Friday, May 13, 2011

Wa-Tanzania ni watu wa kutisha kweli,Leo Mji wa Songea ulijaa watu viwanja vya Klbang'oma wakati Slaa,Mbowe na Zito walivyo wakusanya

Wakati jana Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi walikuwa na mkutano wao viwanja vya shule ya msingi Majengo Mjini hapa,basi watu walikuweko pale jana leo ni mara tano yake.Wlikwenda kuwasikiliza viongozi wa CHADEMA Walivyokuwa waki mwaga Sera yao na Ilani ya Chama chao.

Lakini kinacho nishangaza watu wa Tanzania ni wanafiki sana,kama kweli umati ule ungekipigia CHADEMA ukweli ushindi ungekuwa wao,Hata hivyo Chama Tawala wasizarau na kuwaona wanaokwenda kushabikia kuwa watarudia kaosa walilo lifanya uchaguzi mkuu uliyopita.

Mikutano hii inayofanywa na CHADEMA ambayo inakusanya wanachama wao,na si wanachama wao inawezekana na Wa CCM wamo katika mkusanyiko huo,Nivizuri sasa kujichunguza ili kuona kosa liko wapi,Isiwe tu ni kukosoana majukwaani TUMEFANYI HIVI mbona nyie MMEFANYA VILE ZAIDI YETU haitasaidia.

Si wakati sasa wa ChamaTawala kukosoana wenye kwa wenyewe ama kusoa vyama vya upinzani,kinacho takiwa kurudi kwenye mashina ya Chama na Matawi maana Chama bila wanachana kinakuwa hakina nguvu,hali ya zamani irudi naheshima ya Chama itaonekana kama ilivyo kuwa miaka ya 70.

No comments:

Post a Comment