Monday, May 23, 2011

IPI MAANA HALISI YA LUGHA?


Baadhi ya wana- Isimu wanadai kuwa Lugha ni:-
  • Hill ( 1958 ) huyo alidai kuwa  lugha ni umbo asili lililoshonana sana ambalo alama zake zinatokana na sauti zinazofanywa na ala za sauti katika binadamu. Na
  • Hall ( 1960 ) yeye lugha kwake ni mpangilio wa sauti ambazo kwao hufanya maumbo yenye maana. Lakini
  • Lado ( 1964) akasema lugha ni chombo cha mawasiliano baina ya binadamu katika jumuiya fulani. Naye,
  • Potter ( 1960 ) ameona lugha ni utaratibu wa alama za sauti zilizopangiliwa kutokana na mazoezi au matamshi ya watu.

Ni mtazamo upi utasema maana ya lugha ni sahihi kati ya tafsiri hizo hapo zilizotolewa na wana – Isimu hao.Kama haitoshi wana – Isimu hawa nao mitazamo yao ni hii:-
  • Mhina /Kiimbila ( 1971 ) Mtazamo wake kuhusu Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa,ambazo kikundi Fulani cha watu hutumia kwa kuwasiliana au kuiwezesha jumuiya ya watu wa utamaduni wapeane habari.Hivyo hivyo naye:-
  • Mbunda ( 1976) kadai kuwa lugha ni kujieleza au tufikiriavyo na kupelekeana habari baina ya binadamu kwa njia ya sauti zinazotamkwa na kusikika.

Ni mitazamo ipi ambayo inaweza  kuleta maana ya lugha kati ya mitazamo ya Wana – Isimu  waliyo toa kuhusu maana ya lugha? Nii imani yangu wana - Isimu na si wana - Isimu wa lugha watanisaidia  na wengine wenye kutaka kujua maana ya lugha.

No comments:

Post a Comment