Monday, May 23, 2011

BADRA ATAJA SABABU ZA KUKATIKA UMEME MARA KWA MARA

 Meneja wa  husiano wa TANESCO Badra Masoud amesema tatizo la kukati kwa umeme mara kwa mara ni kwa sababu ya uchakavu wa mitambo yake inayo tumia umeme wa maji.Alisema umeme wote unaozilishwa unatumika hakuna umeme wa ziada.Aidha alisema mgao unaoendelea sasa si wa TANESCO ni kwa sababu ya matengenezo ya mitambo ya umeme wa gesi Songosongo..Amesema umeme unaotumika hivi sasa ni MEGAWAT 350,na umeme wote wa maji,mafuta,na gesi unaozalishwa ni MEGAWAT 750
Amesema kuwa mitambo hiyo ni ya siku nyingi na kuifanyia ukarabati ni gharama kubwa ni bora kununua mitambo mipya .alisema umeme wote unaozalishwa ni kutoka kwenye vyanzo vya maji,mafuta na gesi.




LUGHA YA KISWAHILI ITUMIKE KUONYESHA UZALENDO - DKT. NCHIMBI

 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt  Emanuel Nchimbi amesema lugha ya kiwsahili itumike kuonyesha uzalendo wa Mtanzania.Lugha ambayo itamsaidia mtanzania kuwasiliana na mwenzake kiurahisi,watu watumie kiswahili kwenye ngoma,maigizo,michezo,mashairi,ngonjera,nyimbo.Dkt Nchimbi alitoa mifano kuwa kama kuna timu yetu inacheza na timu ya nje watu wanaishangilia timu hiyo,alisema huo ni ukosefu wa kinga ya uzalendo.
Dkt Nchimbi alisema hayo wakati wa kufungua kongamano la kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo.Alisema Lugha ya kiswahili ndiyo inayomwonyesha mtanzania na utamaduni wake.

Wanafunzi wajenge tabia ya kujifunza lugha ya kiswahili kwa kusoma vitabu mbalimbali,ili kukuza misamiati ya kiswahili,miundo,mbinu na tamathali za semi.

IPI MAANA HALISI YA LUGHA?


Baadhi ya wana- Isimu wanadai kuwa Lugha ni:-
  • Hill ( 1958 ) huyo alidai kuwa  lugha ni umbo asili lililoshonana sana ambalo alama zake zinatokana na sauti zinazofanywa na ala za sauti katika binadamu. Na
  • Hall ( 1960 ) yeye lugha kwake ni mpangilio wa sauti ambazo kwao hufanya maumbo yenye maana. Lakini
  • Lado ( 1964) akasema lugha ni chombo cha mawasiliano baina ya binadamu katika jumuiya fulani. Naye,
  • Potter ( 1960 ) ameona lugha ni utaratibu wa alama za sauti zilizopangiliwa kutokana na mazoezi au matamshi ya watu.

Ni mtazamo upi utasema maana ya lugha ni sahihi kati ya tafsiri hizo hapo zilizotolewa na wana – Isimu hao.Kama haitoshi wana – Isimu hawa nao mitazamo yao ni hii:-
  • Mhina /Kiimbila ( 1971 ) Mtazamo wake kuhusu Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa,ambazo kikundi Fulani cha watu hutumia kwa kuwasiliana au kuiwezesha jumuiya ya watu wa utamaduni wapeane habari.Hivyo hivyo naye:-
  • Mbunda ( 1976) kadai kuwa lugha ni kujieleza au tufikiriavyo na kupelekeana habari baina ya binadamu kwa njia ya sauti zinazotamkwa na kusikika.

Ni mitazamo ipi ambayo inaweza  kuleta maana ya lugha kati ya mitazamo ya Wana – Isimu  waliyo toa kuhusu maana ya lugha? Nii imani yangu wana - Isimu na si wana - Isimu wa lugha watanisaidia  na wengine wenye kutaka kujua maana ya lugha.

Sunday, May 22, 2011

LEO SHEREHE KULA AU KULWA MJINI SONGEA KUANZAIA JIMBONI HADI KWENYE VIGANGO VYAKE KOMUNIO YA KWANZA.

Nimbele ya kanisa Kuu la Jimbo Kuu la Songea waumini walikuwa wanatoka katika Ibada ya kwanza na kupisha Ibada ya Pili ambayo itakuwa ya Kutoa Komunio ya kwanza  kwa watoto wa shule zinazo zunguka mji wa Songea ambazo ni Mfaranyaki,majimaji, Majengo na Mashujaa.

KOMUNIO YA KWANZA ILIAMBATANA NA KWAYA KUKOLEZA IBADA HIYO.

 Kwaya ya Kigango cha Matarawe kikikolezea Ibada ya Komunio ya kwanza iliyotolewa na Mkurugenzi wa Miito Padre Nikodemas  Mbano.
 Padre Mbano anakomonisha watoto wa Komunio ya kwanza leo Aliyeshika Kalis ni Katekista au mwalimu wa dini wa watoto hao,kazi yake imedhihirisha pale walipoweza kujibu kaswali waliyo ulizwa kutoka kwenye katikesimu

Watoto hao wako tayari kwenda kukomunika kwa mara yao ya kwanza.Baada ya Sakramenti hiyo watoto hawa  watatakiwa kupata Kipemara.kulingana na Imani yao ya Romani Catholic ili akamilike katika uumini wao.

65 wapata Communio ya kwanza Kigango cha Matarawe

 Mkurugrnzi wa Miito wa Jimbo kuu la Songea padre Nikodemus Mbano  ametoa Kommunio ya kwanza kwa watoto 65 katika cha Matarawe Manispaa ya Songea leo.Hivi sasa sherehe hizo ziko kwenye familia zenye watoto hao kula na kunywa.

Picha hiyo hapo chini ni watoto wa komunioa ya kwanza wanakwenda kupokea Ekaristi kwa mara yao ya kwanza.
Mama aliyesimama ni mhudumu wakati ibada mwalimu Mama Kapinga.Akiangalia utaratibu wa kominika kwa watoto hao katika kigango hicho.

Saturday, May 21, 2011

SHEIKH YAHYA HUSSEIN AZIKWA LEO MAKABURI YA TAMBAZA JIJINI DAR.

 Rais Dkt Jakaya Kikwete amehudhuria mazishi ya Mnajimu wa Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein,mazishi yamefanyika katika makaburi ya Tamzana Jijini Dar es salaam leo.
 Baadhi ya waombolezaji wa msiba huo numbani kwake marehemu Sheikh Yahya Hussein leo
 Viongozi wa Dini wakiwa wamahitimisha sala ya kumsali marehemu katika makaburi ya Tambaza jioni ya leo
 Mheshimiwa Freeman Bowe asema kuwa Sheikh Yahaya Hussein alikuwa mtu wa watu pengo hilo halitazibika kiurahisi
Waombolezaji wakiwa na jeneza kuelekea makaburini,maelfu ya watu Jijini walifurika kumsindikiza Sheikh Yahya Hussein kwenye nyumba yake ya milele.Mungu ailaze roho ya Sheikh huyo mahali pema peponi.

WAPENZI WA BLOG NAWATAKIA WEEK END NJEMA YENYE AMANI NA UPENDO TELE

Furahieni Jumamosi karibu na Jumapili ambayo wengine Duniani watajumuika na wakristu wenzao kwenye majengo ya Ibada kumshukuru mungu kwa kuwaweka salama kwa wiki nzima na kufanikisha masuala yao ya kifamilia na kimaendeleo ya Taifa lao.

UGONJWA AUSIYO JULIKANA UMEZUKA TENA SHULE YA MSINGI JUHUDI ILIYOKO WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA LEO

 Wanafunzi wa shule ya msingi Juhudi wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma wamekubwa na ugonjwa wa ajabu ambapo mwanafunzi anaanguka na kupiga kelel kama vile anachapwa,Malimu mkuu wa shule hiyo Bwana Gabriel Ngoi anasema kuwa pamoja na maombezi yaliyo fanywa na waombaji kwa imani zao lakini haikusaidia chochote,
Inasemekana ugonjwa kama huo uliwahi kutokea mwaka uliyopita,Sasa wazazi ,Jamii na shule yenyewe inalichulia vipi suala hilo nyeti?

MWANAFUNZI KUMPANGIA NYUMBA MITAANI ATASOMA KWA MAKINI ?

 Inasikitisha sana kwa vitendo ambavyo wanafunzi waliopangiwa mitaani ili wawe karibu na shule,baadhi ya wapangishaji wa nyumba hizo kuwaona wanafunzi hao kama watu wazima hasa kwa wasichana kwa kuwataka kimapenzi ndani yao hata walimu wakawamo.Je huo ni ungwana ? kumfanyia hivyo mtoto wa menzako,ua ule usemi wa mtoto wa mwenzako ni wako ulipitwa na wakati?
Huyu mwanafunzi aliwaambia wenzake kuwa yeye ada ya shilingi  20,000 anajitafutia mwenye baada ya kutoka shuleni,huchukua madumu ya maji na kuyauza kwa kutumia baiskeli,basi huwa anachoka sana hata akifika shuleni hata mwalimu hawezi kusikiliza vyema.

WAKUU WA WA MKUTANO WA SADC WAHITIMISHWA LEO

 Katika kutano huo Rais Jakaya Kikwete alihudhuria,na baada ya huhitimisha mkutano huo Nchini Namibia aliwahi kwenye mazishi ya Mtabiri wa Afrika Mashariki Marehemu Shekhe Yahaya Hussein
 Pia Rais Robert Mugabe za Zimbabwe alikuwepo katika mkutano huo wa wakuu wa SADC Masuala ya Madagasca yalijadiliwa.
Mkutano huo utafanyika tena baadaye kukamilisha masuala mengine.

Friday, May 20, 2011

HIVYO NI BIASHARA GANI NZURI KUWA NA MABASI AU MALORI?

NI NANI ALAUMIWE ALIYERUNDIKA TAKA ILIBAADAE ZIKATUPWE AU WATOTO WANAOTAFUTA VITU KWENYE MADAMPO HAYO?

Hilo ni Guta la kuhifadhia taka mbalimbali zinazotolewa kwnye nyumba za wakazi wa eneo la shule ya msingi Mfaranyaki Manispaa ya Songea,Leo Blog  hii iliwakuta watoto wawili mmoja alijifanya kama hana habari na nini mwenzake ndani ya guta hilo kachakura chakura taka hizo ili apate kile anachotaka kukipata.

Taka ni mkusanyiko wa taka nyingi zimeshatumika na mahali palipotupwa taka  hizo napo ni pachafu pia,watoto kwenda kutafuta vitu hapo ni kujitafutia maradhi,sasa nani mwenye kosa aliyerundika taka hizo,au watoto wanaitafuta vitu kwenye taka hizo?

MMEM II NI MAFANIKIO YA MMEM I, MATUNDA YAMEONEKANA

 Mafanikio ya Mapango wa Maendeleo ya elimu ya Msingi ( MMEM ) I ni kuwa na Mpango wa pili wa MMEM II
 Mpango wa pili wa MMEM 2007 - 2011 ni kuboresha yale yaliyoanzishwa na MMEM I
Nini matokeo ya MMEM ni kuanzishwa kwa Mpango wa Mandeleo ya Elimu ya Sekondari MMES Mpango unaoboresha elimu ya sekondari,ambapo shule za sekondari za wananchi nyingi zimejengwa na watoto wengi wamanufaika na shule hizo vijana wengi kutoka katika shule hizo wamechaguliwa kuingia kidato cha tano.
Hivyo Mipango kama hiyo isidharauliwe  ila ni kuiboresha katika kujenga maabara,majengo ya utawala,walimu wa masomo ya sayansi na sayansi jamii wapelekwe ,waandaliwe mazingira rafiki ya kuishi na nyumba za walimu pamoja na maktaba.

HIVYO WAKULIMA HAWA WANAPATA FAIDA NA MAZAO YAO?

 Blogu hii leo imepita katika soko la mazao ya chakula SODECO Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma na kukuta shehena ya magunia ya mahindi ya msimu huu mengine yamelazimishwa kukauka ili wayauze kwa walanguzi kwa bei ya hasara.Lakini nilikutana na mkulima mmoja alisema mahindi hayo ya mwaka huu yanaizwa kwa sababu ya shida.
Akaendelea kusema kuwa wanalazimika kuuza kabla ya musimu wa kuyauza kwenye ghala la chakula la taifa kwa kuwa watoto wanahitaji ada,sare na matibabu.Mkoa wa Ruvuma mwaka huu utakuwa na mavuno makubwa ya mahindi ikilinganishwa na musimu uliyo pita.

MGAO WA UMEME HAUSABABISHWI NA TENESCO

 MENEJA wa mifumo mikuu ya umeme aliiambia TBC kuwa mgao wa umeme uliyotangazwa na vyombo ya Habari hausababishwi na shirika la umeme Tanzania TANESCO hii imesababishwa na matengenzo ya mitambo ya Gesi.Alisema kuna umeme wa maji ambao ni mkubwa,unafuatiwa na umeme wa mafuta na umeme wa Gesi.
 Mitambo ya kufufua umeme iliyoko Jijini Dar es salaam Ubungo
 Kama unatokea Tazara kuelekea Ubungo mkono wako wa kushoto ukiwa kwenye daladala zitokazo Mbagala kwende Ubongo  utaiona mitambo hiyo
Mitambo ya umeme wa Gesi inayofanyiwa matengenezo na kusababisha mgao wa umeme, mafundi ndio hao wanachakarika ili umeme urejee kama zamani.

MIPANGO YA MATENGENEZO YA BARABARA MWAKA 2010/2011 MKOANI RUVUMA YATAJWA

 MENEJA wa Wakala wa barabara TANROARDS Mkoani Ruvuma Injinia Ibraham Kasimbo aliyeshika kipaza sauti ,ametaja mipango ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 kuwa ni pamoja na :-
  • Matengeneo ya kawaida.
  • Matengenezo maalum.
  • Matengenezo ya kuboresha.
  • Matengenezo ya madaraja.
  • Matengenezo kwa kutumia fedha za maendeleo.
Alisema hayo siku ya kikao cha barabara (TANROARDS ) kilicho fanyika katika ukumbi wa Songea Club hivi karibuni.

Wajumbe waliyohudhuria kikao hicho walishukuru sana TANROARDS kwa kazi nzuri za utengenezaji wa barabara ya lami kutoka Songea hadi Lukumburu.Ila wameitaka TANROARDS kusimamia makandarasi kwa karibu zaidi.

Wednesday, May 18, 2011

VURUGU MGODI WA NORTH MARA WANANCHI WANAUWAWA FAIDA YA SERIKALI AU WENYE MGODI ?

Serikali lazima ithamanishe uhai wa wananchi na dhahabu zinazochukuliwa na wawekezaji Nchi kubakia na mashimo,kwa sababu wa - Tanzania wanaendela kufa kwenye migodi, Pia serikali haipati faida yoyote kwenye migodi hiyo,Ni miaka 50 ya Uhuru lakini migodi haija wanufaisha wananchi wa nchi hii.
Vyombo vinatumika vibaya sana maana Polisi ni wa serikali yetu ,lakini wanatumia nguvu bila kutafakari.Si wakati wa kulaumiana cha msingi wananchi wa maeneo hayo kufuata kanuni na sheria za haki.( Source Baragumu na Chanel TEN)

KITENDO CHA UBAKAJI KWA WAKIMBIZI NI UBINADAMU AU NI UNYAMA ?

  1. Wasomali na wa Ethiopia  wapatao 91 walioingia nchini Musumbiji bila kibali wamefanyiwa vitendo vya unyanyasaji ambapo binadamu wa kawaida hawezi kufanya hivyo,si kosa lao hawa hawana amani kwao.wanaume wamepigwa hadi kujeruhiwa,wanawake wamebakwa mbele za wanaume waliyo kuwa wamekimbia nao.
Wakimbizi hoa hawakupenda kukimbia nchi yao,wamekimbia kwa kutaka kusalimisha maisha yao,sasa wanakokimbilia kutafuta usalama nako hakuna amani.Hawa walitakiwa wapelekwe kwenye vyombo vya sheria sio kufanyiwa vitendo hivyo. ilitJe huo ni ubinadamu?
Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Mtwara Bwana Nestory Mpota amesema kuwa wakimbizi hao wamepokelewa mkoani humo wakati taratibu za kuwashita raia hao wa Somalia na Ethiopia kuingia nchini kinyume cha sheria. ( Source ITV )

BREAKING NEWS //////// SHERIA MYPA YA UFUGAJI MBWA NCHINI CHINA YAKOSESHA WATU RIZIKI

Sheria mpya iliyowekewa kwa wafuga mbwa nchini China itawaathiri kimaisha wananchi wanaotegema ujira wao kutokana na kuwa piga brashi mbwa wanao pelekwa kwenye saluni za watu wanaofanya kazi hiyo.

Inasemekana kuwa mtu anatakiwa kufuga mbwa mmoja ukilinganisha na sasa mtu mmoja na mbwa zaidi ya 10,kwa hiyo sheria ya kuwa na mbwa mmoja ita wafanya wa brashi mbwa wakose ajira maana idadi ya mbwa itakuwa ndogo.

VIKWAZO BARABARANI TUNDURU MTWARA NI TATIZO KWA WAFANYA BIASHARA

Vikwazo katika barabara ya Tunduru Mtwara vimekuwa kero kwa wafanya biashara wa kusafirisha mazao ya chakula kutoka wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kwenda Mkoa wa Mtwara.
Huyo mama yeye anasafirisha mpunga kutoka Tunduru kupeleka Mtwara anasema Tunduru wanalipia ushuru na katikati kuna vikwazo vingi mmno ambapo akilipia hapati hata lisiti ya kuonyesha.Anasema kutokana na malipo mengi njiani na bei ya mchele itakuwa juu,vinginevyo ataingia hasara.Je sasa kifanyike nini ili bei za vyakula isipande ?

BREAKING NEWS ............ZAIDI YA WAMEXIKO 500 MBARONI NCHINI MAREKANI

Imeripotiwa kuwa zaidi ya wa- Mexiko 500 wametiwa mbaroni nnchin Marekeni baada ya kukamatwa kwenye malori  wakiingia nchini humo bila ya kuwa na vibali.

MAMBO YA KUZINGATIA KUPATA HATI MILKI ZA KIMILA

Bi Agnes Julius Afisa Ardhi Sekretarieti Mkoa wa Ruvuma aliiambia RCC kuwa mtu akitaka kuomba kupata hati milki za kimila sharti :-
  • Kijiji kipime mipaka.
  • kipate cheti cha kijiji
  • mipaka ya kijiji itambuliwe
  • kuwe na matumizi bora ya ardhi
  • kujaza fomu namba 18
Alisema Wilaya ya Namtumbo imeandaa hati 6,298 imetoa  hati 5,850 na Mbinga imeandaa hati 250 imetoa hati160.

MWANA- MAZINGIRA AFAIDIKA NA MAZINGIRA YAKE KATIKA UJASIRIAMALI MJINI SONGEA

 Bwana Thomas Mwingira akiwaelezea watumishi wa TUJIFUNZE KUSINI mali ghafi zinazotumika katika utengenezaji mifagio hiyo mali ghafi hizo ni vipyagi na miti fagio mmoja na shilingi za Tanzania 5,000/=,awali miaka ya 70 Bw.Mwingira alikuwa Pailoti wa Ngede za Jeshi la Ulinzi Tanzania JWTZ Ukonga Dar es salaam.
Bwana Thomas Mwingira ni mkazi wa Chemchem Matogoro Manispaa ya Songea 45 ni mwana mazingira ana msitu wake wa miti ya kupanda pia mfugaji wa nyuki,vilevile ni fundi wa kutengeneza mifagio ya kufangilia na kudekia kama unAvyo mwona na fagio wake akionyesha katika ofisi za TUJIFUNZE KUSINI leo.

WALANGUZI WA SABABISHA VIKWAZO VINGI KATIKA BARABARA ZA MTWARA - NA LINDI

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Anatori Tarimo anasema kuwa walanguzi wa mazao ya korosho katika wilaya ya Tandahimba na wilaya nyingine mkoanai wana kwepa kulipa ushuru katika halmashauri za wilaya hizo na kukosesha mapato ya taifa.
Alisema kati ya Mtwara mjini  na Tandahimba toka asubuhi hadi jioni ni magari 10 ndiyo yanapita na kupata vibari vya kusafirisha mazao.lakini imegundulika walanguzi wengi wanakwepa kulipa ushuru katika Halmashauri lakini ni hao hao wanalalamikia mikoa ya Lindi na Mtwara ina vikwazo vingi barabarani. kuliko mikoa mingine.

HALMASHAURI NCHINI ZA HIMIZWA KUTUMIA RBC - MSHANA

Tuesday, May 17, 2011

Breaking News Asilimia 71 ya wakazi wa Lindi hawatumii chumvi yenye madini Joto

Wananchi wa Mkoa wa Lindi wengi hawatumii chumvi iliyo wekwa madini joto,Huyo ni muuzaji mdogo mdogo wa mji wa Lindi anasema bei ya madini joto iko juu shilingi 45,000 wao kama wauzaji wadogo hawawezi kumudu hivyo wanauza hivyo hivyo ili wayamudu maisha.
Uongozi wa mkoa huo unasisitiza watu watumie chumvi yenye madini joto kwa kuwa asilimia 71  ni kubwa mmno maana kuna hatari kubwa kupata magonjwa ya uvimbe wa goita.

MANISPAA YA SONGEA BARABARA ZAKE ZILIKUWA HIVYOO KULIKICHA KWELI

 Picha ilipigwa mwembechai  akiyaangalia magari yakielekea Lizaboni Manispaa ya Songea (Na Juma Nyumayao)



TANZIA ( BURIANI MWANDISHI WA HABARI HAPPY KULANGA

 Marehemu Happy Kulanga alikuwa akiandikia magazeti ya Mtanzaia,Tujifunze Kanda ya Kusini na Mtangazaji wa Radio Songea,Happy Kulanga alifariki Mkoani Iringa kuzikwa jana Iringa Mlandege.
 Katika uhai wake alikuwa na ziara ya Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi Salum Mnjagila mwenye kushika kitabu kwenye Miradi ya MUKEJA NA VICOBA  Subira Songea Manispaa.
Happy Kulinga mwenye suti ya bluu akipiga picha Seed Farm Manispaa ya Songea kwenye Miradi ya MUKEJA  na VICOBA wakati wa ziara hiyo.Mungu ailaze roho ya marehemu Kulanga mahali pema peponi Amin