Sunday, May 15, 2011

BREAKING NEWS!!! KICHAA ALIYEPELEKWA KWA BABU MCHUNGAJI LOLIONDO ASEMA FOLENI NI NDEFU BAADA YA KUPATA KIKOMBE

Imeshudiwa na watu waliyokwenda kwa mchungaji huyo kwa lengo la kupata kikombe,mara masai aliyekuwa kichaa alipelekwa pale amefungwa kamba.Babu akawaambia waliyempeleka kuwa wamfungulie kamba.wakafanya vile.Babu akampe kikombe baada ya hapo alipata usingizi.

Ushuhuda unasema baada ya kuamka kichaa huyo alimuuliza babu kuwa foleni bado ni ndefu?,babu alimjibu kuwa bado,watu walishangaa,mambo yanayotokea kwa babu Loliondo.Aidha babu anasema kama ni waathirika wa UKIMWI ni vyema kwenda wote mme na mke hakuna haja ya kufichana.

Alisema kikombe bado ni shilingi 500 kwa wa- Tanzania .wa - Kenya shilingi 1,200 na wageni wa Nje shilingi 1,500/=,Anasema hajaambiwa kuongeza bei kwenye tiba hiyo,wenye imani kwa Mungu wanapona.

No comments:

Post a Comment