Wednesday, May 4, 2011

Naibu Waziri wa Nchi Elimu TAMISEMI akagua madarasa Namtumbo


NAIBU Waziri wa Nchi Elimu TAMISEMI Mhe. Kasimu Majaliwa leo ame kagua vyumba viwili vya madara katika shule ya msingi Mchomolo vilivyojengwa na wananchi wakishirikiana na TASAF katika Halmashauri ya Namtumbo  katika siku yake tatu ya ziara ya kukagua shughuli za elimu katika mkoa wa Ruvuma.

Mhe. Majaliwa baada ya kukagua madarasa hayo alizungumza na wanafunzi kisha akaendela na ziara yake katika High School ya kidato cha tano na sita ambapo alikagua mabweni,samani za shule na kusungumza na wanafunzi.

Aidha aliwaambia wanafunzi wasome kwa bidii kwani taifa linawategemea wao katika kuendeleza shughuli za uzalishaji mali,pia alimshukuru Mkurugrnzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya  hiyo kwa ahadi yake ya kuinunulia bajaji sekondari hiyo,pia akaongezea kusema kuwa serikali nayo ikombioni kapele magari katika high school zotenchini  fedha ikipatikana.( Source Kanisia Mhagama )

No comments:

Post a Comment