Monday, May 9, 2011

DADA DESTERIA NDUNGURU NI MJASILIAMALI PIA ANAFUNDISHA KUDARIZI

 Aliyesimama ni Dada Desteria Ndunguru ambaye ni mkurugenzi katika kiwanda chake cha kudarizi mashuka,foronya na vitambaa vya mezani,masofa.shuka la futi sita kwa sita kitanda na foronya mbili pinki kama lile karibu yake ni Tshs.29,000/= na blue,kijani ni Tsh.27,000/=

Lakini Dada Ndunguru pia anafundisha wasichana kudarizi miezi sita tu wanakuwa  wanafahamu na kwenda kujiajiri wenyewe.Ada ni Tshs 100,000/= akiingia Tshs.50,000/= akimaliza course yake anamalizia Tshs 50,000/=
Hayo ni mashuka yanauzwa yakiwa na foronya mbili

Ana Vyereheni vya Kudarizi vitatu ( 3 ) Dada Ndunguru anasema wanafunzi wako wa awamu mbili wanaoanza asubuhi mpaka saa sita na saa sita mpaka saa 12.Kwa hiyo watu Talented kama Dada Ndunguru wakipatikana wengi masuala ya ajira yata kuwa ndoto.maana vijana wengi watakuwa wanajipatia fedha kwa kutumia ufundi walioupata.

1 comment:

  1. Shukrani kwa taarifa hii. Kweli Dada Ndunguru anafanya jambo muhimu sana katika maisha ya hao wasichana, tukizingatia matatizo ya ajira yalivyo.

    Katika dunia ya leo, suala la ujasiriamali linatiliwa kipaumbele, tofauti na miaka ya ujana wetu sisi, ambapo ilikuwa unaenda shule na ukimaliza unapata ajira serikalini au kwenye mashirika.

    Namtakia Dada Ndunguru kila la heri na mafanikio zaidi na zaidi katika shughuli hizi.

    ReplyDelete