Wednesday, October 31, 2012

TAASISI YA MASHEIKH NA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA WATOA TAMKO LAO KUHUSU GHASIA ZILIZIJITOKEZA


                                   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO la jopo la Masheikh na  Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania lililotolewa tarehe 19/01/ 2011,Jijini Dar es Salaam liliwakumbusha watanzania umuhimu wa kuzingatia utawala wa sheria na kutii  amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.
     Jopo la Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania limesikitishwa sana na kitendo cha kunajisiwa Qur’aan Tukufu, Surat Al Waaqia’h (56) Aya ya 76.
Jopo hilo limehuzunishwa na kitendo cha polisi cha kuchelewesha kuchukua hatua za haraka baada ya kitendo hicho kutokea, ambapo kumechangia kuamsha hamasa mbaya na hasira za Waislam.
     Isitoshe Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imesikitishwa na mihemko  hasi na ghadhabu za baadhi ya Waislamu kufanya vitendo mbalimbali vya uhalifu vikiwemo vya uchomaji wa Makanisa na kuharibu mali za watu kwani Uislam hauluhusu mlalamikaji  kujipa haki ya kuhukumu na kuadhibu.
      Aidha Taasisi hiyo imestushwa na baadhi ya matamko ya viongozi wenzao wa Dini ya Kikristo kuitumia kadhia hiyo kuitia doa Uislam na Waislam kitu kitakacho tikisa misingi ya udugu wao na utanzania wao kiasi cha kutamani kuzaliwa ‘ Tanzania mpya’ iliyo fumbo kubwa,na hivyo kuzua hofu juu ya mustakbal wao kama taifa.
       Vilevile Taasisi hiyo haikupendezwa na baadhi ya Waislam kutumia mikusanyiko isiyo halali kupingana na Jeshi la polisi la kutaka kuachiliwa huru wenzao watuhumiwa ambao wako mikononi mwa chombo cha dola.
     Kadhalika Taasisi hiyo imepongea Jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama kwa kutuliza ghasia zilizojitokeza bila ya kutoa uhai wa mtanzania yeyote,pia kwa Masheikh na Maimamu na waislam wote waliyonyesha utulivu mkubwa katika kipindi kile kigumu.( Source  Sheikh Khamis Mataka katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislam Tanzania – Gazeti la Tazama Tanzania )

Tuesday, October 30, 2012

BAADA YA KUADIMIKA KWA SIKU KADHAA SASA NAJA NA UHABA WA MAJI ,PETROL NA DIZELI WAIKUMBA MANISPAA YA SONGEA KWA MUDA MREFU SASA

 Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma mwaka huu imekumbwa na uhaba wa maji baada ya vyanzo vya maji katika msitu wa Matogoro kukauka,kabisa lakini wataalamu wa mazingira wanadai kuwa kuna miti ambayo siyo rafiki wa maji  iliyopandwa katika msitu huo sasa imekuwa mikubwa na inanyonya maji yote yaliyopo ardhini.
kutokana na hilo maji yamekauka.hivyo wananchi wa Manispaa hiyo wanatumia maji yanayo uzwa na vijana wa yeboyebo na mikokoteni,bila ya kuelewa kuwa na maji salama ama la,yote ni kumwachia Mungu.
Wakati maji yame adimika katika Manispaa ya Songea , tatizo jingine limejitokeza la uhaba wa mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa.yanapo patikana ni foleni kwenda mbele Blog hii kesho itakuletea foleni hizo.

Saturday, October 20, 2012

SEND OFF OF DEODAT THOMAS MAGALI ROYAL VILLEGE DODOMA JANA IMEFANA SANA

 Deodata Thomas Magali na Mpambea wake wa pili kutoka kushoto wakiwa wenye tabasamu katika Send off yake iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Royal Village katika manispaa ya Dodoma.
 Deodata akimkabidhi Baba mkwe wake keki kwa heshima zot za Kiruguru katika sherehe hizo usiku wa kuamkia leo,

 Mr & Mrs Thomas  Magali wakiwapungua wageni waalikwa katika Send off ya Binti yao Mpendwa Deodata Thomas Magali katika Ukumbi wa Royal Village usiku wa kuamkia leo Katika Manispaa ya Dodoma.
M
 Mr Magali mdogo wa Bwana Thomas Magali ambayw alifanya utambulisho wa Familia ya Bwana na Bibi Magali kwa wageni waalikwa katika ukumbi wa Royal Village katika Manispaa ya Dodoma.
 Mr Thomas Magali Maneja wa Benki ya NMB Tawi la Mazengo katika manispaa ya Dodoma katika send off ya Binti yao mpendwa Deodata Magali Royal Vilaage,
 Mama Magali, mama wa Deodata Magali katika Sherehe ya Send off ya Binti yao mpendwa Deodata Magali Royal Village manispaa ya Dodoma.
Katika sherehe hizo wa wapambe na ndugu wa karibu  walishuhudia Deodata na Mpambe wake wakilishana  keki ikiwa kama ishara ya upendo na amani kati yao.wakwanza kulia ni Deodata.
Mama Sikapundwa mwenye nyeusi akienda kuwapongeza Deodata Magali na Mpambe wake wakatikwa kumpongeza.

Sunday, October 7, 2012

TUJIFUNZE KUSINI INAWATAKIA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE NCHINI MAFANIKIO MEMA KATIKA MITIHANI YAO YA KUMALIZA ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA NNE TAIFA

Watulie katika kufanya mitihani hiyo,wala wasibabaishwe na watu wenye uchu wa fedha kuwa wanauza mitihani , huo ni uongo na utapeli,toka lini mitihani iliuzwa kama karanga mitaani.
Kama mmoja wenu atasoma katika mtandao huu ,basi uwe balozi wa wenzako kuwa dawa ya kufaulu mtihani ni kujiandaa vyema na sio kununua au kuibia mtihanu.Tunawatakieni mafanikio mema katika kuvuna kile mlicho panda.

HIZO NDIZO JUHUDI ZA SERIKALI ZA KULIWEKA JIJI LA DAR ES SALAAM KATIKA HADHI YA KUITWA JIJI KATIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZAKE

 Hiyo ndiyo kampuni iliyopewa kupanua na kujenga barabara Jijini Dar es Salaam za magari na mabasi yaendayo kasi ,kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari/foleni,Pamoja na leo ni Jumapili lakini mpiga picha wa Blog hii amewakuta wafanya kazi wa kampuni hiyo wakiwa kazini saa 1.00 asubuhi Maeneo ya Mbezi.
Hiyo ndiyo jitihada za serikali katika kuboresha miundombinu ya barabara,eneo la Mbezi Jijini Dar es Salaam,wafanyakazi wa Kampuni wa upanuzi wa ujenzi wa barabara Jijini walikuwepo kazini,pamoja yakuwa leo ni Juma pili.

Saturday, October 6, 2012

MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM KARIBU UTAPUNGUA KUTOKANA NA UPANUZI WA BARABARA KUTOKA JANGWANI HADI MBEZI

 Ujenzi kutoka Magomeni Mapipa Jijini Dar es Salaam  Manzese Darajani ( na Christian Sikapundwa )
Ujenzi kuelekea Ubungo ukiwa manzese Darajani Jijini Dar es Salaam ,Ni kwa kiasi gani serikali ilivyo pania kupunguza msongamano wa magari Jijini kama unavyo shuhudia.
Barabara zikionekana kutokea Magomeni Mapipa kuelekea Ubungo.


Jitihada za Serikali za kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam zinaanza kuonyesha matunda.
Jitihada hizo zimeonekana katika maneo ya magomeni Mapipa ambapo kampuni inayojenga barabara imeweka kambi yake maeneo ya Jangwani inayo panua barabara hadi  Mbezi,nakwamba barabara hizo zikikamilika foleni ya magari katika Jiji hilo itapungua,hasa wakati wa asubuhi watu wakienda kazini na nyakati za alasiri watu wakitoka kazini kurudi nyumbani kwao.
Hayo ni majibu yanayotokana na ahadi za serikali ya Awamu ya nne wakati wa kunadi sera zake kupitia Chama Tawala.Na mwenye macho haambiwi tazama.

STENDI YA MABASI YA MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA SASA YA HAMIA VIWANJA VYA NANE NANE,BAADA YA MAMLAKA YA USTAWISHAJI WA MJI CDA KUTIFUA STENDI YA ZAMANI KWA GREDA ILI MABASI YASIENDELEE KUSIMAMA HAPO KWA KUKAIDI AMRI ILIYOTOLEWA NA MAMLAKA HAYO

 Hiyo ndiyo stendi ya mabasi mkoani Dodoma iliyoko maeneo ya Kisasa,katika viwanja vya nanenane,kuelekea Dar es Salaam,kati ya Ihumwa na Kisasa.
Baada ya muda kadhaa makao makuu ya nchi kukosa stendi ya kudumu na kuwa na stendi za muda katika maeneo  ya Reli karibu na Bohari ya Serikali mjini hapo sasa imehamishiwa Kisasa katika viwanja vya nanenane.Iwapo wataijenga kwa hadhi ya Stendi basi  eneo hilo ni zuri maana lipo ndani ya uwanja wa Nane nane.Tunawatakia wenye dhamana kufanikisha azma hiyo ili makao makuu yapate heshima yake.