Friday, May 13, 2011

APOTEZA FAHAMU BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA POLISI LINDI

 Aliyetuhumiwa kuingia mpirani bila kiingilio Bwana Ally  akiwa chumba cha kupiga picha akiwa hana fahamu katika hospitali ya sokoine mkoani Lindi

 Bwana Ally aliwa mapokezi akisubiri aingie kwa mganga ili amwandikie na apate matibabu huku akiwa hajijui yuko wapi,kwa sababu ya kupokea mkong'oto kutoka kwa askari polisi.Dezo mara nyingi inahasara au balaa kama lililofika bw.Ally
 Sehemu ya bega huwenda alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali,si unajua polisi tena hachagui pa kupiga,kutokana na mafunzo yao Ethics zao,na kama alikuwa hajawahi kukutana na mharifu basi akikukuta hasira zote za mafunzo zitaishia hapohapo.
 Hapo bwana Ally amepata matibabu yuko hoi bin taabani,amepata fahamu akisubiri kurudi nyumbani kwake akawasumulie mshahara wa kuzamia viwanjani Gate Crusher ,Sijui siku nyingine kama atajaribu tena na polisi watawaona kama wakwe zake.
Ilikuwa siyo masihala ilikuwa ni kipigo kwenda mbele sasa mikono kama imevimba hivyo kweli ataacha kupoteza fahamu.Lakini hawa polisi wanalinda usalama wa raia na mali zao,kwa mtindo huu utakubaliana na usemi huo?


MTU mmoja mkazi wa Manispaa ya Lindi Bwana Ally Ahmeid amepoteza fahamu baada ya kupokea kipigo kutoka kwa polisi kilichoongozwa na askari G 6617 John wa kituo cha Lindi,alipojaribu kuingia mpirani bila kulipa kiingilio.akaone mchezo timu ya Ilulu Stars na Ruvuma worriers hivi karibuni.

Mwangalizi wa Haki za Binadamu wa wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi Bwana Christopher Lilai amesema kuwa mtuhumiwa baada ya kupokea kipigo hicho alikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine Hospital  ( Source Christopher Lilai Lindi )

No comments:

Post a Comment