Wednesday, May 11, 2011

MASISTA WA DMI WASAIDIA WANAWAKE 6,000 NA WATOTO 3,500 KATIKA VIJIJI 45 VYA SONGEA MKOA WA RUVUMA

 Sister Jaculine SOOSAI Mary ( DMI ) ni mkuu wa chuo kikuu cha Teknolojia ya Kompyuta Saayansi kilichopo Ruhuwiko Mkoani Ruvumua.Masisita hawa wa Bikira na Washirika wa DMI watawa wanaojitolea kusaidia masikini na wasiojiweza bila masharti yoyote ambao makao makuu yao yako India.


Shirika hili limefanya kazi katika vijiji 45 vya Songea na kusaidia zaidi wa wanawake 6,000 na watoto 3,500 kwa lengo la kuinua haki za watoto,kuthamini elimu ya watoto,kuwainua kielimu watoto masikini,kuimarisha uangalizi wa watoto walioko kituoni na kusimamia mipango ya mila na desturi.


Aidha shirika hilo linatarajia kujenga kituo cha watoto yatima na watoto wenye mazingira magumu na watoto wa kawaida chenye kugharimu shilingi milioni mia sita,( 600,000,000/= ) kati ya hizo shilingi milioni mia tano zitatolewa na shirika la India na shilingi milioni mia moja ichangiwe na wnanchi wa Mkoa wa Ruvuma na wenyeji wanaoishi nje ya mkoa wa Ruvuma wenye uchungu na watoto hao.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt. Christine Ishengoma ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuchangia chochote mtu alicho kuwa nacho ili kituo hicho kijengwe kama kijiji cha kuwalea watoto hao zikiwemo familia zitakazo teuliwa na shirika hilo ili watoto hao wajue kuwa kumbe hao ni wazazi wao.
Aidha Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri wamekabidhiwa vitabu vya stakabadhi kwa ajili ya makusanyo ya fedha hizo.
Mwalimu Soeciosa Katambala mwenye kiti wa DMI akielezea jinsi shirika hilo linavyo fanya kazi hapa Tanzania na nchi nyingine Duniani katika kikao cha ushauri cha mkoa RCC katika ukumbi wa Songea Club jana.

No comments:

Post a Comment