SHULE kongwe za Kigonsera ya Songea boys zitapewa shilingi
100,000,000 na serikali kwa ajili ya
ukarabati wa majengo na miundombinu,ambapo shule ya wasichana ya Songea
imeshapewa sh.50,000,000 wanachotakiwa warudishe mchanganuo wa matumizi wapewe
nyingine.
Hayo yamaesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Elimu TAMISEMI
Mhe.Kassim Majaliwa wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani Ruvuma katika ukumbi wa songea Club hapo jana.
Mh.Majaliwa alisema kila shule italetewa shilingi 50,000,000
ila kwa shule ya sekondari ya Kigonsera fedha hizo wazitumie kwa kununulia
jenereta kubwa lenge uwezo wa kufua umeme wakusambaza shuleni hapo.
Sambamba na hilo waziri alisema kuna upungufu wa walimu
40,000 wa shule za sekondari na 179,000 wa shule za msingi nchini.ambapo pengo
hilo litazibwa hivi karibuni kwakuwa walimu wa stashahada na shahada watamaliza
mwaka huu na mwakani.
No comments:
Post a Comment