Sunday, May 15, 2011

JUMAPILI NJEMA KWA WATU WOTE NI JUMAPILI YA KUHIMIZA MIITO MITAKATIFU KWA WATOTO WETU

 Padre Basley Malenda Paroko wa Parokia ya Ruhuwiko akitoa mahubili katika kigango cha Matarawe Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma,ahimiza miito kwa vijana ikiwemo Upadre,Utawa na Ndoa Takatifu.
u
 Muda wa kupeleka vipaji ulipo fika Padre Malenda alipokea vipaji hivyo.
Wapeleka vipaji walisindikizwa na kwaya ya Mtakatifu Anna wa Parokia ya Mjimwema Songea Manispaa na kwaya wenyeji ya Kigango hicho.

Wazaizi wawaruhusu watoto wao waingie kwenye miito ya Upadre,na Utawa,Padre Basley Malenda Paroko wa Ruwiko alisema hayo kwenye mahubiri yake katika Kigango cha Marawe Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma.
Alisema mavuno ni mangi ila wavunaji ni wachache,Mapadre ni wachache na walioko ni watu wazima hivyo vijana wanatakiwa kuingia kwenye wito huo wa uchungaji wa kondoo,maana mchungaji mwema huwajua kondoo zake kwa majina.
Padre Malenda alisema vijana wanakatishwa tama na wazazi kwa madai kuwa wakiingia upadre watakosa wajukuu na kutotoa huduma kwao hasa huduma ya kipesa.wengine ni vjiana wenzao wakiwa shuleni hasa akiwa na maendeleo huambizana kuwa achana na upadre nenda chuo kikuu upate kazi nzuri yenye kipato.
Amewaomba wazazi  wa Matarawe kuwaruhusu watoto wao waingie kwenye wito kwa kuwa wakazi wa Matarawe walimkatalia kuwa hawana Padre aliyetokea hapo.

1 comment:

  1. Ahsante sana kwa ujumbe huu. Ni ujumbe mzuri sana na kweli wazazi tunabidi tuwahamasishe watoto/vijana wetu. Kwani hawa waliopo sasa wanazeeka na kanisa /makanisa yanahitaji vijana.Amina.

    ReplyDelete