Wednesday, May 11, 2011

BILIONI MOJA ZATUMIKA KUJENGA DARAJA LA KALULU TUNDURU LAKINI HADI LEO HALIJA KAMILIKA

'Miradi mikubwa na midogo ya ujenzi wa barabara haitakuwa na ubora  na viwango kama hakuna utaalamu wa kutosha,usimamizi na ushauri.' alisema Mbunge wa Tunduru Mhe.Ramo Makani.


MIRADI mikubwa ya ujenzi wa barabara ni muhimu kuzingatia maelekezo ya wataalamu ( Professional) katika kupata barabara zenye viwango na bora zenye kuonyesha ukomavu wa utaalamu alionao mjenzi wa barabara husika.

Mbunge wa Tunduru Mheshimiwa Ramo Makani alisema hayo na Blog hii kwenye kikao cha  kamati za barabara za mkoa  TANROAD kilichofanyika katika ukumbi wa Songea Club leo .

 Mhe.Makani alisema kuwa miradi ya barabara lazima ifuate kanuni ya utatu katika utekelezaji wake,alitaja utatu huo kuwa ni pamoja na Mmiliki ( owner )  wa mradi,Mhandisi mshauri ambaye atafanya bajeti,michoro na mkandarasi.

Alisema kuwa miradi hiyo lazima utalamu wa wahandisi utumike katika kuhakikisha ubora,gharama halisi itakayo tumika katika mradi,kujipanga.ndipo zabuni zinaitishwa za ujenzi wa barabara.

Kisha mhandisi mshauri  nakuwa na wataalamu katika shughuli za ujenzi huo na kuhakikisha kazi inaisha kwa wakati waliokubaliana katika mkataba,baada ya ufuatiliaji na usimamizi wa hali ya juu.

Aidha alishangazwa na mradi wa ujenzi wa daraja la kalulu linalo unganisha Matemenga na Kalulu liligharimu shilingi bilioni moja lakini hadi leo daraja hilo lililoko Wilayani Tunduru halija kamilika.,inaelekea hakukuwepo msimamizi  na mshauri wa mradi huo.

No comments:

Post a Comment