Msoma mashairi wa siku ya MEI MOSI mwaka huu katika uwanja wa majimaji Songea Bwana Salumu Rashidi wa Msikiti wa Ijumaa Mahenge Manispaa ya Songea. Na kibwagizo chake kisemacho Mkoa wetu wa Ruvuma unalisha mikoa mingi.Ina maana Mkoa huu unazalisha chaukula kingi na ziada.
Kwa hiyo watunzi wa mashairi wajikite katika fani hii ambayo vijana wengi wa sasa wameipa kisogo utunzi wa mashairi.Tukumbuke mashairi tuliosoma zamani ya 'Sisi balogi hatuna aibu,Tunaingia nyumba pasipo mlango.'.katika kukua kwa lugha ya Kiswahili Mashairi yalikuwa miongoni mwa nyanja zilizo fanya kiswahili kijulikane.
Ni kweli, lugha ya mashairi si sawa na lugha ya kawaida. Inahitaji tafakari, nidhamu, na ufahamu wa hali ya juu. Ili tuweze kujipima kama tumefikia kiwango, inabidi tuwe tunasoma mashairi ya zamani, kama vile "Hamziya," "Al-Inkishafi," "Rasi'Ghuli" na "Mwana Kupona," na pia mashairi ya karne zetu hizi, kama vile yale ya Shaaban Robert, Amiri Andanenga, Ahmed Sheikh Nabhany, na Haji Gora Haji.
ReplyDeleteTusipofanya juhudi ya kusoma namna hiyo, tena kwa makini sana, na kwa maisha yetu yote, hata utungaji wetu utapwaya. Vitabu vipo nchini, ila tatizo ni uvivu wa jamii yetu katika suala la kununua na kusoma vitabu.