Sikiliza mkasa huu anauelezea Padre Basley Malenda.
Kijana mmoja jina lake
hakulitaja alipendwa sana na wazazi wake,pia yeye aliwapenda
wazazi wake kila walicho mwambia alikitii.Lakini kijana huyo alitaka kuingia
kwenye wito wa Upadre.Akawaambia wazazi wake azma yake hapo baadaye.
Wazazi hawakuwa tayari kumruhusu ila walimtafutia mchumba
mzuri sana,na mchumba naye alimpenda sana kijana,akawa anafika kumfulia
nguo,kumpikia,ila kijana bado alisikia wito unamwita.
Kijana aliamua kwenda kwa Padre amweleze yanayo
mtatiza,Padre akamuuliza ni kweli wanakupenda hao,kijana akajibu ndiyo.Padre
alimwambia aende nyumbani,basi yule Padre alisali pale muda kidogo kilio
kilisikika kwa yule mzee kuwa kijana amekufa.
Basi walipo peleka kuzika padre yuleyule alisalia
maiti,kisha akawambia waingize mwili kaburini,yule binti naye akaingia kwa
uchungu kuwa anampenda sana,mara
mtu mmoja akasema mfukieni nay eye,Binti aliruka kuwa haiwezekani.
Basi padre akawaambia toeni mwili nje ya kaburi,akamuuliza
mama mzazi kuwa uko tayari kijana wako awemzima maana nina uwezo kwa kumfanya
awe hai.yule mama alisema hapana nitamzaa mwingine.Baba naye alipo ulizwa
alisema huyu kafa basi tutatafuta motto mweingine.
Zamu ikafika kwa mchumba akaulizwa kama
mchumba wake akiwa hai atakuwa tayari kuwa naye? Mchumba alisema mbona wanaume
wako wengi.Basi aliwambia waliofunga sanduku walifungue.kijana akaamka kisha
padre alimuuliza kuwa kama huko ulikokuwa alisikia baba ,mama na mchumba wake walivyokuwa
wakisema,alisema niliwasikia wote.
Ndipo yule alipogungua kumbe hakuna upendo wa dhati miongoni
mwa binadamu, binadamu na kifo,wanasema kwa nje tu maoyoni hakuna.Ndipo Padre Malenda aliposema
mototo kama anawito wa upadre mruhusu akaitikie
wito kwa aliye mwita kuwa mchungaji wa konddo zake.
No comments:
Post a Comment