Wednesday, December 7, 2011

NAMSHUKURU MUNGU,MAJIRANI NA ZIMAMOTO DODOMA KWA KUOKOA MAISHA YA MKE WANGU NA WATOTO WANGU,KUTOKANA NA AJALI YA MOTO ULIYOTOKEA KATIKA NYUMBA HIYO WIKI LIYOPITA

 kama Mungu hajampangia mtu kifo,hata vitendo vya kishetani vya mauaji vikifanywa na watu au mtu haviwezi kufanikiwa.Ndivyo Mungu alivyoonyesha miujiza yake usiku wa saa 2.baada ya mama huyo,Mrs Sikapundwa alivyo taka kupata kifo kibaya cha kuungulia ndani ya nyumba,namshukuru sana Mungu,majirani kikosi cha Zimamoto cha Manispaa ya Dodoma kwa jitihada zao za kuvunja dirisha na kumwokoa mama huyo.
 Isitoshe Mke wa mwanagu mkubwa Bibi Coleta Epimak Sikapundwa naye alitaka kuwa katika kifo hicho cha kinyama,lakini Mungu alikataa,kilikuwa kilio kikubwa cha kutisha.E Mungu uabudiwe sana.
Watatu ni mtotoBinti wa darasa la saba Sarah Sikapundwa,kulia akiwa na Bibi yake Mrs Sikapundwa mwenye kitambaa cheupe kichwani.Leo nisngekuwa nao hao duniani,kwa ajili ya watu wenye uwezo wa kuwa na mamlaka ya maisha ya watu wengine zaidi ya Mungu ,lakini kaonyesha kuwa yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa mamlaka na uhaia wa mtu.

1 comment:

  1. Pole sana Mzee Sikapundwa, kwa tatizo hili kubwa. Kama usemavyo, Mungu ni mkubwa na ndiye anayeongoza maisha yetu. Nawatakieni kila la heri katika kujipanga upya kutokana na tatizo hili, na kuangalia mbele.

    ReplyDelete