Mwenyekiti wakikao cha Bodi ya barabara TANROADS cha mkoa Dkt Christine Ishengoma alisema mkoa wake una mtandao barabara kilometa 5,485.5 kati ya hizo kilometa 216.5 sawa na asilimia 4 ndizo za kiwango cha lami na kati ya hizo kilometa 18.5 ni lami ya Halmashauri ya Mbinga,na halmashauri za Tunduru na Namtumbo hazina lami Labda baada ya kumaliza miradi ya barabara za kiwango cha lami.
Dkt Ishengoma alisema viongozi wa kada zote katika Halmashauri zote kusimamia thamani za ujenzi wa miradi ya barabara ili zifikie kiwango kilichokusudiwa na wananchi.
Aidha amekemea vitendo vinavyo fanywa na baadhi ya wafanya kazi wa ujenzi wa barabara ya Songea Namtumbo vya kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi wa barabara hiyo,na si kwa barabara hiu bali na kwa miradi mingine ya barabara,kwa kuwa vitendo hivyo vinachelewesha miradi kukamilika kwa wakati uliyopangwa.
No comments:
Post a Comment