Thursday, December 15, 2011

RUVUMA IMETANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2011 NA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA KWA AWAMU YA KWANZA WANAFUNZI 16,818 NA WANAFUNZI 163 WAMEFUTIWA MATOKEO KWA UDANGANYIFU

 Kaimu RAS Dokta Enselm Tarimo akielezea hatuazitakazochukuliwa ili kupandisha kiwango cha ufaulu.
Baadhi ya waandishi wa habari ofisini kwa RAS mjini Songea jana wakimsikiliza anavyo pambanua mikakati hiyo ya kuinua ufaulu mwaka ujao.
Waandishi wa habari wa TBC na Blogger wakimrekodi Afisaelimu mkoa Bibi Paulina Mkonongo jana baada ya kutangaza matokeo ya darasa la saba kuingia kidato cha kwanza mwakani

Kaimu Ras Dkt Tarimo aelezea mikakati
Kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Dokta Anselm Tarimo jana alitangaza matoke ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingingi na uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2012 mkoani Ruvuma.na kwamba wanafunzi 163 wamefutiwa matokeo yao kwa ajili ya udanganyifu.
Dkt Tarimo alisema walimu wakuu wa shule za msingi 7 ambazo zimebainika wanafunzi wao wamefanya udanganyifu watapata adhabu ya kuvuliwa madaraka iwapo itathibitishwa.
Alisema nawasimamizi wa mitihani nao wakikutwa na hatia wataondolewa dhamana ya kuwasimamia mitihani tena kwakuwa wamekiuka viapo vyao walivyoapa vya utunzaji wa siri.
Dkt Tarimo alisema kutokana na matokeo mabaya mwaka huu,amegiza halmashauri za wilaya kufanya tathimini ya matokeo hayo kabla ya Desemba mwaka huu, na Juma la kwanza la mwezi januari mwaka 2012 kila halmashauri iwakilishe kwenye kikao cha mkoa cha kutathimini maendeleo ya elimu.
Aidha alisema kuwa mikakati ya itakayochukuliwa na uongozi wa mkoa mwaka ujao ni pamoja na kutoa chakula kwenye shule za msingi na sekondari,kwa kuwa hakuna sababu ya kuacha kuwapa wanafunzi chakula shuleni wakati mkoa huu unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.
Kuhusu kuinua kiuwango cha ufaulu Dkt tarimo amewaagiza maafisa elimu wilaya wote kuandaa mpango wao wa kazi,ambao watabandika kwenye ofisi zao,kwa Mkurugenzi wake na kwa mkuu wa wilya hiyo,na nakala ipwelekwe Mkoani.
Naye Afisaelimu wa Mkoa huo Bibi baulina Mkonongo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kila halmashuri itaweka utaratibu wa ufuatiliaji wa ufundishaji,ukaguzi wa ndani,kwa maelekezo ya wakaguzi wa shule.
Alisema walimu wakuu wa shule watafuatili kwa karibu mahudhurio ya wanafunzi,walimu ili kuthibiti utoro kwa wanafunzi  na walimu.
Wanafunzi 123 wakiwemo wavulana 67 na wasichana 56 wanasubiri shule mbili za sekondari ambazo bado kusajiriwa.

No comments:

Post a Comment