Thursday, August 30, 2012

BWANA JUMA NYUMAYO AKARIBISHA WAFANYA KAZI WENZAKE NA WAGENI ENGINE NYUMBANI KWAO KWENYE MSIBA WA MKE WA MDOGOWAKE ASKARI WA JWTZ MSHANGANO JANA

 Bwana Juma Nyumayo akiwaonyesha sehamu ya kukaa,wageni na wafanyakazi wenzake wa ofisi ya TUJIFUNZE jana kwenye mazishi ya mpendwa shemeji yake mke wa mdogowake ambaye ni askari wa JWTZ yaliyo fanyika kwenye makaburi ya nyumbani kwao Mshangano.
 Ili kuwa na ulinzi wa kutosha Bw.Nyumayo alikuwa akimwelekeza kitu mbwa wake nje ya kibanda chake hapo jana baada ya mazishi.
Hapa viongozi wa Dini pamoja na Bw.Nyumayoa wakiandaa Sanda kwa ajili ya kwenda kuuvesha mwili wa marehemu.
Ndani ya chumba ambamo baadhi ya akina mama wafiwa walikuwa akimfariji mama mfiwa hapo jana kabla ya mazishi.
 Hapo ni eneo la makaburi ambapo vijana hao wanaonekana wakiandaa mahali ambapo marehemu atakapo hifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele.Na roho ya Marehemu Mama Juma ipunzike kwa amani mahali pema peponi Amen.


Chumba ambapa baadhi ya akina mama wafiwa wakimfariji mama mzazi wa marehemu Mama Juma watatu kutoka kulia aliyefunga kitambaa kichwani na shuka jekundu.Mama Malika.

Sunday, August 26, 2012

SHEREHE ZA JUBILEI YA MIAKA 25 YA JIMBO LA MBINGA PAMOJA NA MIAKA 25 YA ASKOFU MSTAAFU EMMANUEL MAPUNDA,RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA AHUDHURIA LEO

 Askofu Emmanuel Mapunda
 Rais Mstaafu Mkapa
 Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbert Mtega
Waumini kanisani Mbinga,

RAIS AHESABIWA NA FAMILIA YAKE NYUMBANI KWAKE IKULU,KISHA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA KUSEMA WAACHE KUANDIKA HABARI ZA KUCHOCHEA

 Rais Kikwete azungumza na waandishi wa habari leo Ikulu baada ya kuhesabiwa na familia yake
 Kikwete akisikilia maswali kutoka kwa waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam leo baada ya kuhesabiwa
 Rais akiwaambia waandishi hao kuacha kuandika habari za uchochezi zitakazo wafanya waliyojifungia msikitini kuwa na nguvu zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akipigilia msumari kwa wale waliyo patikana na nyaraka za kuwaasa waislamu wasihesabiwe akiwemo kijana wa Chuo kikuu,alisema ndani yake wapo viongozi wakubwa na wanatambulika kwa majina ila hakuna haja ya kuwatangaza kupitia vyombo vya habari .' Hao tutakula nao ' alisema.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amehesabiwa na familia yake nyumbani kwake Ikulu leo asubuhi,katika chumba cha siri kwakuwa sensa ni siri ya anae hesabiwa na karani wa sensa.
Baada ya kuhesabiwa Rais aliongea na waandishi wa habari waliyofika katika zoezi hilo,ambapo alirudia yale ambayo aliyazungumza katika hotuba yake aliyoitoa kupitia vyombo vya habari.
Aidha waandishi nao waliuliza kuwa baadhi ya watu wameonekana kuwa wamefanya vitendo vya kushawishi watu wasihesabiwe kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria.Rais aliwajibu kuwa maelekezo yametolewa jana kupitia hotuba yake na kwamba kwa kua zoezi ni la siku 7 watu hao watashughulikiwa iwapo watazidi kuendelea na harakati zao.
Ila alitoa angalizo kwa vyombo vya habari kuandika habari za kuchochea,maana habari mbaya kwao ndiyo habari nzuri.wakizisikia wanajua kuwa hoja zao zimesikika,hasa wale waliyo jifungia katika misikiti Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Moa wa Lindi awataka wananchi kushiriki na kutoa ushirikiano na makarani wa Sensa zoezi lililo anza leo nchini kwa siku 7

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Ludovick Mwananzila amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa iliyoanza leo nchi nzima.
Aidha mkuu huyo amesema kuwa yeyote atakaye bainika kuwasahwishi wananchi kuacha kuhesabiwa ,hatua  za kisheria zitachukuliwa zidi yake.

ZOEZI LA SENSA KATIKA MANISPAA YA SONGEA LIMEANZA VIZURI - KATIKA MTAA WA SABASABA MATARAWE NA MARIA KIBUMU

 Karani wa Sensa akijaza mambo muhimu kwa mkuu wa kaya katika mtaa wa Sabasaba Matarawe Manispaa ya Songea saa 1.30 leo.
 Karani wa Sensa Bi. Maria Kibumu akiendelea kujaza taarifa muhimu za mkuu wa kaya ndani ya uwanja wa Sabasaba leo.
 Wa kwanza kushoto ni Mjumbe Mzee Razalo Luambano akiwa na Karani wa Sensa Bi. Maria Kibumu kuhakikisha zoezi hilo linaenda vizuri.
 Bi.Maria kibumu alisema kuwa hajapambana na tatizo lolote katika zoezi hilo katika mtaa wake ,ipokuwa siku tatu za nyuma alicheleweshwa kupata idadi ya watoto wa shule ya watoto wadogo ya Charity iliyoko ndani ya uwanja wa Sabasaba.
Sensa ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa na watu wake,hivyo watu ambao wanashabikia watu wasihesabiwe,ni kosa watu kama hao si wema wa Taifa letu linye sifa tele ya Amani na utulivu miongoni mwa wananchi wake.
Sera ya nchi ni Sera isiyokuwa na udini,ukabila, rangi ama Itikadi,ila ni Sera inayo jali maendeleo ya kila mwananchi kwa Itikadi yoyote,Imani yoyote.

Mjusi na takwimu za mashirika isiwe sababu ya kususia Sensa – Dr.Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aongea na wananchi kupitia vyombo vya habari ,kama kaida yake kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa kuhesabiwa katika Sensa iliyoanza saa 6 usiku kwa wasafiri na wenye mazingira magumu.





RAIS wa Jamhuri ya Tanzania Dr.Jakaya Kikwete amewaasa wananchi kujitokeza katika sensa iliyoanza jana usiku  kwa wasafiri na watu walioko katika mazingira magumu,kuhesabiwa na kuwapa ushirikiano wa kutosha Makarani wa Sena,na kwamba madai ya kurudishwa mifupa ya Mjunsi iliyoko Ujerumani,na madai ya viongozi na wanaharakati wa Dini ya kiislamu ya Takwimu zilizotolewa na mashirika visiwe vigezo vya kususia Sensa.
Alisema kuwa kususia sensa kwa sababu hizo ni kutoitendea haki serikali,kwa kuwa taarifa za Takwimu zinatolewa na ofisi ya Taifa ya Sensa na siyo ya mashirika.na katika sensa hakuna masuala ya udini au rangi,Sera yetu haiusiki na sera za ubaguzi wa rangi au udini kama ilivyo wakati wa Ukoloni,kwa kuwa wakoloni walikuwa na Sera za ubaguzi.
    Hivyo Rais amewataka wananchi kushiriki katika Sensa kwa maendeleo ya Taifa letu na si vingine,Aidha amewataka viongozi wa vyama,Serikali kusimamia zoezi hili lifanikiwe katika maeneo yao.
      Katika Mkoa wa Ruvuma zoezi hilo limeanza ,ambapo makarani wa Sensa wameshapata vifaa vyote vinavyo husiana na zoezi hili na hivi sapo katika kuhesabu watu katika kata zao.Ikiwemo Mtaa wa Sabasaba na nje ya uwanja wa sabasaba Matarawe manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Katani wa Sensa Bi. Maria Kibumu na Mjumbe wake  Razalo Luambano wamesha pitia zaidi ya kaya 5 na wanasema hawaja kumbana na matatizo yoyote hadi muda tuna kwenda mitamboni.



Sunday, August 19, 2012

BARAZA LA IDD LIMESOMWA KATIKA UKUMBI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA SONGEA LEO

Mji wa Songea na vitongoji vyake ni shamra shamra kwenda mbele,inapendeza,unapofika kwenye makutano ya barabara ya kanisa kuu na ya kutokea msikiti wa mkoa ,inapendeza kweli siku kuu ilivyo angukia Juma pili.Karibu sana kwetu Songea Ruvuma.

Tuesday, August 14, 2012

WANAFUNZI 20 WATUNUKIWA ZAWADI KWA UFAULU WA DARAJA LA KWANZA KIDATO CHA SITA MWAKA 2012



WANAFUNZI 20 walifanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita mwaka huu wametunukiwa zawadi na Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo,kati yao Wavulana 10 na Wasichana 10 kutoka katika shule kumi bora nchini.
Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Shukuru Kawambwa kuwa zawadi hizo ni pamoja na Cheti, Laptop na shilingi 200,000 kila mmoja kutokana na kufanya vizuri katika masomo ya sayansi,Mhe. Kawambwa alisema kuwa wanafunzi hao wametoka katika shule 8  za Serikali na mbili ( 2 ) kutoka shule binafsi ,amezitaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule za sekondari za Kibaha,Mpwapwa,Mzumbe,Kilakala,Ifunda,Fedha,Mariani,Tabora , Minaki na Tabora wasichana.
Aidha shule 10 zilizofanya vizuri katika masomo zimezawadiwa shilingi milioni moja kila shule,ambapo zawadi hizo zitatolewa na Waziri Mkuu Mhe. Pinda kwa wakuu wa shule hizo jioni hii leo.

Friday, August 10, 2012

MUNGU NI MUUMBAJI WA VITU VYOTE NA HAINAMAKOSA

Sikuwepo katika mtandao sasa nimerudi tena,kwa nguvu ya uumbaji wa Mungu ,anaweza kufanya chote katika uumbaji wake kuonyesha uwepo wake.Fatilia na kuchunguza picha hiyo ya akina dada hao,Haina tofauti na watoto wa kike waliyozaliwa Makete waliyo ungana kwa kubebana.

Hiyo ndiyo kazi ya muumba wetu yote ni mema kwetu.