Tuesday, May 10, 2011

UJENZI ENDELEVU KWA MAJENGO YOTE KATIKA SHULE NI MUHIMU SANA

Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo amesma Halmashauri zinapaswa kuwa na mipango ya kuhamasisha wananchi kuwa na ujenzi endelevu katika shule za msingi na sekondari kwa nyumba za walimu,vyumba vya madarasa,maabara,vyoo,utawala ili kuweka mazingira mazuri ya kufundisha na kujifunza.

Aidha amesema walimu wanaopangwa kwenye halmashauri hizo wapatiwe motisha kwenye nyumba watakazo anadaliwa mkiwemo umeme wa sola ili wawe sawa na wenzao waliomaliza nao mafunzo.alisema hayo kwenye kikao cha ushauri cha mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa Songea club jana.

No comments:

Post a Comment