Kaimu RAS wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Anselim Tarimo waktangaza matokeo ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwaka 2012.
Afisaelimu Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo anaelezea hatua zitakazochukuliwa za kuinua kiwango cha ufaulu ,kama ilivyo fanya vizuri Manispaa ya Songea.
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoani Ruvuma wakifuatilia matangazo hayo ofisini kwa kaimu Ras huyo Hapa songea Jioni hii leo.
Mmoja wa waandishi wa habari wakitafakari jinsi mkoa ulivyo fanya vibaya katika mtihani huo,wakati mkoa una chakula cha kutosha,nini tatizo.

Kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Dokta Anselim Tarimo leo
ametangaza matoke ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingingi na uchaguzi wa
wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2012 mkoani Ruvuma.
Dkt Tarimo ametangaza matokeo hayo kwa kusema kuwa si mazuri
sana na yanasikitisha,alisema wanafunzi waliyo faulu mtihani ni 16,941 mkiwemo
wavulana 8,335 na wavulana 8,606 sawa na asilimia 46.1 ya watahiniwa 36,718
waliyofanya mtihani mkoani na GPA ya 3.49,ambapo wasichana wamafanya vizuri
zaidi ya wavulana.
Matokeo hayo ya kimkoa ni wastani wa matokeo ya kiwilaya,ambayo
yanaonyesha Halmashauri za Mbinga,Namtumbo na Tunduru zimeshuka kiufaulu
ikilinganishwa na mwaka 2010.
Alitaja ufaulu huo kuwa Mbinga ni asilimia 40.2 ( GPA 3.32
) ni chini kwa asilimia 0.82,Namtumbo
asilimia 50 ( GPA 3.44 ) na Tunduru asilimia 41.2 ( GPA 3.56 ).
Songea Manispaa ufaulu ni asilimia 67.2 ( GPA 3.21 ) ni
ongezeko la asilimia 2.46 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2010 kwa asilimia
64.54.
Wanafunzi wote 16,941 waliofaulu wakiwemo wavulana 8,335 na wasichana 8,606
wamepata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza
mwaka 2012. kwa asilimia 99.2
Wanafunzi 34 wamepangiwa shule za wanafunzi waliyofaulu
vizuri zaidi wavulana 18 na wasichana 16,wanafunzi 38 wamepangwa shule za
ufundi wavulana 35 na wasichana watatu ( 3 ) na wanafunzi 56 wavulana 30 na
wasichana 26 wamapangwa shule za bweni za kawaida,ambapo wanafunzi 16,813
wamepangiwa shule za kutwa katika halmashauri zao.
Aidha wanafunzi 24 wavulana 15 na wasichana 9 wenye ulemavu
wamepangwa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kati yao 2 waioona wavulana na bubu viziwi 22
wavulana 13 na wasichana 9.
No comments:
Post a Comment