Wednesday, May 11, 2011

UTEGEMEZI WA WANAWAKE KWA WANAUME SASA HAUNA NAFASI - MHAGAMA

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake ( UWT ) Mkoa wa Ruvuma Bibi Kulthum O.Mhagama ameiambia Blog hii kuwa kipindi cha wanawake kuwa tegemezi kutoka kwa waume zao au wanaume kimepitwa na wakati.Aliema kuwa yeye kaitka nafasi aliyopewa katika mkoa amehakikisha wanawake wanajiingiza kwenye ujasiriamali kwa kuingia kwenye vikundi vya uzalishaji mali.

Bibi Mhagama amesema kuwa ameshahasisha wanawake kuanzisha miradi ya upandaji miti ambayo baadaye watapata mbao ,ambapo Mbinga wamepanda miti heka 10,Tunduru miti heka 30,Namtumbo mitu heka 60 upandaji wa miti hiyo ni mradi yao wanawake wa mkoa huo,lakini pia inachangia katika kuhifadhi mazingira.

Aidha alisema kuwa amewahasisha wanawake katika mkoa kupnda mazao  yasiyo hitaji mbole za viwandani kama vile ulezi,mpunga,soya,karanga kwa lengo la kuwasaidia wale ambao hatakuwa na uwezo wa kununua mbolea za viwandani.

Pia alisema amewahamasisha wanawake kuwafanya kazi katika vikundi vya uzalishaji mali vya usindikaji wa vyakula,kwa kupata mikopo kutoka SIDO,Better Life Mhe.Mbunge Manyaya,na VICCOBA Mhe. Likokola.

Vingine ni vikundi  300 vya sindikaji wa juisi,jam,pombe kali kule Mbinga na kati ya vikundi hivyo kuna vikundi vya utengenezaji wa nguo za batiki na wafugaji wa kuku wakienyeji mkoa mzima.( viongozi kama hawa ndiyo wanaotakiwa kipindi hiki cha kujishughulisha si vyema kutegemea kila kitu kutoka kwa mwanaume).



No comments:

Post a Comment