aliyeumia hapo ni mkulima anae uza kwa hasara kwa wafanya biashara,wangekuwa na soko la uhakika wangenufaika na wao.
Magunia unayoyaona ni mahindi na maharage katika soko la SODEKO katika manispaa ya Songea wanasubiri kwenda kuya uza katika ghala la serikali Ruhuwiko kwa bei ya sh.300/=  kwa kilo wakati wao kwa wakulima wameyenunua kwa sh.150 /= kwa kilo.Je nani mjanja kati ya mkulima na mfanya biashara ?. ( Picha na Christian Sikapundwa)

Friday, October 15, 2010

ANAYEBEZA RUZUKU YA PEMBEJEO ZA KILIMO,NINANI?,WAULIZE WAKULIMA WA MAHINDI RUVUMA AU ANGALIA MAHINDI YALIVYO LUNDIKANA KATIKA GHALA LA CHAKULA RUHUWIKO YAKISUBILIWA KUNUNULIWA.

 Haya ni mahindi ambayo bado hayajanunuliwa yako nje ya ghala la chakula la taifa Ruhuiko,na muda wa mvua uko jirani,je Serikali inawafikiria vipi wakulima wamkoa wa RUVUMA?
 Hayo ni mahindi yaliyo nunuliwa lakini yapo nje ya ghala kwa kukosa nafasi,kwenye maghala ya kuhifadhia chakula,yakiendelea kulundikana hapo na mengine mengi bado kununuliwa unafikiri kitatokea nini?.Na hapo chini ni foleni ya maliri yakisubiri kupakuliwa ili mahindi yao yauzwe,maana hata nafafi ya kuyaweka mahindi usiyonunuliwa haipo.Kuna haja ya kubishana na wanaosema Ruzuku ya pembejeo haifanyi kazi.kama una macho tazama usingije kuhadithiwa.

Thursday, October 14, 2010

MHARIRI WA MAGAZETI VIJIJINI KANDA YA KUSINI NA WAFANYA KAZI WOTE WANIOMBA ROHO YA BABA WA TAIFA MWALIMUJ.K.NYERERE IKAE MAHALI PEMA PEPONI.




Leo ni kumbukumbu ya miaka 11 tangu Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kututoka,kwa niaba ya Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,kutanamkumbuka Baba wa Taifa kwa kuanzisha kisomo chenye manufaa.kwa lengo la kupambana na maadui ujinga,maradhi na umasikini.

Mwaka 1965 Tanzania ilikuwa na madarasa 7,257 yakiwa na watu wazima 541,562 mkiwemo wanaume 206,214 na wanawake 335,345,pia kulikuwa na madarasa ya kujifuza kiingereza na hesabu 14,043,vikundi 1,914 vya wanawake 112,739 waliyojishughulisha na mapishi,ushonaji,ufumaji na utunzaji wa watoto.

Katika miaka ya mwanzoni baada ya Uhuru Baba ya taifa alianzisha Eilumu ya Watu Wazima,chini ya Wizara ya Elimu ya Taifa na kuunda idara ya Elimu ya Watu Wazima nakuteuliwa Mkurugenzi Masaidizi wa Elimu ya Watu Wazima Novemba 1969.

Pamoja na mambo mengine Mwalimu Nyerere aliyazungumzia sana masuala ya Umoja wa nchi za Kiafrika,uongozi bora,uchumi,rushwa,Jumuiya ya Afrika Mashariki na Vijana ambao ndiyo nguvukazi ya taifa.

Kituo cha Mradi wa Magazeti vijijini Kanda ya Kusini TUJIFUNZE na wafanya kazi wote wanamkumbuka Mwalimu Nyerere siku ya leo,wakiwemo ndani ya Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi na Mkurugenzi  wake Bwana Salum Mnjagila katika Serikali ya awamu ya nne ikiongozwa na Rais Jakaya Kiwete ambaye ameirudisha Kurugenzi hiyo.

Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima imekuwa kitengo kwa muda mrefu chini ya Afisa elimu kiongozi na kuwa na Mkurugenzi Msaidizi Bwana Salum Mnjagila.Kwa kumuenzi Baba wa taifa Tunamshumuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuyaendeleza yale mazuli aliyoyaanzisha Mwalimu Nyerere na Waziri wa Elimu Prf.Jumanne Maghembe,Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na nje ya Mfumo Rasmi Bw.Salum Mnjagila katika harakati za  kupambana katika kufuta ujinga nchini.

Aidha kwa niaba ya vituo  7 vya Kanda vya magezeti vijijini tunamombea Baba wa Taifa aendelee kuwa mwenye Heri na Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi.Kutokana na kampeni ya elimu ya watu wazima ndipo vituo hivi viliaanza.

Mwaka 1974 Januari toleo la kwanza la Gazeti la Kanda ELIMU HAINA MWISHO la kisomo lilitolewa,mwaka 1979 magazeti mawili ya kisomo ya Kanda ya TUJIELIMISHE Kanda ya Kaskazini na TUJIENDELEZE Kanda ya mashariki.

Mengine ni magazeti matatu ya kisomo ya TUJIFUNZE Kanda ya Kusini,NURU YETU Nyanda za Juu Kusini,na  ELIMU YETU Kanda ya Kati yalianzishwa Julai mwaka 1980.Dhamira ilikuwa kutoa elimu kwa kujali makundi yote yakiwamo ya watu wazima ambao walikuwa wengi hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu baada ya Uhuru.

Lakini leo nchini kuna zaidi ya asilimia 30 ya watu wazima hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu si ajabu kwa kuwa wengi waliodhani wamejua na wakasahau kama kuna kusoma vitabu wamerudia tena hali ya kutijua kusoma.

Tena vijana wengi walioacha shule kwa sababu tofauti zikiwemo za ufataki,wakuhonga pipi na chipsi watoto wa wenzao,wanawake wakubwa wanawakimbia wakiwaangalia walivyo jipangilia wanaona ghali na kukimbilia rahisi,kumbe ubahili wao ni hasara kwa taifa letu.kwa hiyo elimu ya watu wazima itaendelea,bado kuna wanaoingia kidato cha kwanza hawajui kusoma,hawa watakuwa wapi?.

Kila mtu anahitaji elimu ya watu wazima hata awe na shahada  kibao,hawezi kujua kila jambo,sasa siku akitaka kujua jambo ambalo halijui kwa mtu mwingine,basi hiyo ni elimu ya watu wazima.Hivyo ni kweli kwamba wasomi wote wanajua kuitumia Computer sawasawa ? au wasomi wote wanayajua masomo yote?,basi kama hapana,siku akitaka kujifunza chochote asicho kijua wakati akiwa shuleni  basi huyo atakuwa kwenye elimu ya watu wazima.

Tuesday, October 12, 2010

MKURUGENZI WA CHEMBELE APPLIED ZONE SONGEA NA LODGE YA KISASA IPO BOMBAMBILI

CHEMBELE APPLIED ZONE NI MABINGWA WA USAFIRISHAJI WA MIZIGO:-
  • Songea  Dar es salaam,Dar es salaam Shinyanga
  • Dar es salaam,Makambako hadi Songea

Kwa mahitaji yako ya kusafirisha mizigo Dar es salaam Tupo mtaa wa Swahili Kariakoo.
Songea tupo Soko kuu mkabala na Benki ya NBC,

Piani wauzaji wa pikipiki za aina ya :-
 Mkurugenzi wa Chembele Applied Zone Bwana Agaton Chembele.hiyo hapo chini ni lodge ya ke ya kisasa kabisa  eneo la Bombambili Songea karibu na kanisa la Roman Katoliki.karibuni sana  uliza kwa Chembele ummefika.
  • Mwada jet Fighter
  • Dawan katika maduka yetu ya :-
  • .Songea soko kuu Mkabala na NBC
  • Morogoro karibu na kituo cha daladala Masika.
  • Mbimga
  • Masasi Mtwara
  • Kahama na
  • Dar es salaam mtaa wa Swahili Kariakoo.

Monday, October 11, 2010

MAFIGA MATATU SI NENO GENI MASIKIONI KWA WENGI JE HAYO...

MAFIGA MATAU UNAYAJUA ? WAULIZE WAENDESHA KAMPENI

Wakati kampeni za Urais ,Ubunge Udiwani na Viti maalu zikiendela majimboni,utapata semi kemkem moja wapo ni  ya mafiga matatu,mafiga ni mawe,tofali au udongo uliyotengenezwa kwa shughuli mahususi za upishi kuinjika sufuria la wali au ugali,chungu cha mboga wali au ugali,lakini wataalamu wa lahaja za Kiswahili watakueleza vizuri.

Katika harakati za kuwini chochote lugha kadhaa zitaibuka ili ushindi upatikane,basi usemi huo ulidhirishwa pale Mgombea Urais Dk Jakaya Kikwete alipo onyeshwa hayo mafiga matatu na sufurika kubwa ikiwa juu yake kama unavyoiona kwenye picha hiyo hapo chini, kabla hajahutubia wananchi katika uwanja wa majimaji mjini Songea kunadi Sera za CCM hapo jana.

Ujumbe wa mafiga matatu kwa hapa katika jimbo la Songea mjini ! figa moja ni la Dk Kikwete,figa la pili ni la Dk Nchimbi na latatu ni Ngongi,hii ninamaana tarehe 31 mwaka huu. Watu wachague mafiga matatu  ya CCM.

Ni kwamba figa la kwanza wamchague Rais Kikwete,figa la pili wachague wabunge wao wa CCM na la tatu wachague Madiwani  wa CCM.Habari ndiyo hiyo.lakini mafiga hayo kwenye picha yametengenezwa na mchwa yapo katika urefu unaofanana na unene unaofanana.

USIJALI OFISI, JALI ENEO LA KUTOLEA HABARI ZA TUJIFUNZE KUSNI

Mambo haya bwana we acha tu Habari ni habari haijalishi zinatoka vijijini au mijini peke yake.

HABARI ni habari ila zimetofautiana pale wanazuoni walipo sema kuna habari zinaitwa Hard news na nyingine Story .hata kama  ziwe hard news au story zinatoka kwenye sources. Hata hivyo vijijini ndiko waliko wadau wengi wanaotakiwa kutoa habari na kupata habari,lakini idadi kubwa ya hawa hainufaiki na vyombo vya habari labda kwa sababu ya ugumu wa kuwafikia waliko au magazeti yakipelekwa hayanunuliwi,luninga na radio ni ngumu kwao ndio usiseme.

Kwa upande wa luninga wanaweza wakapata baadhi yao,tatizo ni nishati ya umeme kwao ni ndoto,radio hivyo hivyo maeneo mengine mawimbi ya baadhi ya radio hayafiki au hazisikiki vyema kama kwetu kusini hasa mwambao mwa ziwa nyasa wanasikia radio Malawi ama Mozambiki.Magazeti ndio usiseme kununua nakala moja ya shilingi 400/= ni hasara kubwa kwa baadhi ya kaya huku vijijini.

Lakini wote wanahitaji kuhabarishwa iwe kwa luninga,radio au magazeti.Na wanahaki ya kutoa haratizo sio za kuzisika za vibaka Dar. Wanaiba simu  wao siyo habari hiyo au bajaji umekanyaga bata hiyo siyo habari,habari kwo ni Juam kaiba mihogo,mpunga,bata wa kijiji kinacho fuata tatika kata yao.

Basi hilo ndilo kweli basi wenye vyombo wakipata habari za vijijini kama zimemfikia mhariri maezani kwake hata moja ionekane kwenye gazeti siyo lazima iwe front page hata ndani kwenye ukurasa wa  habari za mikoani,humbuka habari ni habari.
 Hii ni ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI ( ruralpresssongea.blogspot.com ) join with as please Hapo chini ni shule ya sekondari Mkuzo katika Manispaa ya Songea iliyojengwa na Dt.Emanuel Nchimbi anaegombea Jimbo la Songea Mjini.ni ya kidato cha tano na sita (Picha na Christian Sikapundwa )

Sunday, October 10, 2010

KAMPENI ZA URAIS ZA CCM, RUVUMA ZIMETIA FORA KWA PIKIPIKI KWA MBWEMBWE KIBAO UWANJA WA MAJIMAJI LEO

Rais Jakaya Kikwete kaendelea na kampeni za kuwania kuendelea Ikulu kwa kutoa ahadi kuwa ndani ya miaka mitano ijayo :-
  • Barabara ya Njombe Songea itafanyiwa ukarabati wa hali ya juu kwa kuwa barabara hiyo imeanza kuchoka.
  • Kujenga chuo cha waganga Mjini Songea mipango imesha andaliwa.
  • Kuunganisha barabara kwa kiwango cha lami Mtwara hadi Mbamba – Bay.
  • Kuboresha kilimo kwa kuongeza pembejeo.
  • Kuleta vitabu vya masomo ya Fizikia,Kemia na Biology katika shule za sekondari  nchini.
  • Kuboresha huduma za afya.

Alisema Iani ya CCM ya mwaka 2005 imetekelezwa kwa kiwango cha juu katika sekta zote,kwani CCM ni chama dume tena dume la mbegu.alisema Ukarabati mkubwa umefanyika katika hospitali ya Mkoa.mahindi ya wakulima yatanunuliwa fedha zipo,pia wameruhusiwa kuuza mahindi nje ya nchi ila waweke akiba, yote hayo  ni mchakato wa Ilani ya CCM  ilivyo utekelezwa katika miaka mitano ya uongozi wa Dk Jakaya Kikwete.

Alisema tatizo la marelia vyandalua vyenye dawa vipo kwa kina mama,hivyo waume zao watanufaika na vyandarua hivyo.Hata hivyo alisema tatizo la UKIMWI  bado ni kuwa kwani hakuna chandalua cha kuuzuia.Dawa ni kuacha  au kutumia kinga.Tanzania bila UKIMWI  inawezekana kama mtafuata maagizo ya viongozi wa Dini ,viongozi wa siasa na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

Aidha alimnadi mgombea ubunge  wa jimbo la Songea mjini Dk Emanueli Nchimbi,ambaye kama mbunge wa jimbo hilo,amejenga shule ya sekondari Mkuzo ya kidato cha tano na sita,ameezeka bati shule za manispaa ya songea,amejenga barabara tatu kwa kiwango cha lami na manispaa na ya nne ni kutoka Makambi hadi mjini.
 Dk.Jakaya Kikwete akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa majimaji leo wakati akianza kampeni za kugomgea Urais kupitia CCM mkoani Ruvuma.
 Dk Emanuel Nchimbi akielezea mafanikio ya ilani Ya CCM ya mwaka 2005 kwa mambo mengi ya maendeleo aliyoyafanya katika manispaa ya Songea zikiwemo barabara tatu za lami na ya nne inatarajiwa kumalizika hivi karibuni,kuboresha majengo ya shule za msingi na kujenga shule ya sekondari ya Mkuzo.ya kidato cha tano na sita.

Saturday, October 9, 2010

KUWAFANYA WATU WAWE WATULIVU NA USIKIVU WABURUDISHE

Koda ni ngoma kutoka wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma ni moja ya ngoma zinazo chezwa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.hiki ni kikundi kilicho tumbuiza watu siku ya uzinduzi wa jengo la Chama Cha walimu (CWT) Songea siku ya mwalimu duniani iliyofanyika Kitaifa mkoani humo.

BURUDANI NI MUHIMU KWA MAISHA YA KULA MMOJA ANAYEISHI






Mungu kampa kila mtu kipaji chake,lakini kunavipaji vingine ni adimu sana ni wachache tu ambao wamejeliwa kuwa nacho,jaribu kufuatilia wenye vipaji mbalimbali utaktua wametofautiana.
Watoto hawa watatu ni wasanii wa muziki wa kizazi
kipya hivyo kinachotakiwa kuwaendeleza au wao wakiendeleze kipaji hicho.mwenye vipaza sauti viwili ndiye,anayeongoza wenzake ni Alfa Jofrey wa kidato cha kwanza mateka sekondari Manispaa ya Songea wenzake wanasubili majibu ya Darasa la saba.walitumbiza wananchi siku ya uzinduzi wa kampeni ya Ubunge,udiwani na Viti maalumu katika viwanja vya shule ya msingi Majengo Songea Mjini.


WATANZANIA HATUKO NYUMA KWA NGOMA ZA ASILI ,FURAHI NA KIODA TOKA MBINGA


Kikundi hicho ni cha ngoma ya kioda kutoka  wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma  ngoma hiyo inachezwa kwa ustadi mkubwa .ilichezwa siku ya Mwalimu Duniani iliyofanyika kitaifa  Mkoani Ruvuma.

NDONDO SI CHULULU, KIMATA MATARAWE SONGEA

Mwalimu Antonia Raphael kainga mwenye kofia anayeonyesha .anaelezea jinsi ya kutengeneza sabuni,kwa Rais Jakaya Kikwete mwenye suti ya bluu na kofia alipotembelea banda hilo siku ya walimu Duniani kitaifa Ruvuma katika uwanja wa majimaji Songea  hivikaribuni.

Kikundi cha KIMATA cha akina mama walimu cha uzalishaji mali kilianza na mtaji wa shilingi 120,000 2007 kutengeneza sabuni za kufulia za mche ambazo ni .Lovela.Net work na mkaa.Antonia Raphael kapinga ni mweka hazina wa kikundi hichi anaye elezea kwa wagenie waliyo tembelea banda hilo kwa Rais Jakaya Kikwete .Mradi huo sasa unafaida ya shilingil 4,000,000 .fedha ambazo zinawasidia watoto yatima na wenye mahitaji maalumu kuwasomesha.

Friday, October 8, 2010

Hand craft make the group of woman to get money Tunduru

The group of women teachers at Tunduru District Ruvuma Region are trying to find money by involving in hand craft.Esha Chandu is the one how shows different things made by hard wood known as mpingo.this the swahili name.One of the interested thing was a thermos of tea,cups of the tea,plates and  animals such elephants anti lops  and other many item.

But she said that the market is not available.So they trying to look for market every were if possible through this Blog. Remember these are the group of women teacher situated in Ruvuma Region Tanzania for any contact please make it through blog.

Esha Chandu showing the thermos made by using Mpingo tree which is black in colour to the guest of honer President  Jakaya Kikwete during the ceremony of Teacher's day in majimaji stadium Songea Ruvuma Region this month.

Science must start from the grass root.

Sarah Joseph is standard five at Mathin Luther Dodoma Municipality, She always doing home work at their home,with computer.Although she in low class but she can do wonders with computer.
I was not believe that when she told me do give assignment on how to use mouse,keyboard, hard ware and soft ware.

Now it's better for the other schools to give their pupils the knowledge of using computer bigging from home then at school this will make their teacher to teach them easily.    

Thursday, October 7, 2010





Mkurugenzi wa Elimu ya watu wazima Nje ya Mfumo rasmii S.Mnjala






 

 MHESHIMIWA LIKOKOLA MWENYE SULUALI NA KILEMBA ANAWONYESHA WAGENI WANIOONGOZANA NA MKURUGENZI SALUM MNJAGILA ALIYEMFUTA BUSTANI YA MICHE YA MITI YA MATUNDA NA MITI YA MBAO KWA LENGO LA KUHIFADHI MAZINGIRA KATIKA KITUO HICHO.

BWANA SIMBILA AKIANGALIA BUSTANI YA MBOGA YA HEWANI KATIKA KITUO CHA VICOBA HOUSE SEED FARM ,LIKOKOLA ANASEMA BUSTANI HIYO HAINA HAJA YA KUTAFUTA ENEO LA KUTAYARISHA KINACHU TAKIWA NIKUAANDAA KASHA LA MBAO,KUWEKA UDONGO ,KUCHANGAYA MBOLEA YA SAMADI KISHA KUPANDA MICHA NA KUIMWAGILIA.

VICOBA HOUSE KUNA MIRADI YA KILA AINA INAYOENDESHWA NA VIKUNDI VYA MUKEJA NA VICOBA KATIKA MKOA WA RUVUMA NA BAADAYE TANZANIA NZIMA,NI VIKUNDI VYA UJASILIA MALI,KAMA SACCOS,BENKI ZA VIJIJINI BUSTANI,KUOTESHA UYOGA NA MENGINE.

JAKAYA KIKWETE AFURAISHA WALIMU

JENGO LA CWT MKOA WA RUVUMA KATI YA MAJENGO 21 TANZANIA BARA AMBALO LIMEZINDULIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE SIKU YA WALIMU DUNIANI ILIYOADHIMISHWA KITAIFA  SONGEA MKOANI RUVUMA OKTOBA 5 ,2010    MAANDAMANO YA WALIMU WOTE NCHINI, HAPA  WILAYA YA TUNDURU WAKIPITA MBELE YA MGENI RASMI, RAIS KIKWETE, KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI  MKOANI RUVUMA SIKU YA WALIMU DUNIANI


Sunday, October 3, 2010

Naingia kazini

Nawakaribisha kwenye blog yangu ya ruralpresssongea.blogspot.com kwa jina hilo hapo juu . TUJIFUNZE KUSINI jina hili linamaana sana kwa wadau wa maendeleo ulimwenguni. Daima kusini kumekuwa na matukio mengi na kuachwa nyuma kimaendeleo, ukianza na Bara la Afrika kusini mwa jangwa la sahara ni matatizo, Tanzania hali kadhalika. Kwa Blog hii nitaleta vitu vingi ambavyo ni changamoto ya kusaidia maendeleo na kuifahamu kusini na fursa za kimaendeleo kuliko watu wengi wanavyodhania asanteni karibuni sana.